ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 6, 2017

WAKULIMA WA PAMBA WILAYANI GEITA WAIOMBA SERIKALI KUTATUA KERO YA PEMBEJEO NA WATAALAM WA KILIMO.

Shamba la Pamba.
Afisa Kilimo  wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Samweli Abuye  akizungumza na wakulima wa Kijiji na Kata ya Kagu.

Baadhi ya wananchi wakifuatilia kwa umakini maelekezo ya Kilimo cha pamba ambacho kinatarajia kuanza hivi karibuni.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akizungumza na watendaji wa kata na vijiji na kutoa msisitizo wa kuwasisitiza wananchi kwenye maeneo yao kulima zao la Pamba.







PICHA NA JOEL MADUKA 





Wakulima  wa zao la pamba katika tarafa ya Bugando Wilaya na Mkoani  ya Geita wamesema  wamekuwa wakikata tamaa kuendelea na kilimo cha zao hilo kutokana na sababu mbalimbali wanazokumbana nazo likiwemo suala la pembejeo pamoja na bei za pamba kutokueleweka.

Wakizungumza katika kikao cha maelekezo kwa watendaji wa serikali ya Vijiji na Kata kwenye ukanda wa tarafa ya Bugando, wakulima wa zao hilo  Faustin Nyamhanga, Faida Mwendesha  na Mateso Kabegelo, wameyatupia lawama makapuni yanayojihusisha na ununuzi wa zao hilo  kwa kile walichodai kwamba wanakuja na bei yao mkononi ambayo ni ya ughalalizaji.

Pamoja na mambo mengine, wameendelea  kuikumbusha serikali kuendelea kuyapatia ufumbuzi masuala ambayo yameonekana kuwa ni changamoto kwa wakulima.

Diwani wa kata ya Nyamboge, Daudi Bakazahala ameiomba Idara ya Kilimo Wilayani humo  kushirikiana na  Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Geita ili kushughulika na wahasibu wa makampuni ya ununuzi wa pamba kwenye maeneo ya vijijini ambao wamekuwa na tabia ya kuwaibia wakulima.

Kutokana na kero ambazo zimeelezwa na wakulima pamoja Diwani, Mkaguzi wa Zao la pamba Wilaya ya Geita Venance Kankutebe, amesema kutokana na uchache wa viwanda imekuwa ni changamoto kwa upande wa bei, huku Afisa Kilimo Samweli Abuye akijibu ombi la diwani wa Nyamboge kwa kubainisha kwamba ni vyema wao kama viongozi wa kata kumfikishia mwenyekiti ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Juu ya madai ambayo wamekuwa nayo kwani yeye ndiye msimamizi mkuu wa kikosi kazi cha ufuatiliaji wa kilimo cha pamba.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.