ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 7, 2017

TANESCO YAKABIDHI NYUMBA MBILI ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MTERA DAM


Mkuuwa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mhe.Jabir Shekimweri, (kushoto), akifungua pazia ikiwa ni ishara ya kuzindua nyumba mpya ya Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Mtera DAM, iliyoko jirani na Kituo cha Kufua Umeme wa maji, Mtera, katikati ya mikoa ya Dodoma na Iringa, Septemba 6, 2017. Nyumba hiyo na nyingine iliyokarabatiwa zimejengwa kwa msada wa TANESCO kwa thamani ya shilingi milioni 35. Wengine pichani, ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja mama Joyce Ngahyoma,(wakwanza kulia), aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, , (kulia) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia Ufuaji umeme, Mhandisi Abdallah Ikwasa. (kushoto), na Mkuu wa shule hiyo, Bw. Simon Dissa.

 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja, Mama Joyce Ngahyoma,(aliyesimama), akitoa hotuba kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.
 Mama Joyce Ngahyoma
 Mkuuwa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mhe.Jabir Shekimweri, (aliyesimama), akitoa hotuba yake kwenye hafla hiyo.
 Nyumba mpya ya Mawlimu Mkuu shule ya sekondari Mtera DAM, iliyojengwa na TANESCO na nyingine iliyokarabatiwa kwa thamani ya shilingi milioni 35.
 Mkuu wa Wilaya Mhe. Shekimweri, (kulia), na Mama Joyce Ngahyoma, wakiwa mbele ya nyumba hiyo baada ya kuizindua na kuikabidhi kwa Mkuu wa shule.
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumzia utaratibu wa kukabidhi nyumba hizo.
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo wakiwa na furaha.
 Mkuu wa shule ya sekondari Mtera DAM, Bw. Simon Dissa, akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo aliishukuru TANESCO kwa kupunguza uhaba wa nyumba za walimu na sasa bado wanahitaji nyumba 15.
  Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo wakiwa na furaha.
 Wananchi wakifurahia hotuba
 Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TANESCO wakiongozwa na Mama Joyce Ngahyoma.
Meneja wa Kituo cha Kufua Umeme wa Maji Mtera, Mhandisi John Skauki, akielezea ushirikiano baina ya TANESCO na wana jamii ya Mtera ambao alisema ni mzuri.
Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO
Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO walio katika Kituo cha Kufua umeme wa maji Mtera, wakifuatilia hafla hiyo.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limekabidhi majengo mawili ya nyumba za walimu, shule ya sekondari Mtera DAM, iliyoko jirani na Bwawa la kufua umeme wa maji Mtera, (Mtera Hydro Power Plant), lililoko katikati ya mikoa ya Dodoma na Iringa.
Nyumba hizo zilizogharimu shilingi milioni 35, moja ikiwa mpya na nyingine imekarabatiwa, zimekabidhiwa kwa uongozi wa Wilaya ya Mpwapwa Septemba 6, 2017 na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja, Bi. Joyce Ngahyoma, ambaye alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Dkt. Tito Mwinuka.
Akizungumza kabla ya kukabidhi nyumba hizo, Bi. Joyce Ngahyoma alisema, wakazi wa kata ya Mtera ni wadau na washirika wakubwa wa TANESCO katika kulinda miundombinu ya umeme ya kituo cha kufua umeme cha Mtera ambayo ina gharama kubwa kwa hivyo walipowasilisha maombi ya kujengewa nyumba ya mwalimu Mkuu, TANESCO ilikubali ombo hilo bila kusita.
Alisema, uongozi wa TANESCO baada ya kupokea maombi hayo ulifanya tathmini na kutoa kiasi cha fedha shilingi Milioni 35 ambazo zilitumika kujenga nyumba jipya na kukarabati nyumba nyingine.
Nyumba mpya iliyojengwa na TANESCO kwa ajili ya makazi ya Mwalimu Mkuu, ina vyumba vinne, choo, bafu na jiko, alisema.
“Napenda nichukue fursa hii kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa mnaotupatia na niwaahidi tu kwamba Shirika litaendelea kushirikiana na serikali na jamii kwa ujumla katika kuhakikisha sekta ya elimu, afya na huduma nyingine zinaimarika kwa kutoa michango ya hali na mali.” Alisema Bi. Ngahyoma.
Alisema, sambamba na msada huo, TANESCO imekuwa ikisaidia jamii ya wana Mtera, katika kuwapatia huduma ya afya kwenye zahanati ya wafanyakazi, huduma ya elimu ya awali(chekechea), kwenye shule ya chekechea iliyojengwa kuhudumia watotot wa wafanyakazi, na pia usafiri, ambapo mabasi yanayochukua wafanyakazi kwenda na kutoka kazini, huwasaidia pia wananchi.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia ufuaji umeme, Mhandisi Abdallah Ikwasa, alisema, Kituo cha kufua umeme wa maji Mtera, kilijengwa kuanzia mwaka 1984 na kukamilika mwaka 1988 na kuwa na uwezo wa kufua umeme Megawati 80 na tangu kipindi hicho hadi hivi sasa, TANESCO imekuwa ikishirikiana na wananchi katika kulinda miundombinu ya kituo hicho.
Mnamo mwaka 2005 na 2006, Shirika lilichangia kiasi cha shilingi milioni 34 kujenga madarasa mawili mapya na ujenzi wa ofisi ya walimu, alisema Mhandisi Ikwasa.
Akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kupokea majengo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. Jabir Shekimweri, amewataka wananchi wa Kata ya Mtera,  kuendelea kushirikiana na TANESCO, katika kulinda miundombinu ya Shirika hilo kwenye bwawa la kufua umeme wa maji la Mtera, (Mtera Hydro Power Plant).
“Ndugu zangu msada huu umekuja kutokana na faida inayopatikana kutokana na miundombinu hiyo, kwa hivyo niwaombe muendelee kushirikiana na TANESCO na viongozi wa serikali ya kijiji katika kuhakikisha usalama wa miundombinu hiyo unaendelea kuwepo kwani wafanyakazi wa TANESCO pekee hawawezi kulinda miungdominu hiyo peke yao kwa sababu eneo ni pana sana.” Alifafanua.
Mhe. Shekimweri alisema, msada wa majengo hayo, utasaidia kutatua changamoto ya nyumba kwa walimu ambao kutokana na uhaba mkubwa wa nyumba walimu wanaishi maeneo ya mbali na shule na hivyo inapelekea utendaji kazi wao kuwa wa chini.
“Nimeambiwa kuwa ufaulu kwenye shule hii ni mzuri na walimu wakiishi maeneo ya karibu na shule, basi ufaulu huo bila shaka utaongezeka sana.” Alisema.
Lakini pia niwaombe wananchi, umeme unaopatikana hapa unategemea sana uwepo wa maji, kwa hivyo nitoe rai, ni lazima tutumie maji haya kwa busara kubwa naelewa zipo shughuli za uvuvi lakini uvuvi mwingine ni ule haramu wa uharibifu, niwajulishe tu hivi karibuni tutakaa kikao ili kuweka matumizi bora ya maji haya ili kuzuia athari zinazoweza kupelekea uharibifu wa vyanzo vya maji yanayoletwa kwenye bwawa hili, alisisitiza.
Mkuu huyo wa wilaya aliishukuru TANESCO kwa kuisaidia serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwenye eneo hilo na .
“ Nimeambiwa kuwa sio tu mmesaidia ujenzi wa nyumba moja mpya na kukarabati nyingine lakini pia mmekuwa mkisaidia wananchi katika kuwapatia huduma za afya kwenye zahanati ya wafanyakazi, hali kadhalika mmekuwa mkiwasaidia wananchi katika usafiri ambapo wamekuwa wakitumia usafiri wa wafanyakazi wenu, hili ni jambo jema katika kujenga mahusiano mema baina yenu na wananchi.” Aliongeza Bw. Shekimweri.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.