ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 28, 2017

RAY: OKWI HAWEZI KUIFUNGA YANGA


Vincent Kigosi ‘Ray’.

MSANII wa Bongo Movie’s, Vincent Kigosi ‘Ray’ amewaambia mashabiki wenzake wa Yanga kuwa, wasihofi  mabao ya Emmanuel Okwi wa Simba, kwani huwa anazifunga timu ndogo tu.

Yanga leo Jumamosi inacheza na Simba kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam mechi ya Ligi Kuu Bara raundi ya nane.

Mpaka sasa Okwi ndiye kinara wa mabao akiwa nayo nane.

Ray alisema: “Yanga ipo vizuri kila idara hivyo na ninaamini haitatuangusha kwenye mchezo huu ingawa wapinzani wanapiga kelele za Okwi, watambue kuwa huyo haiwezi Yanga.

“Okwi anaonekana katika mechi ndogo lakini katika mechi kubwa anafunikwa hivyo wasitegemee jipya kutoka kwake.”

WIZARA YA MADINI NA YA ARDHI KUHAKIKI UPYA MADAI YA FIDIA BUCKREEF.

Waziri wa Madini,Bi Angellah Kairuki akiwa na Meneja wa Mgodi wa Buckreef Peter Zishoo(Katikatika) na pembeni ni Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM)Mkoani Geita Joseph Kasheku Msukuma wakati walipotembelea baadhi ya maeneo ya Mgodi Huo.
Waziri wa Madini,Bi Angellah Kairuki akiwa na mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi wakati wa kikao na wabia wa mgodi wa Buckreef alipotembea kwa lengo la kujadili namna ambavyo wanatakiwa kuanza kazi za uchimbaji kwenye mgodi huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita na Mbunge Joseph Kasheku Msukuma akiwa kwenye kikao hicho wakati alipokuwa akichangia hoja ya fidia kwa wananchi wa kata ya Busanda na Kaseme.
Mjiolojia wa mgodi huo Bw Anthony Minde,akisisitiza kutokuafikia swala la kuwalipa fidia baadhi ya wananchi.
Waziri wa Madini,Bi Angellah Kairuki akisisitiza kupereka taarifa hiyo kwenye Wizara ya ardhi kwaajili ya kutathimini kwa upya maeneo hayo.
Baadhi ya wajumbe waliokuwepo kwenye Kikao hicho.

PICHA NA MADUKA ONLINE.


Wizara ya madini kwa kushirkiana na wizara ya ardhi inatarajia kufanya uhakiki upya kwenye Mgodi wa Buckreef ili kuwalipa fidia wananchi wa kata za Busanda na Kaseme ambao wamekuwa wakidai fidia kwa muda mrefu kwenye mgodi huo.

Hatua hiyo imetokana na kutokuwepo kwa maelewano baina ya wabia wa Mgodi huo ambao ni Kampuni ya Tanzam 2000  inayomiliki asilimia 55 huku asilimia 45 zikimilikiwa na shirika la madini nchini (STAMICO) waliogoma kulipa deni hilo kutokana na kutokuwa na uhakika na madai hayo na kutokuwa na leseni.

Mjiolojia wa mgodi huo Bw Anthony Minde alisema hakukuwepo mgogoro wowote kwani mkataba wa uthamini ulisainiwa na mkuu wa wilaya pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita wakati huo, hivyo suala la kulipa fidia linakuwa gumu kwa upande wao.

“Nafikiri waliosema kwamba walikuwepo ni kwamba Afisa wa Serikali na ni wa Shinyanga, tuliletewa baada ya kuomba kwamba hii tathmini ifanywe na mtu wa serikali ikaidhinishwa na kusainiwa kwenye ngazi ya wilaya na mkoa kabla ya kuletwa kwetu ili tuisome kuona kama iko sawa, Tunamshangaa Mbunge anaposema ripoti hiyo haikusainiwa” Alisema Minde.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoani Geita Bw Joseph Msukuma aligoma kukubaliana na taarifa hiyo na kudai kuwa walipeleka mthamini ambaye hakuripoti kwenye Halmashauri ya wilaya ya Geita na kwamba walikuwa wakifanya uthamini huku wakiwanyang’anya marudio wananch.

“Walileta mthamini kutoka Shinyanga ambaye hakuripoti kwenye Halmashauri ya wilaya ya Geita, ulipotokea mgogoro pale Kaseme tukaja, mlikuwa mnafanya uthamini mnanyang’anya na marudio ya wananchi, ndo wananchi wakagoma likasimamishwa hilo zoezi, huyo aliyekuja kurudisha kwenye ngazi ya Halmashauri ni nani aliyeridhia? Na kama kweli mlifanya uthamini hawa asilimia mia moja wametokea wapi?” Alisema Msukuma.

Waziri wa Madini Bi, Angellah Kairuki amechukua uamuzi wa kupeleka madia hayo kwenye wizara ya ardhi na kwamba atamueleza Waziri husika kurudisha wathamini wake kwa mara nyingine ili kujiridhisha kwa kila mwananchi kama anaumiliki halali wa eneo analoliombea fidia.

“Sasa mimi uamuzi wangu ni kwamba, kama Serikali tutakaa tutalipeleka suala hili wizara ya ardhi kupitia kwa waziri wa ardhi ili aelekeze wataalam wake, wathamini wake tena kurudi kwenye jina moja baada ya jingine katika majina hayo elfu moja na sitini na mbili kila mmoja kuweza kujiridhisha eneo lake ni lipi na kama kweli ana umiliki nalo ili baada ya hapo sasa kama wao walikuwa wamesema hawawezi kulipa kwa sababu hawana uhakika na orodha kamili tutakuwa tumelimliza na wasipolipa tutakuwa tumejua nia yao sio nzuri” Alisema Kairuki.

DC MTATURU AZINDUA MSIMU WA KILIMO 2017/2018


Na Mathias Canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu amezindua msimu wa kilimo 2017/18 ikiwa ni Sehemu ya kuwasihi wananchi kuanza kujiandaa kwani tayari wakati wa kuanza kilimo umekaribia.

Katika uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji na kata ya Ihanja wilayani Ikungi Mhe Mtaturu pamoja na  mambo mengine lakini amewasihi kutumia vizuri mvua za mwanzo kupandia.

Katika mkutano huo wa uzinduzi  Mhe Mtaturu pia ameanzisha utaratibu huo wa kuzindua msimu wa kilimo kila mwaka ili kuwaandaa wakulima kuingia msimu mpya mapema ikiwemo kuyakumbusha makampuni ya mbegu kuwafikishia wakulima mbegu kabla mvua kuanza kunyesha.

Sambamba na utaratibu huo wa kuzindua msimu wa kilimo kila mwaka  pia kutakuwa na zoezi la kufanya maonesho ya zana na teknolojia mbalimbali za kilimo ili wakulima wapate muda wa kujifunza mbinu mpya za kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

Mhe Mtaturu aliwaagiza maafisa ugani kuwa na mashaba darasa na madaftari ya wakulima sambamba na  kuwaunganisha wakulima hao na makampuni ya mbegu ili waweze kupanda mbegu bora zikiwemo zile zinazokomaa kwa muda mfupi.

Aliwakumbusha wakulima wote kulima mazao ya chakula ili kuwa na usalama wa chakula ambapo aliyataja mazao hayo ambayo yanastahili hali ya ukame kuwa ni pamoja na Mtama, uwele, Mpunga, viazi lishe,viazi vitamu na mihogo.

Pia aliwataka wakulima kulima mazao ya biashara ili kuwa na uchumi imara huku akitikisa msisitizo  zaidi katika mazao ya kipaumbele katika wilaya hiyo ambayo ni Korosho, Pamba na Alizeti.

Mhe Mtaturu aliwahakikishia wananchi kupanda mbegu mapema za korosho na dawa za kupulizia ili kuua vijijidudu vinavyoshambulia.

Alisma kuwa tayari Wilaya ya Ikungi imepokea Mbegu Tani 20 za Pamba ambazo zitaanza kusambazwa wiki ijayo kwa wakulima waliojiandikisha.

Akisoma taarifa ya idara ya kilimo kwa Mkuu wa Wilaya, Kaimu afisa kilimo Wilaya  ya Ikungi Ndg Teendwa Senkoro alieleza lengo la wilaya hiyo ku ni kulima hekta 124,038 za mazao mbalimbali katika msimu wa mwaka 2017/18 na kuvuna tani 208,700 za mazao mbalimbali.

Mhe Mtaturu ametimiza ahadi yake ya kuanzisha msimu wa kilimo aliyoahidi hivi karibuni wakati alipofanya kikao kazi na wakuu wa Idara na Vitengo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe Ally Mwanga alimpongeza Mhe Mtaturu kwa juhudi zake mbalimbali za kimaendeleo anazozifanya katika Wilaya hiyo tangu ateuliwe kuhudumu katika nafasi hiyo. 

Alisema kuwa waheshimiwa Madiwani na Halmashauri wataendelea kumuunga mkono katika jitihada hozo ili kuwasaidia wananchi kujiletea maendeleo.
 

Wednesday, October 25, 2017

DAS CHINTIKA: WALIMU TUMIENI KONDOMU ILI KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

Katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka akiwa kwenye mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa akizungumza na baadhi ya walimu walihudhuria mkutano huo.
Baadhi ya walimu waliokuwa wanaimba wimbo wa walimu wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa uliofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.

Na Fredy Mgunda,iringa. 

Walimu wa halmashauri ya manispaa ya Iringa wametakiwa kutumia kondomu ili kujikinga na magonjwa ya zinaa amboya yamekuwa yakipunguza nguvu kazi ya taifa.

Hayo yamesemwa na katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa.

Chintinka alisema kuwa kumekuwa na ongezeko la waathirika wa ugonjwa wa ukimwai kutokana na kufanya mapenzi bila kutumia kondomu.

“Jamani hapa Iringa kuna tatizo kubwa la ugonjwa wa ukimwi hivyo niwaombe walimu wangu tutumie kondomu ili kujiepusha na gonjwa hili vinginevyo vizazi vyetu vyote vitaambukizwa ukimwi” alisema Chintinka

Chintinka alisema njia ya kuwa salaama kuepukana na gonjwa hili ni kujikinga kwa kutumia kondomu maana hata watoto wetu wameathirika kutokana na wazazi kutokuwa makini na matumizi ya kinga

“Naombeni tuwakinge hawa watoto wetu ambao wameathirika ili wasiwaambukize watoto wengine maana bila hivyo tutakuwa na kizazi kilichoathirika” alisema Chintinka

Aidha Chintinka aliwaomba walimu walioathirika kujitokeza ili kupewa lishe ambayo inatolewa na serikali bure hivyo walimu wametakiwa kujitokeza na kuweka wazi kwa mwagili wake ili aweze kupata mgao wa pesa za lishe.

“Jamani walimu fungu la lishe kwa walimu walioathirikia ni nono kweli naombeni walimu mjitokeze ili mfaidi fungu hili nono maana mimi nafahamu sisi ndio tunaotenga naombeni fikisheni ujumbe huu kwa walimu wengine ambao hawajafika hapa” alisema Chintinka

Chintinka aliwataka watumishi wanaotoa siri za watumishi walioathirika kuacha tabia hiyo mara moja ili kuwaweka huru waathirika na wengine waweze kujitokeza na wapate lishe iliyotengwa na wilaya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho manispaa ya Iringa MWL. Zawadi Mgongolwa alikiri kuwepo kwa viongozi wa sekta hiyo ambao wemekuwa wakitoa siri za walimu na watumishi walioathirika na ugonjwa wa ukimwi.

Kwa kweli mgeni rasmi umeongea ukweli kero kubwa kwa walimu ni kutolea siri nje kitu kinachowafanya walimu waathirika kujificha na maradhi yao” alisema Mgongolwa

Naye katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale alimpongeza mgeni rasmi kwa ujumbe wake ambao umekuwa faraja kwa walimu na kuwaongezea hali ya kwenda kufanya kazi ya uwalimu kwa kujituma na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wao.


Tuesday, October 24, 2017

JEH MARUDIO YA UCHAGUZI WA KENYA 2017 YATAFANYIKA?


Wakati kukiwa na sintofahamu nchini Kenya kuhusu marudio ya uchaguzi mkuu 2017 karatasi za kuhusika na mchakato huo tayari zietua katika maeneo yote ya uchaguzi kwaajili ya kutoa fursa kwa wananchi kuamua.

Fuatilia mahojiano ya Mtangazaji wako Albert G. Sengo na mchambuzi Simon Sawe yaliyofanyika leo ndani ya kipindi cha KAZI NA NGOMA ya 93.7 Jembe Fm Mwanza.
Ballot papers for the rerun presidential election arrive at the Jomo Kenyatta international airport.
Karatasi za kura.

SERIKALI YALIFUNGIA GAZETI LA TANZANIA DAIMA KWA SIKU 90



Serikali ya Tanzania kupitia idara ya habari maelezo imelifungia gazeti la Tanzania Daima ambalo ni gazeti la kila siku, kwa muda wa siku 90 .

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji mkuu wa serikali Tanzania Dr, Hassan Abbas, amesema gazeti hilo limefungiwa kutokana na ukiukwaji wa maadili ya taaluma ya habari ikiwemo kuchapisha habari za uongo na za kichochezi ambazo zinaweza kuzusha hofu miongoni mwa jamii.

Miongoni mwa habari zilizosababisha kufungwa kwa gazeti la Tanzania Daima , ni ile iliyokuwa na makosa ya kihariri kwenye toleo nambari 4706 la Oktoba 22, 2017 ambalo liliandika kuwa 'ASILIMIA 67 YA WATANZANIA WANATUMIA ARVS' dawa za kufubaza makali ya ugonjwa wa ukimwi. 

Habari nyingine katika toleo hilo ilieleza kuwa "MAKINIKIA PASUA KICHWA".
Idara hiyo imedai kuwa gazeti hilo limetoa habari yenye uongo wenye nia ya kuleta dharau dhidi ya hatua ya serikali na makubaliano yaliyofikiwa baina yake na kampuni ya Barrick Gold Corporation.

Tanzania Daima, linakuwa gazeti la nne kufungiwa na serikali ya Tanzania ndani ya miezi minne ikiwemo gazeti la Raia Mwema na Mwana Halisi lililofungiwa kwa kile kilichodaiwa kuwa ni uchapishaji wa habari za uongo na kichochezi ambazo zingeweza kuhatarisha usalama wa taifa hilo.




katika siku za hivi karibuni vyombo vya habari vimekuwa vikimulikwa kwa karibu nchini Tanzania.

Ikumbukwe kwamba mapema mwaka huu Raisi Magufuli alivionya vyombo vya habari nchini humo 'visifikiri kwamba viko huru kwa kiwango hicho.' kauli ambayo inatoa angalizo la umakini katika kazi za kila siku za vyombo hivyo kwa muujibu wa sheria ya mitandao na sheria za Tanzaia.

SHUKUDIA MWANZO MWISHO TUZO ZA FIFA Football 2017



The Best FIFA Football Awards™ are coming to London on Monday 23 October – and you can follow the entire day’s events with FIFA's digital platforms! Join us for hours of intrigue as the biggest names in world football descend on the London Palladium by getting behind-the-scenes glimpses – from fascinating photos to interviews with the stars.

Follow the glitz and glamour with our live FIFA TV on YouTube stream,.You can keep across the action with our live blog, starting at 15:30 CET, bringing you live updates as all the excitement unfolds. You’ll naturally want to follow our social media platforms throughout the day, too.

Exclusive photos, videos and interactions all await you on Twitter, Facebook and Instagram. You'll have an 'access all areas' pass with our Instagram story, so make sure you're following along.

You can also get your posts noticed using the hashtag #TheBest.

Please note that the viewing of the TV Show will be blocked in the following countries : USA, Puerto Rico, Albania, Austria, Belarus, Belgium, Bosnia and Herzegovina, Bulgaria, Croatia, Cyprus, Estonia, Georgia, Greece, Hungary, Latvia, Liechtenstein, Lithuania, Macedonia (FYROM), Montenegro, Poland, Portugal, Serbia, Slovakia, Switzerland, Turkey, Ukraine

MAKONDA AHAMIA KWENYE KIKAPU.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA leo ametoa msaada wa Generator ya kisasa, Mabati 150 na Mipira 110 kwa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es salaam ili kujengea uwezo timu ya Mpira wa Kikapu ya Mkoa.

Generator hiyo ya kisasa ina uwezo wa KV 35 na haitoi mngurumo wa sauti (silent) ambapo ikijazwa mafuta inaweza kutumika kwa muda wa masaa nane mfululizo.

RC MAKONDA amesema anataka kuona Timu ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam inakuwa timu kubwa itakayotoa Wachezaji wakubwa wanaocheza ligi za ndani na Nje ya Nchi.

Uamuzi wa RC MAKONDA kugawa vifaa hivyo ni baada ya kualikwa kwenye ligi ya mchezo wa Kikapu Uwanja wa Taifa na kujionea Uchakavu wa Bati unaosababisha Wachezaji kunyeshewa na Mvua, Ukosefu wa Generator umeme ukikatika na uhaba wa Mipira hali iliyokuwa ikiwapa wachezaji wakati mgumu.

Aidha RC MAKONDA aliahidi kujenga viwanja vitatu vya Mchezo wa Kikapu ambapo tayari ramani imetengenezwa na muda sio mrefu atasaini mkataba na mkandarasi wa ujenzi wa Viwanja hivyo.
Ili kuendelea kuimarisha Michezo Dar es salaam RC MAKONDA anaunda kamati maalumu ya kushughulikia michezo ya aina zote.

Tayari RC MAKONDA amepata mdau atakaejenga Swimming pool la kisasa Kinondoni kwaajili ya Mchezo wa Kuogelea.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa kikapu Dar es Salaam OKARE EMESU amemshukuru RC MAKONDA kwa msaada wa vifaa hivyo pamoja gharama za mafundi.

Monday, October 23, 2017

USIKU HUU NA TUZO ZA FIFA 2017.

 England. Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa Fifa 2017 baada ya kuwapiku wachezaji Lionel Messi na Neymar katika kipengele hicho.

Tuzo hizo zimetolewa usiku huu (Oktoba 23) ambapo mchezaji huyo aliyeambatana na mpenzi wake na mwanae amewashukuru waliompigia kura kwa kuweza kushinda pamoja na mashabiki na wachezaji wenzake.

“Nashukuru wote mlionipigia kura kwa kunifanya nishinde tuzo hii,” amesema Ronaldo.

Mbali na tuzo hiyo Ronaldo ametajwa katika kikosi bora cha mwaka 2017 ambacho kimewajumuisha Messi na Neymar na nyota wengine akiwemo Sergio Ramos, Toni Kroos, Andres Iniesta, na Dani Alves.

Tuzo ya mchezaji bora wa kike wa Fifa 2017 ilienda kwa Lieke Martens ambaye hakuudhuria katika utoaji wa tuzo kutokana na kujiandaa na kujiandaa na mechi ya kufuzu kombe la dunia la wanawake.

Ukumbi ulilipuka kwa shangwe wakati linatangazwa goli bora la mwaka ‘Puskas’ ambapo katika magoli 10 bora mashabiki walisikika wakimtaja nyota wa Arsenal, Olivier Giroud ambaye alitangazwa kama mshindi.





Wengine walioshinda tuzo za Fifa 2017 ni Zinedine Zidane (Kocha bora kwa waume), Sarina Wiegman (kocha bora kwa wanawake) Gianluigi Buffon (Kipa bora), Mashabiki wa Celtic (Kikundi bora), Francis Kone (Mchezo wa kiungwana).

UN NA AU ZATOA WITO WA AMANI KABLA YA UCHAGUZI WA MARUDIO KENYA.

Katika taarifa ya pamoja, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat wamewataka viongozi wote kuunga mkono amani na wahakikishe uchaguzi unafanyika kwa mujibu wa sheria. Aidha wamewataka wanasiasa na wafuasi wao waandae mazingira ya amani na wajiuepushe na kuibua ghasia na machafuko.

Uchaguzi wa rais wa marudio nchini Kenya unafanyika Alhamisi wiki hii, baada ya Mahakama ya Kilele kubatilisha uchaguzi wa Agosti nane baada ya kinara wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga kuwasilisha kesi ya kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee. 

Hivi sasa chama cha Jubilee kinasisitiza uchaguzi uendelee kama ulivyopangwa lakini muungano wa NASA unasema uchaguzi wa marudio bado haujatimiza masharti ya kuufanya uwe huru na wa haki. Odinga ametoa wito kwa wafuasi wake kususia uchaguzi huo.

Raila Odinga (kushoto) na Rais Uhuru Kenyatta
Wakati huo huo Rais Kenyatta amesema yuko tayari kufanya mazungumzo na Odinga lakini baada ya uchaguzi wa Alhamisi. Aidha amesema atatia saini muswada wa sheria mpya ya uchaguzi iliyofanyiwa marekebisho. 

Wapinzani wamepinga marekebisho hayo. Kenyatta amesema kuna usalama wa kutosha kwa ajili ya uchaguzi wa Alhamisi huku akitoa wito kwa wale ambao hawataki kupiga kura wasiwazuie wale wanaotaka kupiga kura.

YANGA YAKANUSHA TAARIFA YA KUWEKA KAMBI MORO.


Pamoja na taarifa kama Yanga itaweka kambi mjini Morogoro umeonyesha kuendelea kufanya siri jambo hilo.

Taarifa za Yanga kuweka kambi mjini Morogoro kujiwinda dhidi ya Simba Agosti 28 zilianza juzi lakini uongozi wa Yanga kutotaka kuliweka hadharani jambo hilo.

Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amesisitiza kwamba watatangaza kambi yao ilipo baada ya kufika Dar es Salaam.

“Kwa sasa tuko Shinyanga, tutakapofika Dar es Salaam tutatangaza kambi yetu ni wapi, si sasa,” alisema.

Taarifa nyingine zinaeleza, Kocha George Lwandamina alivutiwa na kambi ya Morogoro ambayo aliitumia kujiandaa wakati wa Pre Season.

“Kocha aliipenda sana kambi ya Morogoro, utulivu na hali ilivyo. Nina uhakika kocha atataka Morogoro,” kilieleza chanzo.

UKUTA MKUBWA WA BEIJING (THE GREAT WALL) UNAVYOINEMEESHA NCHI YA CHINA KATIKA SEKTA YA UTALII

Sehemu ye Ukuta Mkubwa ndani ya Mji wa Beijing nchini China (The Great Wall),kama uonekanavyo pichani mapema leo mchana,ambapo Maelfu ya watu wakiwemo Wenyeji na wageni hufurika kutembelea ukuta huo wenye historia kubwa nchini humo.Kuusoma zaidi BOFYA HAPA,Ukuta huo umekuwa kivutio kikubwa kwa wenyeji na wageni mbalimbali ambao wamekuwa wakifurika kila kukicha na kujionea historia kubwa ya ukuta huo nchini China,inaelezwa kuwa ukuta huo ni mojawapo ya chanzo kikubwa cha mapato katika nchi hiyo hasa kwa upande wa sekta ya Utalii.

Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani na Uongozi wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies wapita maelezo mafupi kutoka kwa wenyeji wao kabla ya kupanda Ukuta wa The Great Wall mapema leo mchana,ikiwa ni sehemu ya kujifunza,kuona na kutazama fursa mbalimbali za Kiutalii mjini humo na namna wenyeji wa mji wa Beijing wanavyofanya shughuli zao kiutalii.
Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani na Uongozi wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies na baadhi ya wenyeji wakielekea kwenye geti kuu la kuingilia Ukuta huo wa The Great wall,mapema leo mchana.
Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani na Uongozi wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies wakiwa na Mwenyeji wao,wa tatu kulia wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya The Great Wall,mjini Beijing nchini China.Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies Mohamed Said Kiluwa (mwenye njano),akipata maelezo mafupi kutoka kwa mmoja wa wadau wake aliombatana nao Risasi Mwaulanga,huku baaadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani wakisikiliza kwa makini,kulia ni Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Philomena Kasanga, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha,Mansoury Kisebebo pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani (pichani kati)Zuberi Mhinana na nyuma yake ni Katibu Tawala Msaidizi – Uchumi na Uzalishaji -Mkoa wa Pwani,Shangwe Twamala pamoja 
Sehemu ye Ukuta Mkubwa ndani ya Mji wa Beijing nchini China (The Great Wall),kama uonekanavyo pichani mapema leo mchana,huku ukiwa mesheheni Maelfu ya watu wakiwemo Wenyeji na wageni (watalii) wakipanda ukuta huo ikiwa kama sehemu ya utalii na kujua historia ya ukuta huo uliopo nje kidogo ya mji wa Beijing nchini China.
The Great Wall ndani ya mji wa Beijing kama uonekanavyo mapema leo.

Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani na Uongozi wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies wakiwa katika  picha ya pamoja mapema leo mara baada ya kupanda Ukuta wa kihistoria ndani ya mji wa Beijing,nchini China
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies Mohamed Said Kiluwa akiwa na Wenyeji wake,ambao kwa pamoja wanatarajia kuandaa kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda kwa kuwaalika viongozi Waandamizi wa Serikali ya Mkoa wa Pwani (ambao tayari wamekwishawasili mjini humu),wafanyabiashara wakubwa ambao ni wamiliki wa viwanda na makampuni mbalimbali,litakalofanyika jijini Beijing,nchini China Oktoba 25,2017 ,litakalojumuisha wafanyashabiashara, wamiliki wa viwanda na makampuni wapatao 200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China.