ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 28, 2017

SERIKALI IMESEMA INAFANYA JUHUDI ZA KUOKOA WATU 14 WALIOFUKIWA GEITA.

Naibu waziri wa Nishati na madini Dr,Medadi Kalemani akiwasilia katika mgodiwa wa RZ ambako kumetokea tukio la watu 14 kufukiwa na udongo wakati wakiendelea na kazi za uchimbaji.
Shughuli za uokoaji zikiendelea na hili ni shimo ambalo linatolewa udongo uliojifukia.
Mbunge wa Jimbo la Busanda ,Lorencia Bukwimba akielekea  kwenye eneo la shimo ambapo watu wamefunikwa.
Mbunge wa Jimbo la Busanda ,Lorencia Bukwimba akiwapa pole ndugu na jamaa ambao walikuja kujua kile ambacho kitaendelea kwa undugu zao.
Raia wa kichina ambao ndio wamiliki wa mgodi huo wakiwa katika hali ya mawazo.

Wananchi wakiwa nje ya Ngome ya mgodi wakifatilia kile ambacho kinaendelea .
Jeshi la Polisi likiimarisha ulinzi na usalama kwenye eneo la mgodi.
Sehemu ambayo inatumiwa kutolea udongo.
Ndugu wakiwa katika masikitiko makubwa wakijiuliza ni lini ndugu zao watatoka shimoni.
Mkuu wa Mkoa wa Geita  Meja jenerali Ezekiel Kyunga akiwa katika eneo la tukio akifatilia kile kinachoendelea
Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi akipandisha juu baada ya kutoka shimoni
Kamishina msaidizi wa madini kanda ya ziwa,Mhandisi Yahaya Samamba akitoa taarifa ya shughuli ya uokoaji inavyoendela kwa Naibu waziri wa nishati na madini.
Naibu waziri wa nishati na madini,Dr Medadi Kalemani akioneshwa baadhi ya maeneo yaliyopata dosari kwenye mgodi huo
Naibu waziri wa nishati na madini akitazama shimo ambalo limejifukia







Naibu waziri wa nishati na madini Dr Medard Kalemani akiondoka eneo la mgodi baada ya kuona jitihada zinazoendelea.

NAIBU waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani ametembelea Mgodi wa RZ uliofukia Watanzania 13 na raia mmoja wa Nchini China anayetambulika kwa jina la Meng Juping na kusema kuwa serikali itaendelea kuweka nguvu ili kusaidia uokoaji.

Katika ziara yake hiyo ya dharura Naibu Waziri huyo ametoa pole kwa niaba ya serikali kwa uongozi wa Mkoa, Wananchi pamoja na Mgodi huo kukumbwa na tukio hilo.

Mara baada ya kupokea taarifa ya maafa hayo, iliyosomwa na kamishina msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria, Dk. Kalemani aliutaka uongozi wa Mkoa pamoja kamati ya uokoaji kujikita zaidi kwenye shughuli ya uokojai na waachane na mambo mengine ambayo yanaweza yakasababisha zoezi hilo liwe gumu.

‘’Ndugu zangu mimi kwa niaba ya serikali kuu napenda nitoe pole kwa hiki kilichowakumba Mkoa pamoja na Mgodi lakini napenda kuwaambia kuwa Kamati ya ulinzi na Usalama pamoja natimu ya uokoaji mhakikishe mnasimamia vyema zoezi hili ili tuwaokoe ndugu zetu ambao wamo humo ndani ya shimo,’’alisema Naibu waziri Kaleman.

‘’Kingine niagize hapa hakikisheni mnatoboa shimo kwa kutumia drilling ili tupate mwanya wa kuwapatia chakula ndugu zetu ambao wamefukiwa na udongo wakati juhudi za kufukua zikiendelea ,’’aliongeza.


Akizungumza na Maduka online mapema asubuhi ya leo  kamishina msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria Yahaya Samamba alisema kuwa kamati ya uokozi kwa kushirikiana kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Geita, ilibadilisha mfumo wa uokoaji kwa kutumia wachimbaji wadogowadogo baada ya mashine za kisasa kufikia usawa mita 20 ambazo haziwezi kuhimili uzito.

‘’Mitambo hii imekomea mita 20 tumeona tutumie wachimbaji wadogo ili twende sambaba na uokoaji uliosalama..kwahiyo usiku wa jana (juzi) saa 5:00 kamili usiku tulisitisha kutumia mashie yaani Magreda kutokana na usawa tuliofikia kuwa laini,’’alisema Samamba.

Kwa upande wake Mhandisi kutoka kampuni ya  uchimbaji ya Busolwa Mine Eng. Nayompa wakati akitoa mtazamo wake namna zoezi hilo linavyokuwa gumu alisema ramani zinazotolewa na wachina ni za kubahatisha na hawana uhakika nazo ndizo sababu zimechelewesha uokoaji na zoezi kuonekana halikamiliki kwa wepesi.

“Mimi ninachokiona hapa wachina hawa ndugu zetu wachina wameshindwa kutupatia ramani ya uhakika ndiyo maana tunabahatisha bahatisha tu..mwandishi hata wewe jana ulikuwa shuhuda namna gari la kutoboa lilivyoshindwa kulenga kwenye shimo  walipo ndugu zetu,’’alisema Eng. Nayompa.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Busandwa ambako tukio hilo limetokea Lolensia Bukwimba alisema haipaswi watu kunyosheana kidole kwa sasa wakati nguvu na jtighada zikiendelea kufanywa.

Hata hivyo Rais wa shirikisho wa vyama vya wachimbaji wa madini ,John Wambura Bina,amepongeza juhudi ambazo zinafanyika kwa makapuni ya madini kujitolea pamoja na serikali na wanaamini kuwa juhudi za uokoaji zinazoendelea zinaweza kuzaa matunda.

Viongozi mbalimbali wa serikali na chama jana walitembelea eneo la Mawemeru kuliko mgodi wa RZ ambao unamilikiwa na wawekezaji wa Kichina huku leseni ya madini ikiwa ni ya Mtanzania Ahamed Mbaraka.

Matumaini kwa siku ya leo yanaonekana kwani hadi kufikia majira ya saa moja kamili watu ambao wapo chini waligonga bomba kwa kuashiria kuwa wapo karibu na sehemu ya kutokea.

SERENA WILLIAMS AANDIKA HISTORIA BAADA YA KUSHINDA DADA YAKE VENUS KWENYE FAINALI.

Pamoja sana!!
Serena Williams ameandika historia kwenye tennis kwa mara nyingine baada ya kumshinda dada yake Venus kwenye mashindano ya Australian Open.
Serena amemshinda dada yake kwa seti 6-4 6-4, na kufikisha mataji ya grand slam 23.
Kwa ushindi huo, mchezaji huyo wa Marekani amechukua taji lake mchezaji nambari moja wa mchezo huo lililokuwa ikishikiliwa na Mjerumani, Angelique Kerber.
Mchezaji wa Australia Margaret Court, mwenye vikombe 24, ndiye mchezaji pekee aliye juu ya Serena katika mataji Grand Slam ya mchezaji mmoja mmoja.

Friday, January 27, 2017

ZOEZI LA UOKOAJI MGODI WA RZ GEITA MWANGA WA MATUMAINI

Mashine ya kutolea udongo uliojifukia ikiendelea na juhudi za kufukua ili kupata sehemu ya mlango wa kutokea.


 NA MADUKA ONLINE

NI SIKU  ya pili sasa tangu wachimbaji kumi na nne (14)  ambapo simanzi, masikitiko yameendelea kutanda baina ya jamii na ndugu wa wachimbaji ambao wamefukiwa na udogo kwenye  Mgodi wa RZ uliopo Kijiji cha Nyarugusu Wilaya ya Geita hata hivyo jitihada na zoezi la kuwaokoa bado linaendelea .

Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Geita, Ofisi ya Madini Kanda ya ziwa magharibi ikiyashirikisha makampuni ya Migodi ikiwemo GGM  na Busolwa mine ndiyo wanaosimamia zoezi hilo ambapo imeelezwa hatua iliyofikiwa hadi leo  saa 1:30 asubuhi  walikuwa wamechimba takribani mita 20 kati ya 30 ili kuwafikia wachimbaji hao.

 Kufuatia hatua hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amewataka  ndugu na jamaa wa watu 14 waliofukiwa na kifusi ndani ya Mgodi wa RZ   kuwa na subira wakati waokoaji wakiendelea na Zoezi hilo.

 “Mimi niwatake ndugu na jamaa kuendelea kuvuta subira wakati waokoaji wakiendelea  na kutumia mashine kwa ajili ya kuwaokoa watu waliozama chini ya Mgodi huo jambo ambalo hata Mkoa wa Geita umelipokea kwa masikitiko makubwa sana,’’alisema Kyunga.

 Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ametoa  kalipio kali kwa wawekezaji ambao hawajali ustawi wa wafanyakazi wake kwa uzembe ambao unaweza kuepukika na kwamba alisikitishwa sana namna mgodi wa RZ ambavyo ulikuwa haujali masuala ya miundombinu yake.

ZOEZI LA UOKOAJI
Ingawa matumaini ya wengi yamefifia kuwapata ndugu hao kutokana na ugumu wa zoezi zima ila kuna mwanga wa matumaini umeanza kuonekana.

Kamishina wa madini kanda ya ziwa magharibi Bw. Yahaya Samamba amesema zoezi hilo litakamilika na watu watakuwa salama kutokana na hewa wanayoipata kupitia mpira unaoingiza kwa kutumia mashine.

 Kamishina msaidizi wa  madini kanda ya Ziwa  Yahaya Samamba ameendelea kuelezea kuwa  pamoja na kuunda kamati ya uokoji wamekutana na changamoto kubwa kwa sababu ya duara walikozama watu hao kuwa chini ya kilomita 35.huku akisema wanaendelea kuomba mashine nyingine kutoka kwa makampuni mengine kama zoezi litaonekana kuwa na ugumu.

 “Tumeunda kamati ya uokoji na kamati yetu imehusisha makampuni yote yalioleta mashine zao kwa ajili ya uokoaji huo huku naye akiwataka wananchi kutoanza kutoa lawama kwa baadhi ya vyombo vya Serikali na ngazi nyingine kwenye wizara ya madini,, alisema Samamba.

 Diwani wa kata ya Nyarugusu yalipo maafa hayo, Swalehe Juma  alisema janga hilo limemnyima usingizi na kwamba siku ya jana alilazimika kukesha na waokoaji.

 “Mwandishi nakushukuru kwa kuwa nasi kwenye zoezi hili ni kweli mimi nyumbani ni karibu hata kwa miguu naweza kutembea nikafika lakini siwezi kwenda jambo hili limeninyima raha nitawezaje kwenda kwangu wananchi wangu wako ndani ya shimo,’’alisema Juma.

 MAONI YA WANANCHI.
Hata hivyo baadhi ya wananchi waliohudhuria kushuhudia tukio hili la aina yake katika wilaya ya Geita ikiwa ni mwanzoni mwa mwaka wa 2017, walisema lawama kubwa wanazielekeza kwa mamlaka za madini kwa kushindwa kujisimamia katika kuhakikisha uchimbaji ulio imara kwenye migodi unaboreshwa.

 “kaka hili jambo linasikitisha sana hebu fikiria tangu usiku wa tarehe 26 saa saba usiku mpaka leo siku nyingine ya tarehe 27 tumekutana tena watu wako ndani ya kifusi je watapona licha ya matumaini tunayopewa…Mimi hapa naelekeza lawama kwa ofisi ya Madini Mkoa wa Geita hawakagui migodi ipasavyo,’’alisema Mkazi wa Nyarugusu Saidi Mrisho.

 “Kwanza nashangaa nilimsikia jana kamishina wa madini kanda ya ziwa akisema chanzo ni kutokana na miti iliyokuwa imeshikilia ukuta kuwa imeoza sasa hapa najiuliza je, kazi ya ofisi ya madini nini wanakagua nini na je waliwahi kuwaambia kuwa miti hii haifai katika ukaguzi  wao inapaswa serikali nayo iwachukulie hatua kubwa kwa uzembe huu haiwezekani,’’alisisitiza.

 Katika shughuli za uokoaji wananchi hawakuacha kuipongeza kampuni ya uchimbaji wa madini ya Busolwa Mine inayomilikiwa na mwekezaji mzawa Baraka kwa kujitolea mashine zake za greda kuhakikisha wanafanikisha adhima ya kuwaokoa watanzania 13 pamoja na raia wa china Bw. Meng Juping, ambaye anadaiwa hakuwa na Radio Call kama ilivyokuwa kawaida yake wakati anakwenda kutekeleza majukumu yake ya uzalishaji wa madini ya dhahabu.

APIGWA MAWE HADI KUFA KISA KUIBA KUKU.

Apigwa mawe hadi kufa kisa kuiba kuku.
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Safari Bungate mwenye umri wa miaka 51, mkazi wa kijiji cha Kanyelele wilayani Misungwi Mkoani Mwanza ameuawa kwa kupigwa mawe na fimbo sehemu mbalimbali za mwili na kundi la watu walioamua kujichukulia sheria mkononi kwa madai ya kuiba kuku.

Tukio hili limetokea jana TAREHE 26.01.2017 majira ya saa 04:00 usiku,baada ya kuiba kuku nyumbani kwa Tetema Mathias (40) ambaye ni mkulima na mkazi wa kijiji hicho. 

Taarifa zaidi zinasema kuwa mnamo majira hayo tajwa hapo juu, mwenye nyumba Bwana Tetema akiwa amelele na familia yake, marehemu alifika kwenye nyumba hiyo na kupitia dirishani alizama ndani na kisha kuiba kuku mmoja.

Bwana Mathas alisikia vishindo vya kimya kimya vya kunyemelea visivyo vya kawaida na mara baada ya kunyanyuka toka kitandani kuelekea mahala sauti za chini zilikuwa zikisikika  akamnasa mwizi wake n kuanza kupiga yowe akiomba msaada wa majirani.

Marehemu Safari aliponyoka mikononi mwa bwana huyo akikimbia barabarani ambako alikamatwa na wananchi wenye hasira kali na kuanza kushambuliwa na mawe akichapwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili hadi kupoteza fahamu na baada ya muda akazimika.

Raia wema walitoa taarifa kituo cha polisi, nao askari wakafika eneo la tukio na kukuta mtuhumiwa wa wizi huo akiwa tayari amefariki. 

Mwilia wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu zake kwaajili ya mazishi.

Aidha bwana Tetema Mathias aliyeibiwa kuku anashiiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WAJIJI NA MKOA WA MWANZA, AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KOSA LA JINAI, AIDHA ANAWATAKA WANANCHI PINDI WANAPOMKAMATA MHALIFU WAMFIKISHE KATIKA VYOMBO VYA SHERIA ILI HATUA ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAKE. 
HABARI NA GSENGO.

SIKU YA PILI WALIOFUKIWA MGODI WA NYALUGUSU GEITA HIKI NDICHO KINACHOENDELEA.

Jitihada zikiendelea za uokoaji
IKIWA ni siku ya pili, takribani saa 36 sasa zimetoweka tangu kutokea kwa tukio la watu 14 kufukiwa na kifusi cha udongo kwenye machimbo ya madini mgodi wa RZ Nyarugusu wilaya ya Geita mkoani Geita, na kukiwa hakuna taarifa zozote juu ya hali za wanadamu hao walio chini ya ardhi umbali wa mita 38, Jembe Fm kupitia kipindi cha KAZI NA NGOMA inawasiliana na Mwandishi wa Habari Joel Maduka aliye katika eneo la tukio kupata hali halisi yakile kinachoendelea.

1.Zoezi la ufukuaji linaendeleaje?
2.Mawasiliano na watu hao walio chini ardhini Vipi! yamepatikana?
3.Jeh! kuna uhakika wowote kwa ndugu hao kutoka salama?
4.Ni muda gani zoezi hilo litakamilika?

Haya yanajibiwa kupitia taarifa hii:-BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

MAAFISA WA NGAZI ZA JUU WA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA MAREKANI WAJIUZULU, HAWATAKI KUFANYA KAZI NA TRUMP.


Maafisa wote wa ngazi za juu wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani waliofanya kazi katika kipindi cha uongozi wa rais mstaafu wa nchi hiyo, Barack Obama wamejiuzulu kwa pamoja.
Gazeti la Washington Post limeandika kuwa, kujiuzulu kwa wakurugenzi na maafisa wote wa ngazi za juu wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani ni sehemu ya mwenendo wa kuachia ngazi maafisa wa ngazi za juu wa serikali ya Washington ambao hawataki kufanya kazi katika serikali ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo. 
Kujiuzulu kwa kwa pamoja maafisa wote wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani kunatatiza kazi ya Rais Trump katika sekta ya masuala ya kigeni. 

Wamarekani wakiandamana kupinga uongozi wa Donald Trump.

Mkurugenzi wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani, Patrick Kennedy ambaye amekuwa na nafasi kubwa katika mchakato wa kuhamisha madaraka na ilidhaniwa kuwa ataendelea kufanya kazi katika kipindi cha uongozi wa Trump, naye alijizulu Jumatano iliyopita katika hatua iliyowashangaza wachambuzi wengi wa masuala ya Marekani. Wakurugenzi wengine wakuu waliojiuzulu nyadhifa zao katika wizara hiyo ni pamoja na Gregory Starr, Michele Bond na Tom Countryman.

DECI NYINGINE MBILI ZANASWA MKOANI MWANZA, WAMEPIGA HELA YA HATARI KWA WANANCHI.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 26.01.2017

·         TAHADHARI YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA WANANCHI WOTE WA MWANZA NA MAENEO JIRANI JUU YA UWEPO WA VIKUNDI VYA WAHALIFU WANAOIBIA WANANCHI FEDHA ZAO KWA KUWASHAWISHI KUJIUNGA NA BIASHARA YA UPATU ( KUWEKEZA FEDHA KIDOGO NA BAADAE KULIPWA FEDHA NYINGI KWA MUDA MFUPI BILA KUFANYA KAZI YEYOTE)  KAMA ILIVYOKUWA DECI .

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA DCP: AHMED MSANGI ANATOA TAHADHARI KWA WANANCHI WOTE WA MWANZA NA MAENEO JIRANI KUJIHADHARI/KUJIEPUSHA NA WATU/VIKUNDI VYA WATU AMBAO NI WAHALIFU WALIOKUSUDIA KUJIPATIA FEDHA NYINGI TOKA KWA WANANCHI KWA KUWADANGANYA/ KUWARUBUNI WAJIUNGE NA BIASHARA YA UPATU AMBAPO WANANCHI HAO HUSHAWISHIWA KUWEKEZA FEDHA KIDOGO KWA MUDA MFUPI KATIKA VIKUNDI HIVYO NA BAADA YA HAPO WANAAHIDIWA KULIPWA FEDHA NYINGI ZAIDI YA ZILE WALIZO WEKEZA BILA KUFANYA KAZI YEYOTE. BIASHARA HIYO INATAMBULIKA KWA JINA LISILO RASMI LA KUPANDA MBEGU NA KUVUNA.

HIVI KARIBUNI KUMEJITOKEZA WIMBI KUBWA LA VIKUNDI VYA NAMNA HIYO HAPA JIJI MWANZA NA TAYARI WANANCHI WENGI WAMEIBIWA FEDHA ZAO. KUTOKANA NA KUONGEZEKA KWA UHALIFU WA AINA HII JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEANZISHA NA LINAENDELEA NA MISAKO MAENEO MBALIBALI YA JIJI NA MKOA WA MWANZA, KWA LENGO LA KUBAINI NA KUWAKAMATA WATU/VIKUNDI VINAVYOFANYA UHALIFU HUO. (UPATU)

AIDHA KAMANDA ANATAHADHARISHA WANANCHI KUHUSU VIKUNDI VIFUATAVYO AMBAVYO UPELELEZI UMEONESHA KUWA VINAJIHUSISHA NA BIASHARA YA UPATU AMBAVYO NI; KIKUNDI KINACHOJULIKANA KWA JINA LA AQ POWER CLUB KINACHOMILIKIWA  NA HAPPY ALOYCE MBUYA MIAKA 35, MCHAGA , MKAZI MTAA WA ILIEMELA ENEO LA MAHAKAMANI, MFANYABIASHARA NA MKURUGENZI WA KAMPUNI BINAFSI IITWAYO AQ CUMPUTER CO.LTD, UPELELEZI UMEBAINI KWAMBA MTUHUMIWA TAJWA HAPO JUU AKISHIRIKIANA NA WENZAKE SABA (7) WAMEFANIKIWA KUKUSANYA FEDHA ZAIDI YA TSH 100,000,000/= KUTOKA KWA WANANCHI AMBAO WALISHAWISHIWA KUJIUNGA NA KIKUNDI CHAKE, PIA UPELELEZI UMEBAINI KUWA AQ POWER CLUB SIO TAASISI ILIYOSAJILIWA KISHERI BALI JINA LA BIASHARA LA MTUHUMIWA.

TAYARI MTUHUMIWA TAJWA HAPO JUU NA WENZAKE SABA WAMEKAMATWA NA UPELELEZI UNAENDELEA PINDI UKIKAMILIKA JARADA LITAPELEKWA KWA MWANASHERIA WA SERIKALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA DHIDI YAO, AIDHA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA ANATAHADHARISHA WANANCHI KUHUSU SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA KIKUNDI/ KAMPUNI BINAFSI YA BEGA KWA BEGA MICRO FINANCE COMPANY LTD, KWANI WATU WENGI WAMEKUJA KURIPOTI POLISI JUU YA KUTAPELIWA FEDHA ZAO NA KAMPUNI HIYO, TAYARI JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEWATIA MBARONI WAKURUGENZI NA BAADHI YA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI HIYO NA MAJALADA YA KESI HIZO YAPO KWA MWANASHERIA WA SERIKALI KWA HATUA ZAIDI ZA  KISHERIA.

AIDHA JESHI LA POLISI LINAENDELEA KUZIFANYIA KAZI TAARIFA ZA KIINTELEJENSIA KUHUSU TAASISI ITAMBULIKAYO KWA JINA LA AMKA MWANAMKE (AMWA), KWAMBA PIA INAJIHUSISHA NA BIASHARA YA UPATU, UCHUNGUZI UNAFANYWA ILI KUWEZA KUBAINI UKWELI WA TAARIFA HIZO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANAWATAHADHARISHA WANANCHI WOTE WA MWANZA NA MAENEO JIRANI KUJIEPUSHA NA VIKUNDI VYA AINA HII, PIA ANAWAAASA WANANCHI KUJITAFUTIA KIPATO CHA HALALI KWA KUFANYA KAZI HALALI NA SIO KUWEKEZA FEDHA KIDOGO (KUPANDA) NA KUTARAJIA KUPATA FEDHA NYINGI KWA MUDA MFUPI ( MAVUNO). TAMAA YA KUPATA UTAJIRI WA HARAKAHARAKA UMEWAINGIZA WANANCHI WENGI KWENYE HASARA KUBWA ILIYO TOKANA NA KUIBIWA FEDHA ZAO KWANI HAKUNA KIKUNDI/ MTU ANAYEWEZA KUPEWA FEDHA KWA MUDA MFUPI ALAFU BAADA YA MUDA MFUPI ALIPE FEDHA NYINGI ZAIDI. WANANCHI WATAMBUE KUWA HUU NI MTEGO WA WAHALIFU WA KUWAFANYA WANANCHI WASHAWISHIKE KUJIUNGA NA VIKUNDI HIVYO ILI WAWAIBIE.

IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Thursday, January 26, 2017

PICHA: KUMI NA NNE WAFUKIWA NA KWENYE MGODI WA RZ NYARUGUSU MKOANI GEITA

Shimo lililojifukia jitihada zikiendelea za uokoaji

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Geita.Elisha Mugisha,akitoa maelezo namna ambavyo wanaendelea na jitihada za kuokoa


Kamisha msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria Mhandisi Yahaya Samamba ,akifafanua namna ambavyo wameweza kuwasiliana na makapuni mengine ya uchimbaji wa madini kwaajili ya kutoa msaada kwa watu waliofukiwa


Moja kati ya wafanyakazi kwenye mgodi huo akielezea hali ilivyotokea na shimo lilivyojifukia


Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga,akiambatana na msemaji wa mgodi huo Frances Kiganga pamoja na kamanda wa zimamoto,Elisha Mugisha wakielekea kwenye eneo ambalo shimo limejifukia. 


Eneo la shimo likiendelea kuchimbwa
Jitihada zikiendelea za uokoaji
Baadhi ya waokoaji wakisemezana namna ya kuokoa
Shughuli zikiendelea 
Mwanasheria na msemaji wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya RZ  Frances   Kiganga ,akielezea chanzo cha mgodi huo kujifunika. 

BY. MADUKAONLINE
WATU kumi na nne(14)mmoja akiwa ni Raia wa China wamefukiwa na udongo usiku wa kuamkia leo  majira ya saa saba usiku (7:00)wakiwa wanaendelea na majukumu yao ya uchimbaji  kwenye kampuni ya RZ Iliyopo kijiji cha Nyarugusu  wilayani  na Mkoa wa  Geita.

Sababu za kuporomoka udongo  ni kutokana na mgodi kuchimbwa  zamani na Wajerumani hivyo kupelekea baadhi ya maeneo hayo kuwa na nyufa na vyuma kushindwa kushikilia udongo wa juu hali ambayo imepelekea kuzidiwa na mwisho wa siku kuporomoka.

Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Geita,ikiongwaza na mkuu wa Mkoa huo Meja jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga  imefika katika Mgodi wa RZ kuangalia  na kujionea zoezi la ukoaji  .

Kamisha msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria Mhandisi Yahaya Samamba ,ameelezea  kuwa jitihada ambazo zimefanyika ni kuwasiliana na migodi iliyopo karibu na eneo hilo  na pia wameshaomba msaada Kahama na kwenye mgodi wa GGM kupatiwa vifaa vya uokoaji ili zoezi hilo liwezekufanikiwa kwa urais zaidi.

“Jitihada ambazo tumezifanya hadi sasa tumeomba msaada kahama na kwenye mgodi wa Geita,kupatiwa vifaa ambavyo vitasaidia kwa wepesi zoezi hili la uokoaji ingawa tumeshapata vifaa vingine kutoka kwenye mgodi wa Busolwa”Alisema Samamba.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Geita.Elisha Mugisha,amesema kuwa eneo la chini ambalo limefukiwa na udongo ndio ambalo  kwa sasa wanaendelea kulitanua ili sehemu hiyo iwe kubwa watu waweze kupita.

“Eneo lote lile la chini limefukiwa na udongo lakini kule chini kunaonekana kuna  sehemu za kwenda pembeni ingawa limefukiwa lakini chini kunauhimala  kunauwezekano kule chini wale watu wapo hai na wamepelekewamipira ya hewa na kazi inayofanyika ni kutanua eneo ambalo litasaidia kuwatoa watu hao”tumekwisha kupeleka mipira

Mwanasheria na msemaji wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya RZ  Frances   Kiganga  ameelezea kuwa  chanzo kikubwa ni mashimo ya zamani kwani udongo unapotikisika umekuwa ukisababisha baadhi ya nyufa kuendelea kupata shida.

Baadhi ya wafanyakazi  wa kampuni hiyo Charles Julius Na Robert Stanleyambao wameeleza kuwa mida ya saa saba usiku duara lilinza kushuka taratibu na baada ya hatari hiyo walipewa taarifa ya watu ambao walikuwa chini kupandisha juu lakini hata hivyo jitihada hizo hazikuzaa matunda.

 Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amewataka wanaosimamia zoezi la uokoaji kuongeza nguvu ya uokozi .
Hadi Madukaonline inaondoka kwenye eneo la tukio akuna mtu yoyote ambaye ameokolewa ingawa jitihada bado zinaendelea kwa kuomba mashirika kuweka msaada zaidi wa uokoaji.