ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 22, 2017

MWIGULU AUKUBALI MZIKI WA ALLIANCE: SINGIDA UNITED YASHINDA 2 KAVU.

Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba akizungumza na wandishi wa habari jijini Mwanza mara baada ya mchezo kati ya Alliance Academy dhidi ya Singida United mchezo uliofanyika katika dimba la Nyamagana, ambapo Alliance walitembezewa kichapo cha bao 2-0.
MAELEZO KWA PICHA NYINGINE KUWAJIA HIVI PUNDE........

















ZSSF YATILIANA SAINI NA BANKI TPB BANK UTOWAJI WA MIKOPO KWA WANACHAMA WA ZSSF ZANZIBAR.

MKURUGENZI Mkuu wa Tpb Bank Sabasaba Moshingi kushoto na Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Jamii Zanzibar (ZSSF) Makame Mwadini wakitiliana saini makubaliano ya kutowa mikopo ya Kielimu na Kuazia Maisha kwa Wanachama wa (ZSSF)hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa ZSSF kilimani Zanzibar, wakishuhudia Mwanasheria wa ZSSF Mohammed Fakih na Afisa Mawasiliano wa Tpb Bank Chichi Banda
Mkurgenzi Mkuu wa Tpb Bank Sabasaba Moshingi kushoto akibadilishana mikataba wa mikopo kwa Wanachama wa ZSSF kupata mikopo kupitia Banki ya Tpb Bank, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Mwadini Makame,  kuwawezesha kupata Mkopo wa Elimu ya Juu na kuaza maisha kwa Wanachama wa ZSSF, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Kilimani Zanzibar.wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa pande hizo mbili.
Maofisa wa Tpb Bank wakifuatilia mkutano huo wa utilianaji saini ya kutowa mikopo kwa Wanachama wa ZSSF Zanzibar kupitia benki hiyo hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ofisi za ZSSF Kilimani Zanzibar.
Maofisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF wakifuatila mkutano huo wa utilianaji wa saini.
Afisa Mawasiliano wa Tpb Bank Chichi Banda akitowa nafasi kwa waandishi wa habari kuuliza maswali wakati wa hafla hiyo.
Mkurgenzi Mkuu wa Tpb Bank Sabasaba Moshingi, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utilianaji wa saini kuelezea madhumuri ya hafla hiyo kuwanufaisha Wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar kupata mikopo kupitia Banki yake Tpb Bank. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Mwadini Makame
akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makubaliani ya kupata mikopo kwa Wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF, kupitia Banki ya Tpb Bank.
Maofisa wa Tpb Bank wakifuatilia hafla hiyo ya utilianaji wa saini na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF. 
Mwandishi wa habari akiulisa swali wakati wa hafla hiyo ya utilianaji wa saini baina ya ZSSF na Tpb Bank, kutowa mikopo kwa Wanachama wa ZSSF kupata Elimu ya Juu na Mkopo wa kuazia maisha. 
Mwandishi wa habari akiuliza swali wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi Mikopo wa Banki ya Tpb Bank Ndg. Henry Bwogi akifafanua na kujibu maswali yalioulizwa na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo ya utilianaji wa saini baina ya pande hizo mbili. 
Afisa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF Bi Raya Hamad Khamis akitowa shukrani kwa washiriki wa hafla hiyo ya utilianaji wa saini uliofanyika katika Ofisi za Jengo la ZSSF Kilimani Zanzibar. 
Viongozi wa Tpb Bank na ZSSF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa hafla hiyo. 
Mkurugenzi wa Banki ya Tpb Bank Sabasaba Moshingi akiwa na Maofisa wa ZSSF wakibalishana mawazo baada ya kumaliza hafla ya utilianaji wa saini na ZSSF, katikati Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ZSSF Ndg.Mwadini na Afisa wa ZSSF Miradi Ndg. Muumin.
Mkurugenzi wa Banki ya Tpb Bank Sabasaba Moshingi akisalimiana na Afisa wa ZSSF Ndg Filifili. 
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.com
Zanzinews.com.
Email. othmanmaulid@gmail.com
0777424152. 

MKUU WA MKOA WA MWANZA JOHN MONGELA - AMEKIFUNGA KIWANDA KILICHOKUWA CHA USINDIKAJI WA NGOZI (AFRIKA TANARIZ) KINACHOMILIKIWA NA KAMPUNI YA QUALITY GROUP, BAADA YA KUBADILISHWA MATUMIZI NA KUFANYWA GHALA.

SERIKALI mkoani Mwanza imeamuru kufungwa kwa kiwanda cha Ngozi cha  Africa Tanneries Limited baada ya mmiliki wake kukaidi agizo la kuyafanyia usafi mazingira ya kiwanda hicho na kuja na mpango mkakati wa kukiendeleza ndani ya siku kumi zilizotolewa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Hatua ya mkuu wa Mkoa John Mongela inafuatia ziara yake aliyoifanya kiwandani hapo tarehe 10 Julai, 2017 na kuwaamuru wahusika kuwa na mpango kazi ambao ungeonesha kwa namna gani wataanza kazi ifikapo Januari, 2018, huku akiwataka wahusika wote ambao wanamaslahi na kiwanda hicho kuwepo kiwandani hapo ifikapo 20 Julai, 2017.


Kinyume na matarajio ya Mkuu wa Mkoa, alipowasili kiwandani akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo, majira ya saa 5.43 za asubuhi siku ya tarehe 20 Julai, 2017, alikuta hakuna maendeleo yoyote juu ya hatma ya kiwanda hicho na hata mpango kazi aliokuwa ameagiza hakuuona.

Akitoa maelezo mbele ya mkuu wa mkoa, Mwanasheria kutoka Kampuni ya Galati ya jiji Mwanza, Pendo Gimeno, alisema yeye anachofahamu wapo katika mchakato wa kuhamisha umiliki kutoka kwa mmiliki wa awali ambaye ni Casco kwenda kwa Sky Scraper zoezi ambali lilianza kwa makubaliano tokea mwaka 2015 lakini makabidhiano ya Jalada katika ofisi zao walilipata mwaka 2016.

Mkuu wa mkoa alipotaka kufahamu zaidi juu ya hatua walizofikia, mwanasheria huyo alionesha kutofahamu jambo lingene zaidi ya suala la uhamisho na hivyo kuzidi kuongeza sintofahamu ya jambo hilo.

Naye afisa wa Usalama wa kanda wa Kampuni ya Caspian, Nurdin Suleiman, ambao wanaingia katika kadhia hiyo, kufatia kugeuza eneo la kiwanda hicho kuwa sehemu ya kutunzia baadhi ya mitambo yao, alipohojiwa ni lini wataondoa vifaa vyao ilikupisha shughuli zilizo kusudiwa kuendelea, alisema wao wapo tayari kuviondoa vifaa vyao lakini kufuatia utata uliopo ndio maana wameshindwa kuviondoa, huku akitaja kupata hasara ya mali hizo.

“Mhe. Mkuu wa Mkoa sisi tupo tayari kuondosha mali zetu hata sasa, lakini vikwazo ambavyo tumevipata ni kuwa vitu vyetu vimengiwa sio chini ya miaka miwili, lakini tuliitika wito wa Mh. Mkuu wa mkoa na tulikuwa tayari kuondoa lakini Quality Group ndio walituzuia kuondosha” alisema Nurdin.


Hata hivyo Mkuu wa Mkoa, akaomba ushauri kutoka kwa baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama aliokuwa ameambatana nao akiwapo Katibu Tawala wa Mkoa, ambaye katika ushauri alioutoa, ilikuwa nikutafutwa kwa mmiliki hadi hapo atakapo patikana, ili hali Captain wa Jeshi la wananchi la Tanzania, akimashauri mkuu wa mkoa kuliweka eneo hilo chini ya uangalizi wa serikali hadi hapo sintofahamu iliyopo itakapo malizika.

Kufuatia ushauri alioupata, ndipo hapo mkuu wa mkoa akaamuru kufungwa kwaKiwanda hicho na kisha funguo kuwa chini ya ofisi ya mkuu wa mkoa hadi hapo suluhu itakapo patikana, “Kwamba kuna kamgogoro hapa, serikali ilibinafsisha viwanda hiki ili kiendelezwe katika sekta hiyo hiyo ya ngozi na hata Mhe. Rais mara nyingi amesema juu ya viwanda hivi juu yakuvifufua, aliema Mongella na kuongeza, kwamba alipofika tarehe 10 Julai, 2017 ilikuwa kutoa maelekezo juu kuondoshe vifaa vyote.

 Mongella alisema, kwakuwa shughuli hiyo niya kitaalam nilazima sekta zote zihusishwe ikiwapo watu wa Wizara ya Viwanda, watu wa ubinafsishaji na watu wa ardhi lazima wawe pamoja “Kwa sasa Jengo hili litakuwa chini ya Ofisi yangu na funguo tunaondoka nazo na hakuna mtu mwingine, nakwa uapande wa  wale waliopanga kama Caspian na Vodacom wasubiri lakini waendelee na biashara zao” alihitimisha, huku akimtaka Katibu Tawala wa Mkoa kuweka ulinzi katika eneo hilo.







 
A