ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 23, 2017

MAGUFULI AAGIZA WATU HAWA WACHUKULIWE HATUA.


Rais John Pombe Magufuli amefunguka na kuvitaka vyombo vya dola nchini viwashungulikiwe watu ambao wamekuwa wakipika data za uongo za serikali na kuzichapisha sehemu mbalimbali na kusema watu hao wanapaswa kufikishwa mahakamani.

Rais Magufuli amesema hayo leo katika hafla ya kuwatunuku vyeti vya pongezi maaalum kwa wajumbe waliohusika kuchunguza kiwango, aina ya madini katika mchanga wa madini ambao ni makinikia. Rais Magufuli amesema kuwa kuna haja Waziri wa Sheria na vyombo vya dola kuangalia namna inavyowezekana kuwashughulikia watu ambao wanapika data.

"Niwaombe Watanzania wengi tofauti na wale wachache wanaopiga kelele muwapuuze, mtu ambaye anabadili data za serikali na kusema kuwa uchumi umeshuka nadhani wanapaswa kuchukuliwa hatua vyombo vya dola na wewe Profesa Kabudi ni Waziri wa Sheria muanze kuangalia watu wa namna hii ambao kwao kubadili Takwimu wanaona kitu kidogo, nafikiri kuna sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 na kunakifungu kinasema mtu anayebadilisha Takwimu za serikali anaweza kufungwa hata miaka 2 jela, kwanini hatuvitumii hivi? Unakuta mtu anazungumza makusanyo ya serikali yameshuka wakati anajua kabisa si kweli" alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa mapato ya nchi hayajashuka ndiyo maana Serikali imeweza kununua ndege zaidi ya sita kwa mpigo, serikali imeweza kujenga barabara kwa fedha za ndani, na kusema serikali imeweza kujenga reli kwa kuwa uchumi wake ni mzuri.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.