ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 18, 2018

ZIARA YA WAZIRI WA MAJI JIJINI MWANZA IMEKUJA NA HAYA.

NA ZEPHANIA MANDIA . 
Wizara ya maji na umwagiliaji imesema kuwa, tatizo la maji safi linalowakabili wananchi waishio kwenye maeneo ya miinuko Jijini Mwanza litamalizika ifikapo novemba mwaka huu, baada ya kukamilika mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma ya maji katika maeneo hayo.
Akizungumzia malengo hayo baada ya kutembelea mradi huo unaotarajiwa kugharimu shilingi billioni 34, Waziri wa Maji na umwagiliaji Mhandisi Isack Kamele, ameiagiza Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mkoa wa Mwanza (Mwauwasa) kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Waziri huyo ametoa agizo hilo ili kuwaondolea kero ya maji zaidi ya wananchi laki moja waishio kwenye maeneo yenye miinuko Jijini Mwanza, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ya kuhakikisha kuwa  wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama.

MHANDISI ISACK KAMELE - Waziri wa Maji na umwagiliaji.
Kutokana na mkakati huo dhamira ya Serikali  ni kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa asilimia 95 ifikapo mwaka 2020 katika maeneo yote nchini, ambapo Jijini Mwanza utekelezaji huo umeanza kutekelezwa kwa ufanisi.
 Mradi wa Maji kwenye miinuko Jijini utagharimu shilingi billioni 34, ukihusisha shughuli mbalimbali zikiwemo za ujenzi wa matenki sita yenye ujazo wa lita miilioni 4,850,000, kutandaza mabomba ya kusafirisha na kusambaza maji na kuboresha mtandao wa maji taka.
 Awali akitoa taarifa ya mradi huo kwa Waziri wa Maji na umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwele, Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Jijini Mwanza(Mwauwasa)Mhandisi ANTHONY SANGA, amesema  kuwa utawanufaisha zaidi ya wakazi laki moja.
 Meneja mradi wa huduma ya Maji Jijini Mwanza.

Kukamilika mradi wa huduma ya maji kwenye maeneo ya miinuko, kutasaidia upatikanaji wa Maji Jijini Mwanza kutoka asilimia 90 hadi 95 ifikapo mwaka 2019, kiwango ambacho kitatatua changamoto iliyopo sasa 


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.