ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 13, 2018

KOMBE LABAKI NYUMBANI TANZANIA - NI AZAM FC TENA MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI.



Na Salum Vuai, ZANZIBAR
AZAM FC imetwaa Kombe la Mapinduzi kwa mara ya pili mfululizo baada ya ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya URA ya Uganda kufatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 usiku wa leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein, shujaa wa Azam FC alikuwa ni mlinda mlango, Mghana Razack Abalora aliyecheza penalti mbili za wachezaji wa URA.

Abalora aliye katika msimu wake wa kwanza Azam FC tangu asajiliwe kutoka West African Football Academy (WAFA FC) ya Ghana alipangu penalty ya kwanza ya URA iliyopigwa na Parrick Mbowa nay a mwisho iliyopigwa na Brian Majwega.


Waliofunga penalti za Azam FC ni Nahodha Himid Mao, Yakubu Mohammed, Enock Atta Agyei na Aggrey Morris wakati Bruce Kangwa alimpelekea mikononi mpira kipa wa URA, Alionzi Nafian na penalti za URA zimefungwa na Charles Ssempa, Shafiq Kagimu na Jimmy Kulaba.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa mkongwe visiwani hapa, Mfaume Nassor aliyesaidiwa na Mbaraka Haule na Dalila Jaffar, dakika 90 zilikuwa ngumu timu zote zikishambuliana kwa zamu na ziwaendee makipa wa timu zote, Abalora na Alionzi Nafian kwa kuokoa vizuri.

Ushindi huu unamaanisha Azam FC wanatwaa Kombe la Mapinduzi kwa mara ya nne ya rekodi, baada ya awali kulibeba pia katika miaka ya 2012, 2013 na 2017 wakiipiku Simba SC ya Dar es Salaam iliyotwaa mara tatu 2008, 2011 na 2015. 
    
Yanga SC ndiye bingwa wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi mwaka 2007 wakati timu nyingine zilizotwaa taji hilo ni Miembeni mwaka 2009, Mtibwa Sugar mwaka 2010 na KCCA ya Uganda mwaka 2014.

Jumla ya timu 11 zilishiriki michuano ya mwaka huu ambazo ni URA, Jamhuri, Mwenge, Azam na Simba zilizokuwa Kundi A na Zimamoto, Mlandege, Yanga, JKU, Taifa Jan’gombe na Singida United zilizokuwa Kundi B.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Razack Abalora, Himid Mao, Bruce Kangwa, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Abdallah Kheri/Joseph Mahundi dk59, Stephan Kingue, Frank Domayo/Iddi Kipagwile dk58, Salmin Hoza, Bernard Arthur/Shaaban Iddi dk58 na Yahya Zayed/Enock Atta-Agyei dk64.

URA;Alionzi Nafian, Enock Kibumba, Brian Majwega, Allan Munaaba, Patrick Mbowa, Julius Mutyaba, Nicholas Kagaba, Kalama Deboss/Charles Ssempa dk66, Moses Sseruyide/Peter Lwasa dk81, Hudu Mulikyi na Shafiq Kagimu/Jimmy Kulaba dk82.

UVUVI HARAMU BADO TISHIO MKOANI MWANZA WANNE WABAMBWA.



Watu wanne wamenaswa pembezoni mwa Ziwa Victoria wakijihusisha na uvuvi uliopigwa marufuku na Serikali.

Uvuvi katika Ziwa Victoria ni shughuli kubwa ya kiuchumi na chanzo muhimu cha mapato kwa jamii husika na kampuni za kibiashara. Hali halisi ni kwamba jamii inayoishi kando ya Ziwa Victoria, inategemea uvuvi kama shughuli kuu za kiuchumi.

Licha ya umuhimu huo, kiwango cha samaki kinachotakiwa kubaki ziwani kimepungua kupita kiasi kwa miongo kadhaa. Tathmini ya kiasi cha samaki kinachotakiwa kubaki ziwani, iliyofanywa na Taasisi ya Uvuvi Ziwa Victoria (LVFO), inaonesha mwenendo wa kupungua kwa samaki sangara tangu mwaka 2000.

CCM HAKUNA SABABU YA KUFANYA KAMPENI 2020 TUNAHITAJI KUPITA BILA KUPINGWA: KHERI JAMES

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza na Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal

Wajumbe wa Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018. 

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James (Kulia) akieleza umuhimu wa wakazi wa Kata ya Kimandolu kumchagua Ndg Gaudence Limona kuwa diwani wao wakati akizungumza na Timu mbalimbali za kampeni kwenye kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018.
 Kikao kikiendelea
Wajumbe wa Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018. 


Na Mathias Canal, Arusha

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James amesema kuwa CCM haina sababu ya kufanya kampeni katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 badala yake kuna kila sababu ya kupita bila kupingwa kutokana na uimara wa CCM na serikali yake.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa ameyasema hayo Leo 12 Januari 2018 wakati akizungumza na Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu.

Kheri alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kutatua kero zote zisizo rafiki kwa wananchi kwa utekelezaji wa Mkataba wa wananchi na CCM kupitia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020.

Kheri aliwataka wananchi kujitokeza kwa mwingi kupiga kura hapo kesho 13 Januari 2018 kwani ni haki yao ya msingi kikatiba lakini pia aliwakumbusha kuwa katika uchaguzi huo wananchi wanapaswa kumchagua Diwani wa CCM kwa ajili ya maendeleo endelevu kwa ajili ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla wake.

Katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika kesho katika Kata ya Kimandolu Ndg Gaudence Limo ndiye mgombea wa CCM ambaye aliwahi kuwa Meya wa Jiji la Arusha.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti Kheri alivifananisha vyama vya upinzania nchini Tanzania na waharamia ambao kazi yao kubwa ni wizi na ujambazi, ujangili, udokozi, utapeli na uongo hivyo kupitia ulaghai wao haviwezi kufanikiwa kushika dola kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Aliwasihi vijana kukumbuka majukumu yao kama nguvu kazi ya Taifa kuwa ni pamoja na kusema ukweli, kuwajibika na kuwa watendaji na viongozi madhubuti sio viongozi biskuti.

Aidha, Kheri amewafikishia wakazi wa Arusha salamu za Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuwa anahitaji ushindi wa kishindo wa zaidi ya kura 12,000 na hiyo itakuwa zawadi pekee kwake.

“Ndugu zangu sisi wana CCM tunaweza kujadiliana harusi itafungwa vipi na wapi, tunaweza tukajadiliana aina ya magari ya kununua lakini hatuwezi kuwa na mjadala wa namna yoyote ile kwenye utafutaji wa dola ni lazima CCM ishinde” Alikaririwa Kheri.

SALAMU HIZI HAZIJACHELEWA TEREHE 12 JAN NI SIKU YA KUZALIWA KWA MDAU MUGANYIZI BISHEKO

 
Leo January 12, 2018 ni siku ya kuzaliwa kwa Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank of Africa Tanzania, Muganyizi Bisheko. Wote kwa pamoja tunapenda kukutakia heri na fanaka. Mwenyezi Mungu akujalie maisha marefu.


WAZIRI WA MAJI AWAAGIZA WAKANDARASI WA MAJI KUMALIZA MAPEMA MIRADI HIYO

Waziri wa maji na Umwagiliaji  Mhandisi ,Isack Kamwelwe akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Katoro pamoja na Buseresere wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi kwenye Wilaya ya Chato Mkoani Geita. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akimuomba Waziri wa maji na Umwagiliaji  Mhandisi ,Isack Kamwelwe kutatua changamoto ambayo imeendelea kuwepo kwenye baadhi ya maeneo katika Mkoa huo. 



Waziri wa maji na Umwagiliaji  Mhandisi ,Isack Kamwelwe akikagua baadhi ya miradi ya maji kwenye kijiji cha imalabupina wilayani chato. 




Na,Joel Maduka,Geita.

Waziri wa maji na Umwagiliaji  Mhandisi ,Isack Kamwelwe amewataka wakandarasi wa miradi mbalimbali ya maji kukamilisha miradi hiyo kwa wakati  ili  kuwaondolea wananchi changamoto ya ukosekanaji  maji ambayo imeendelea kuwakabili kwa muda mrefu  .

Mhandisi  Kamwelwe ameyasema hayo  wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani  Chato Mkoani Geita iliyokuwa na lengo la kukagua miradi ya maji inayotekelezwa wilayani  humo.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Katoro na Buseresere amesema matatizo ya maji katika miji ya Muganza, Buzirayombo na Buseresere yataanza kufanyiwa kazi na pindi tu usanifu wa mradi huu utakapokuwa tayari miradi hiyo itaanza kutekelezwa ili kumaliza kero kubwa ya maji.

Isack Saimon ambaye ni mkazi wa Buseresere amemuomba waziri kuharakisha zaidi mradi huo ambao ametoa ahadi kwa wananchi hao kwani kwasasa wameendelea kupata shida kubwa ya kupata maji na kwamba wamekuwa wakinunua ndoo ya maji kwa shilingi elfu moja hali ambayo inasababisha wasio na uwezo kushindwa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Gabriel Luhumbi amewasisitiza wakandarasi  wote wa miradi ya maji kutumia vibarua kwa wananchi wa maeneo husika ambapo miradi hiyo inatekelezwa.


Katika  Wilaya ya Chato jumla ya wananchi ambao wamekuwa wakuipata maji safi na salama ni  ni asilimia 41.

Friday, January 12, 2018

HERI YA MAPINDUZI KWA ZANZIBAR.

Jembe Fm  93.7 Kwenye Miaka 54 ya maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar Tumefika Pamoja #AsanteTanzania Maadhimisho haya ya Mapinduzi ya Zanzibar yawe kichocheo cha kuimarisha misingi ya undugu, umoja na mshikamano miongoni mwa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla.Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Zanzibar #AsanteTanzania #MapinduziDaima

RAIS MAGUFULI AMEAMUA KUSAFISHA NYUMBA HAKUNA MENDE ATAKAYEBAKI: KHERI JAMES

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido. Picha Zote Na Mathias Canal
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akionyesha fimbo ya kimasai baada ya kupewa cheo cha kiongozi wa kimila Olaigwanani rika ya Korianga akizungumza na wakazi wa akiwa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akisalimiana na wananchi wakati akiwasili Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akiwasili Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.

Na Mathias Canal, Arusha 

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa umesifu utendaji wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kutokana na uwajibikaji wake katika kuimarisha chama pamoja na serikali kwa maslahi ya watanzania.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor akiwa ziarani Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.

Kheri alisema kuwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa CCM Taifa ameamua kusafisha nyumba ambayo ni nchi ya Tanzania hivyo hakutegemewi mtu yeyote kusalia kama mende wa kumkwamisha katika umaridadi wa usafi huo wa maslahi ya Taifa.

Mjumbe huyo wa kamati kuu ya CCM Taifa aliwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi tarehe 13 Januari 2018 kupiga kura kwa wingi zitakazompa ushindi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt Steven Kiruswa ili kutekeleza ilani ya ushindi wa chama hicho ya Mwaka 2015-2020 ambayo ni mkataba muhimu kati ya wananchi na CCM.

Alisema kuwa serikali inapaswa kuchukua hatua Kali za kisheria dhidi ya yeyote atakayetaka kuvuruga ama kuleta uvunjifu wa amani Siku ya uchaguzi.

"Ndugu zangu wana Mrandarara nataka niwasihi na kuwahakikishia kuwa MTU yeyote atakayeleta masihara na mchezo mchezo Siku ya uchaguzi anapaswa kuchezewa yeye mchezo mpaka ashike adabu" Alikaririwa Kheri

Alisema kuwa Mara baada ya Mbunge kuchaguliwa tu anapaswa kusimamia vyema asilimia 5% za fedha za mfuko wa vijana zinazotolewa na Halmashauri sambamba na asilimia 5% kwa ajili ya wanawake ili kuendeleza chachu na imani ya vijana na wananchi kwa ujumla dhidi ya serikali yao.

Aliongeza kuwa kumchagua mbunge wa CCM itampendeza zaidi Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe Magufuli kwani atakuwa amepata msaidizi kwa ngazi ya Jimbo atakayetekeleza vyema ilani ya CCM ambayo imeainisha mambo mengi muhimu na msingi kwa maslahi ya watanzania wote hasa wananchi wa Longido.

Uchaguzi wa Ubunge Jimbo la Longido na majimbo mengine matatu likiwemo Jimbo la Singida Kaskazini na Songea Mjini utafanyika tarehe 13 Januari 2018.

Wakati huo huo akiwa Kijijini Mairowa Kata ya Ngarenaibor Mwenyekiti Kheri amewataka mawakala wa CCM kote nchini kuwa waaminifu katika kusimamia vyema chaguzi mbalimbali kote nchini kwani wameaminiwa na Chama hivyo kutojihusisha na viashiria vya aina yoyote ya rushwa.

Thursday, January 11, 2018

OFISA ARDHI MBARONI KWA KUFANYA UTAPELI MWANZA.

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu sita akiwemo Ofisa Ardhi wa Manispaa ya Ilemela, Alex Nyabange (30), kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo utapeli wa viwanja, kutengeneza vyeti bandia vya kitaaluma pamoja namba za mlipa kodi za (TIN), za Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Alhamisi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema watu hao walikamatwa kwa nyakati tofauti kati ya Desemba 30, 2017 na Janauari 9 mwaka huu.

Msangi aliwataja waliokamatwa kwa tuhuma za kuwatapeli watu kwa madai ya kuwauzia viwanja kuwa ni Aloyce Nyabange (30) ambaye ni ofisa Ardhi wa  Manispaa ya Ilemela, Alex Josephat(41) ambaye ni mfanyabishara, Juma Malulu (60) mkazi wa mta wa Ilemela.

Wengine ni Katibu Mhatasi wa kampuni ya Nyambale Civil Works, Getruda Peter (42) mkazi wa Nyegezi na mchora ramani Deodatus Bety (51) mkazi wa Usagara ambao wote walikamatwa Desemba 30, 2017 kwa nyakati tofauti.

“Tulipata taarifa hizi baada ya mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Barnabasi Ibengo (39) mfanyabishara wa Kiseke kuwa ametapeliwa na watu waliosema wana viwanja viwili eneo la Nyasaka na kwamba vinahitaji Sh45 milioni, lakini akawa ametanguliza Sh10 milioni akiamini kuwa ni ukweli kutokana na nyaraka zote walizomuonyesha,” amesema Msangi.

Hata hivyo Msagi amesema mfanyabishara huyo, aligundua kuwa ametapeliwa baada ya kwenda eneo vilipo viwanja hivyo na kuonana na mwenyekiti wa mtaa huo na kuaambiwa hakuna jambo la namna hiyo ndipo alitoa taarifa polisi na kuanza kufuatilia kukamatwa mmoja baada ya mwingine.

Alisema watuhumiwa hao walikutwa na komputa inayotumika kutengenezea nyaraka mbalimbali na baadhi ya nyaraka zinazoonyesha viwanja kwa ajili ya kuuzwa.

Kuhusu vyeti feki Kamanda Msangi amesema walimkamata Evancy Wilson (33) katika mtaa wa Buzuruga Ilemela akiwa na vifaa vya kughushi vyeti vya taaluma mbalimbali.

Amesema tukio hilo lilitokea Janauri 9, mwaka huu saa 11:00 jioni ambapo mtuhumiwa baada ya kukamatwa na kuchunguzwa kwenye kompyuta yake walikuta namba inayofanana na TIN ya TRA na vyeti hivyo vya taaluma vya kughushi.

Amesema walikuta vyeti vya kughushi vya, stashahada, shahada, vyeti, vitambulisho vya mpigakura, nyaraka zinazoonyesha kuwa ni za kuombea mikopo benki, leseni za biashara na flash ambazo zimejazwa vitu hivyo.

“Hili lilitokana na taarifa tulizopata kutoka kwa raia wema kuhusu kuwapo kwa mtu anayetenegeza vitu hivyo ndipo tulianza kufuataili, watuhumiwa wote wapo polisi, upelelezi ukikamilika tutawafakisha mahakamani.

JENGO LA BENKI KUU TAWI LA MWANZA AL- MANUSURA KUTEKETEA NA MOTO



Jeshi la Uokaji Zimamoto Mz mapema asubuhi ya leo limefanikiwa kuudhibiti moto uliozuka kutoka chumba kimojawapo kilichopo ghorofa ya pili ndani ya jengo la Benki Kuu Tawi la Mwanza, lililoko katika barabara ya Nyerere jijini hapa.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Kamanda wa Zimamoto mkoa wa Mwanza Andrew James Mbate amezungumza nasi juu ya chanzo na harakati zao. 

#KAZINANGOMA ya 93.7 @jembefm inamzigo mzima.

SHUHUDIA MIKWAJU YA PENATI ILIYOITUPA NJE YA MAPINDUZI CUP (URA vs YANGA)



Yanga wametupwa nje ya michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar kwa mikwaju ya penati 5-4 na URA ya Uganda baada ya kumaliza dakika 90 bila bao.

SAKATA LA KUJIUNGANISHIA BOMBA LA MAFUTA WATU WA 5 WATIWA MBARONI.

Jeshi la Polisi limewakamata watu watano, akiwemo mwalimu wa Shule ya Msingi ya Kisiwani Kigamboni, Lebeka Nganji kwa kujihusisha na uuzaji wa mafuta ya dizeli yanayosadikiwa yalitoka katika bomba lililounganishwa kwa wizi.


Inadaiwa kuwa bomba hilo liliunganishwa na Samwel Kilanglani (63), ambaye nyumba yake iko umbali wa takribani mita 20 kutoka lilipo bomba kuu la mafuta la Tanzania na Zambia (Tazama).

Kilanglani anadaiwa kujichotea mafuta kutoka katika bomba hilo alilolipitisha chini ya ardhi.

Imedaiwa kwamba mfanyakazi huyo mstaaafu wa Tazama alianza kutoboa bomba la kwanza na kukuta lina mafuta ghafi na kuliziba, kisha kutoboa jingine lililokuwa na dizeli na kujiunganishia hadi nyumbani kwake.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Benedict Kitalika aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Bariki Dickson, Christon Kapinga na Farhan Ahmed ambao wote wanaishi Kigamboni.

Alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na Kilanglani kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kuwataja wenzake ambao huchukua na kuuza mafuta hayo.

“Huyu mtuhumiwa alisema hayupo peke yake hivyo ana wenzake wanashirikiana dili hilo, ndiyo akawataja hao wanne akiwemo mwalimu wa Shule ya Msingi Kisiwani,” alisema.

“Tuliwakamata watuhumiwa sehemu mbalimbali za Kigamboni ambao wote wanafanya dili hilo la kunyonya na kuuza mafuta ya dizeli kutoka kwenye bomba kuu,” alisema Kitalika.

Juzi mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa alieleza kuwa Kilanglani alibainika baada ya mafuta yaliyokuwa yanavuja kuanza kusambaa barabarani.

Mgandilwa alisema Januari 6, walipelekewa taarifa kuwa mafuta yamesambaa kwenye njia ya mabomba ya Tazama yanayopita Tungi, Kigamboni.

Alisema baada ya kupewa taarifa hizo walienda hadi eneo hilo na kuamua kuchimba ili kubaini tatizo.

“Awali tulihisi bomba kubwa limepasuka. Tuliamua kuchimba ili kuyakabili mafuta yasiweze tena kuvuja na kuwasababishia athari wananchi,” alisema.

Alisema wakati wakiendelea na kazi hiyo, walikuta mabomba makubwa matatu ya mafuta, mawili yalikuwa yametobolewa; moja likipitisha mafuta ghafi ambalo lilionekana kuwa limezibwa.

“Bomba jingine ambalo lilikuwa la mafuta ya dizeli lilikuwa limeunganishwa kwa chini ya bomba jingine dogo kwa kutumia koki, tulivyofuatilia tukabaini limeelekea nyumbani kwa Kilanglani,” alisema.

“Huyu mtuhumiwa ni mtaalamu sana. Mtu  wa kawaida hawezi kuunganisha chini kwa chini, ndiyo maana alipogundua bomba la kwanza linatoa mafuta machafu akaziba na kutoboa jingine lililokuwa na mafuta ya dizeli.

“Mafuta yanaposhushwa kwenye meli hupita katika mabomba kwa kusukumwa na mashine kuelekea kituo cha kuhifadhia cha Tazama. Mabomba hayo yamepita karibu na nyumba yake.”

Wednesday, January 10, 2018

MSIBA MZITO WANAHABARI MWANZA KWAHERI ZUBER MSABAHA


Safari ya mwisho ya mwanahabari aliyekuwa mtangazaji wa Radio Free Afrika, Zubeir Msabaha imewahuzunisha wengi wadau si wananchi wa kawaida pekee bali pia hata wadau wenyewe wa tasnia ya habari (wandishi wa habari) wameonekana kuguswa na msiba huo.

Kazi na Ngoma ya Jembe Fm imezungumza na baadhi yao.

Na hiki ndicho walichosema.

KURA YA LOWASSA HAINA ATHARI ZOZOTE KWA UCHAGUZI 2020 ASEMA MCHAMBUZI EDWIN SOKO.


Suala la Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Mhe. Edward lowassa kukutana Ikulu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli limezua mijadala huku watu wakitoleana mapovu nao waungwana wakitoa maoni yao mbalimbali.

Kazi na ngoma ya Jembe Fm leo imezungumza na Mwenyekiti wa Chama cha kupambana na kuzuia matumizi ya madawa ya kulevya nchini OJADACT ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya siasa na kijamii Bw. Edwin Soko.

MVUA KUBWA ZAIDI ZAJA.

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema mvua zilizonyesha juzi katika Ukanda wa Pwani na kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo, ikiwamo jijini Dar es Salaam, zipo nje ya msimu na zinatarajiwa kunyesha kwa vipindi katika mwezi huu.

Aidha, imeeleza mvua hizo zinasababishwa na kimbunga ‘Alva’ ambacho kinatoka eneo la Mashariki mwa kituo cha Madagascar kuanzia Januari 3, mwaka huu na kuongeza unyevunyevu pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa Bahari ya Hindi.

TMA imesema mikoa inayopitiwa na mvua hizo ni ya ukanda wa Pwani ya Kaskazini ikiwamo Pwani, Tanga, Dar es Salaam na iliyopo ukanda ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, ikiwamo Manyara, Kilimanjaro na Arusha.

Meneja wa Kituo Kikuu cha Utabiri cha TMA, Samuel Mbuya, aliiambia Nipashe jana kuwa tahadhari inapaswa kuchukuliwa kwa wasafiri katika Bahari ya Hindi kwa kuwa mwezi wa Januari kuna hali ya joto la bahari eneo la Magharibi kuathiri ukanda huo.

“Kwa kipindi cha Januari mwaka huu mvua hizi zitaendelea ambazo zipo nje ya msimu, Dar es Salaam ikiwamo, hii ni kutokana na joto la Bahari ya Hindi katika eneo la Magharibi,” alisema Mbuya.

Pia katika mikoa ya ukanda wa kati Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma Katavi, Rukwa na Nyanda za Juu Kusini Mashariki, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma na Mtwara yataendelea kupata mvua za msimu hadi mwezi ujao.

Mvua zilizoanza kunyesha mwishoni mwa wiki kanda ya Pwani ikiwamo jijini Dar es Salaam, zilisababisha athari katika maeneo kadhaa ikiwamo wananchi kukosa makazi na kusitishwa kwa muda kwa usafiri wa mabasi yaendayo haraka, maarufu mwendokasi.

Wakazi wanaoishi maeneo ya mabondeni ni kati ya waathiriwa hao kutokana na mvua kuzingira makazi huku barabara kadhaa zikijaa maji kutokana na mitaro na kusababisha msongamano wa magari

kwa waliokuwa wanakwenda kazini, sehemu za biashara, maeneo mengine na wanafunzi waliokuwa wanakwenda shuleni.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Benedict Kitalika, katika taarifa yake juzi aliwataka wakazi wa mabondeni kuhama mara moja bila kusubiri kukumbwa na mafuriko.

“Badala ya kuendelea kuishi katika maeneo hatarishi wakisubiri kuondolewa na serikali, wahame haraka kunusuru maisha yao na wasirudi tena katika maeneo hayo,” alisema Kitalika.

ZUBEIR MSABAHA HATUNAYE TENA.

Aliyekuwa mtangazaji wa muda mrefu wa Radio Free Africa, Zuberi Msabaha amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatano Januari 10, 2018,  jijini Mwanza.

Zuberi Msabaha alikuwa ameugua kwa muda mrefu huku akipatiwa matibabu yake sehemu tofauti tofauti hapa nchini. Msiba wake upo Mabatini jijini Mwanza na mazishi yatafanyika Jumatano yaani leo.

Marehemu Zuberi Msabaha alijijengea umaarufu mkubwa kupitia kipindi chake cha Bolingo Time kinachorushwa hewani na kituo cha Radio cha RFA.

Zuberi Msabaha alikuwa mchambuzi mzuri sana wa muziki wa Dansi hasa muziki wa Kongo ambao mara nyingi unaimbwa kwa lugha ya Kilingala, Kikongo, kikasai, na Kifaransa.

Mungu ailaze Mahali Pema Peponi Roho ya mpendwa wetu Papa Zuberi Msabaha. R. I. P 
#KAZINANGOMA ina kuja na habari zaidi.

Tuesday, January 9, 2018

BREAKING NEWS:- MAGUFULI USO KWA USO NA LOWASSA:


Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowassa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo Bw Lowassa amempongeza Dkt Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu.

“Nimepata faraja sana kuja hapa Ikulu kuonana na Mhe. Rais, tumezungumza nae na nimempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya, lazima tukiri anafanya kazi nzuri na anahitaji kutiwa moyo.”

Picha/Ikulu, Tanzania #magufuli #ikulu #lowassa #tanzania #JembeHabari @harithjaha




SHAKA AWASILI SINGIDA LEO,KUMNADI MGOMBEA UBUNGE WA CCM SINGIDA KASKAZINI.

 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka (Kulia) Akipeana mkono na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Ndg:Peter Monko  Alipowasili katika Ofisi za CCM Mkoa wa Singida leo.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka akisain kitabu cha wageni  katika Ofisi za CCM Mkoa wa Singida (kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Ndg Juma Kilimba.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi  dkt. Denis Nyiraha akimkaribisha  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka alipowasili katika ofisi za CCM Mkoa wa Singida.
''Tutashinda na tutashinda kwa sababu mtaji wa ushindi tunao lengo ni lile lile kuhakikisha Singida kaskazini inaendelea kuwa ngome ya CCM''Alisema Shaka wakati akizungumza na Viongozi wa CCM Alipowasili katika ofisi za CCM Mkoa wa Singida leo.
(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)

RIPOTI: KILA SAA MOJA MWANAFUNZI MMOJA HUJIUA NCHINI INDIA, SERIKALI YASHTUSHWA

Ripoti: Kila saa moja mwanafunzi mmoja hujiua nchini India, serikali yashtushwa
Takwimu iliyotolewa na serikali ya India ni ya kushtua baada ya kuonyesha kwamba, ndani ya kila saa moja mwanafunzi mmoja hujiua nchini humo.
Gazeti la Times of India limeandika kuwa, idadi ya vijana wanaojiua imezidi kuongezeka kiasi cha kuwafanya viongozi wa serikali ya nchi hiyo kuanza kuzitahadharisha familia. Kwa mujibu wa takwimu za mwisho zilizotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya India kuhusiana na suala hilo, sababu ya vijana wengi kujiua ni utumiaji wa madawa ya kulevya, matatizo ya kisaikolojia yanayosababishwa na kuachana wazazi wawili, kugombana na watu wakubwa, masuala nyeti na matatizo yanayohusiana na masomo.
Ongezeko la kujinyonga kati ya vijana nchini India
Aidha ripoti hiyo imeeleza kuwa, idadi ya wanafunzi waliojiua mwaka 2016 pekee ilikaribia 9500 ambapo inaonyesha kwamba, karibu kila saa moja, hujiua mwanafunzi mmoja. Kadhalika ripoti hiyo, imeyataja majimbo ya Maharashtra na Bengal kuwa yanayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiua. Weledi wa mambo nchini humo wanaamini kwamba, mabadiliko ya haraka katika jamii ya India yamekuwa na taathira hasi kwa vijana wa nchi hiyo ambapo kutokana na kutokuwa na uwezo wa kufanya mawasiliano chanya na watu wa familia na marafiki zao, huamua kujiua.
Kukosekana usawa katika ugawaji pato la taifa kunawafanya raia wengi kuwa masikini
Hii ni katika hali ambayo India pia inaongoza kwa kuwa na kiwango cha juu cha vijana wanaojiua duniani. Weledi wa mambo wanaamini kwamba kabla ya serikali kutatua tatizo la kisaikolojia kwa vijana, inatakiwa kwanza kushughulikia hali ya uchumi na kutatua matatizo ya kijamii nchini humo.
KWA HISANI YA  http://parstoday.com/sw/news/world

Monday, January 8, 2018

YANGA YATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI MSIBA WA ATHUMAN CHAMA.

Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Mkwasa ametuma salama za rambirambi kwa familia ya marehemu Athmani Juma Chama ‘Jogoo ‘ kufuatia kifo cha nyota huyo wa zamani wa Yanga kilichotokea katika hospital ya Muhimbili Jana usiku.
Enzi za uhai wake Athman Juma Chama 'Jogoo'

Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Mkwasa ametuma salama za rambirambi kwa familia ya marehemu Athmani Juma Chama ‘Jogoo ‘ kufuatia kifo cha nyota huyo wa zamani wa Yanga kilichotokea katika hospital ya Muhimbili Jana usiku..
Kutoka kushoto waliosimama: Godwin Aswile, Issa Athumani, Dotto Mokili, Said Zimbwe “Terry Butcher”,  Mohamed Rashid, John Bosco, Abeid Mziba, John Manyika (Daktari) na John Mgombelo (meneja).

Waliochuchumaa kutoka kushoto: Juma Pondamali, Athumani Chama ‘Jogoo’ Fred Felix Minziro, Athumani China, Muhesa Kihwelo, Aboubakar Salum ‘Sure Boy’, John Alex, Justin Mtekere na Sahau Kambi.

“Nawaomba wana yanga wote tuungane kwa pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu” Chama alikuwa mchezaji mahiri wa Yanga na alifanya mengi mazuri kwa timu na Taifa enzi za uhai wake”- Mkwasa.

BONDIA VICENT MBILINYI ATAMBA KUMSAMBARATISHA AMANI BARIKI FEB 14 MOROGORO

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimwelekeza jinsi ya kupiga ngumi ya mkunjo wa chini 'Up Cut' wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake na Aman Bariki utakaofanyika Feb 14 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro 
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimwelekeza jinsi ya kupiga ngumi ya mkunjo wa chini 'Up Cut' wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake na Aman Bariki utakaofanyika Feb 14 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandisahi Wetu

BONDIA Vicent Mbilinyi ameingia kambini kwa ajili ya mpambano wake na Amani Bariki 'Manny Chuga' mpambano wa raund 8 utakaofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro Feb 14 mpambano uho utakwa wa utangulizi kabla ya mpambano mkubwa utakaowakutanisha

Twaha Kiduku wa Morogoro na Chiota Chimwemwe wa Malawi mpambano wa raundi 10 mpambano uho wa kimataifa utawakutanisha mabondia hawo baada ya kila mmoja kucheza mpambano mmoja na kushinda na kufanikiwa kukutanishwa kwa viwango vyao

Bondia Mbilinyi anaenolewa na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  amejinasibu kuwa atacheza kufa na kupona kwani njia ya kuelekea mafanikio yake itakuwa ni hiyo kwa kuwa yeye ni bondia mzowefu ivyo Bariki awezi kumsumbua ata kidogo ajiandae na kipigo cha mbwa mwizi siku hiyo si ya mchezo mchezo nitacvheza kufa na kupona alisema Mbilinyi

nae promota wa mpambano uho Kaike Silaju amesema ameamuwa kuandaa mpambano huo mjini Morogoro baada ya kuombwa na mashabiki wa mkoa wa morogoro nae bila hiyana nikamua kuleta mpambano huu kwa mara ya kwanza wayu washamzoea Fransic Cheka sasa huyu ndio atakae mrithi Cheka kwabi Kiduku ni bondia bora sana mchini Tanzania hivyo mashabiki mjitokeze kwa wingi mje mshudie mpambano wa kufungulia mwaka

mbali na mchezo wa masumbwi siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbalio ambapo kutakuwa na wasanii nao wataoneshana umwamba ambapo Vicent Kigosi 'Ray' atapambana na Jacob Stevin 'JB' uzito wa juu ivyo siku hiyo si yakukosa


Siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd.


Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani