ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 1, 2017

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LAKANUSHA SUMU UKUMBI WA MKUTANO UVCCM.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
 JESHI LA POLISI TANZANIA
TELEGRAMS:   POLISI,  
TELEPHONE: 2500712                                                   
KAMANDA WA POLISI,
Fax: 2502310                                                   
MKOA WA MWANZA,

E-mail: mwapol@yahoo.com                                                                                     
S.L.P. 120,          
rpc.mwanza@tpf.go.tz                                                                                
MWANZA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBOVYA HABARI LEO TAREHE 30.11.2017 

KAMANDA   WA   POLISI   MKOA   WA   MWANZA   AMEKANUSHA   TAARIFA   ILIYOPOKATIKA GAZETI LA MWANANCHI LA TAREHE 30/11/2017.

LEO TAREHE 30.11.2017 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WAPOLISI AHMED MSANGI, AMEKANUSHA TAARIFA ILIYOPO KATIKA GAZETI LA MWANANCHILA TAREHE 30/11/2017, TOLEO NAMBA 6334, UKURASA WA TATU, INAYOSEMA KUWAAMETHIBITISHA  JUU  YA KUWEPO HEWA  YA SUMU  NDANI  YA UKUMBI WA  CITY MALL AMBAPO KULIKUWA KUKIFANYIKA MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI WA VIJANA WA CCM(UVCCM) MKOA WA MWANZA.

AIDHA KAMANDA MSANGI ANASEMA, UKWELI NI KUWA ALIPIGIWA SIMU NA MWANDISHIWA   GAZETI   HILO   TAREHE   29/11/2017   MAJIRA   YA   SAA   15:00   MCHANA   ALIYETAKAKUTHIBITISHIWA TAARIFA YA KUWEPO HEWA YA SUMU NDANI YA UKUMBI WA CITY MALLAMBAPO   KULIKUWA   KUKIFANYIKA   MKUTANO   TAJWA   HAPO   JUU.   

KAMANDA   ALIMJIBUKUWA   HANA   TAARIFA   NA   HAWEZI   KUTHIBITISHA   KWANI   HAJAPATA   TAARIFA   YEYOTE KUHISIANA NA YALIYOTOKEA KATIKA MKUTANO HUO, NA YEYE YUPO KWENYE KIKAO CHAKAMATI YA ULINZI NA USALAMA OFISI YA MKUU WA MKOA.

PIA   KAMANDA   HAKUFIKA   ENEO   TAJWA   KAMA   TAARIFA   HIYO     INAVYOSEMA,   HIVYOINAONEKANA MWANDISHI WA TAARIFA HIYO ALIAMUA KUANDIKA MANENO HAYO KWA MANUFAA YAKE BINAFSI HIVYO JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAOMBA GAZETIHUSIKA KUREKEBISHA. 

PIA ANAOMBA WAELEWE KUWA MATUKIO YA AINA KAMA HIYOYANAHITAJI   YAWE   NA   MAJIBU   YA   KITAALAMU   TOKA   KWA   WANASAYANSI   PINDIYANAPOTOKEA.

 AIDHA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINANAEDELE KUOMBA USHIRIKIANO TOKAKWA WAANDISHI WA HABARI KWA KUFANYA KAZI KWA PAMOJA ILI KUWEZA KUENDELEAKUDUMISHA   USALAMA   NA   ULINZI   KATIKA   MKOA   WETU.  

 PIA   JESHI   LINAWAOMBAWAANDISHI   WA   HABARI   KUFANYA   KAZI   KWA   KUFUATA   TAALUMA   YA   UANDISHI   WAHABARI, UWELEDI NA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI ILI KUEPUSHA HABARI ZA AINAKAMA HII AMBAZO ZINALETA PICHA MBAYA KWA JESHI NA MKANGANYIKO KWA JAMII.

IMETOLEWA NA;DCP: AHMED MSANGIKAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.