ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 21, 2017

RANGI ZA KANSAI PLASCON ZATAMBULISHWA RASMI JIJINI ARUSHA


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kansai Plascon Tanzania Amin Habib   akihutubia wageni waalikwa katika  ya hafla ya  kununua oparesheni za Kampuni ya Rangi ya Sadolin nchini.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kansai Plascon Tanzania Amin Habib  akiwa katika picha ya pamoja mara baada   ya hafla ya  kununua oparesheni za Kampuni ya Rangi ya Sadolin nchini.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kansai Plascon Tanzania Amin Habib, akiongea Na Distributors wa Arusha kuhusu ununuaji wa operasheni za Kampuni ya Rangi ya Sadolin.

Wadau wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla ya  kununua oparesheni za Kampuni ya Rangi ya Sadolin nchini 
Meneja wa Kanda wa Kampuni ya Kansai Plascon Tanzania(Tanzania Kaskazini), akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, jana, kuhusu kampuni hiyo kununua oparesheni za Kampuni ya Rangi ya Sadolin nchini  kushoto ni Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo Hussein Jamal.


  Kansai Plascon yainunua Kampuni ya rangi ya Sadolin ya Tanzania


Arusha: Kampuni ya Kansai Plascon Afrika ltd. Ambayo ni kampuni tanzu ya kampuni ya rangi ya Kansai iliyoko Japan, imehitimisha makubaliano yake ya kununua shughuli za rangi za Sadolin nchini Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki.  Hii ilitangazwa na Deodatus Makumpa Meneja wa Kanda ya Kaskazini, Plascon Tanzania wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika Hotel ya Arusha Jijini Arusha

Kampuni ya rangi ya Kansai ni kampuni ya kimataifa ambayo inaendesha shughuli zake nchini Japan, China, Mashariki ya Kati, Ulaya na Afrika. Bidhaa zake inazotoa zinajumuisha upambaji, Viwanda, rangi za kulinda na mitambo, ina vituo vya utafiti na maendeleo nchini Japan, India na Afrika Kusuni.

“Tumefurahishwa na mafanikio haya. Kupitia haya, tutaweza kutumia nembo yenye nguvu ya urithi wa Kansai, uwezo wa kimataifa wa kiufundi, na utendaji wa kuaminika, kutupatia uwezo mpya, kuweza kupata teknolojia mpya na utambuzi ambao ni muhimu zaidi katika kuendelea kukuza nembo hii,” alisema Makumpa

Akiongea kuhusu sababu za kuinunua, Gary van der Merwe, Rais wa Kampuni ya Plascon Afrika Mashariki alisema kwamba makubaliano haya yanadhihirisha nia ya Kansai Plascon katika kujiendeleza zaidi duniani. “Afrika Mashariki ni moja kati ya ukanda ambao unakuwa haraka zaidi kiuchumi barani Afrika. Kwa ukuaji wa kasi wa daraja la kati, kuongezeka kwa nguvu ya utumiaji na kukua kwa miji, huu ni muda muafaka wa kuingiza sokoni bidhaa zetu mbali mbali kwaajili ya kuboresha zaidi mtindo wa maisha yao wakati huo huo tukiwa tunaongeza kuenea kwetu duniani”.

Ununuzi huu hautakuwa na mabadiliko katika uongozi wa juu na nafasi zozote zingine katika kampuni ya Sadolin. Kampuni itaendelea kufanya shughuli zake kama ambavyo ilikuwa ikifanya kwa kutumia wafanyakazi waliopo. Amin Habib ambaye anakalia kiti cha Mkurugenzi Mtendaji amesema kwamba ununuzi huu utapelekea katika matokeo bora na ufanisi zaidi ambao utanufaisha kampuni hii ya rangi. Kuanzia katika teknolojia mpya na iliyoboreshwa kutoka katika kampuni ya rangi ya Kansai ambayo ni kampuni ya kumi ya rangi duniani.

Tangu ianzishwe mwaka 1967 nchini Tanzania, kampuni ya rangi ya Sadolin imekua na kuwa kampuni kubwa zaidi ya uzalishaji wa rangi, ikiwa inajivunia zaidi ya 50% ya soko katika rangi za kulinda naza kutengenezea magari.


Amin Habib amewahakikishia wateja kwamba mabadiliko haya hayatakuwa na athari zozote katika utaratibu wa uendeshaji wa shughuli za kampuni uliopo sasa. Lakini mabadiliko yanakuja na mbinu bora za uendeshaji kwaajili ya kuwahudumia vyema wateja, kwa ufanisi zaidi na kwa bidhaa zenye kiwango ambazo hawakutarajia.” Wauzaji wetu wote, Maghala na maduka yatabakia kuwa wazi kuwahudumia kwa bei ile ile nzuri ambayo wamekuwa ukiifurahia kwa miaka mingi. Katika miezi michache ijayo, tukiwa tunakamilisha mabadiliko, tutaanza kuingia katika kutekeleza makubaliano ya mkataba, kumalizia bidhaa zenye nembo ya Sadolin kutoka katika maghala yetu na kuwasisitiza wateja wetu kuuliza bidhaa zenye nembo ya Plascon kutoka kwa wauzaji wao”.

Kwa kutambua kwamba kununua na kujiunga kwa makampuni huja na hali ya kutokuwa na uhakika katika mtazamo wa raslimali watu na mtazamo wa kiuendeshaji, Gary van der Merwe alisema kwamba kwa kuwa Sadolin kama biashara tayari ilikuwa inaendesha shughuli zake kwa ufanisi, mkakati utakuwa ni kuboresha zaidi na kuongeza katika uendeshaji uliopo ili kuboresha ufanisi.

“Tutafanya kazi ya kupanua zaidi teknolojia ya hali ya juu iliyopo ambayo tumeikuta ikiwa inafanyakazi. Lengo letu litabakia katika kuwekeza katika teknolojia ya kiwango cha juu kuwapa wateja wetu rangi za kiwango cha juu zaidi katika soko.” Alisema.

Lengo letu ni kudumisha nafasi yetu kama wazalishaji wa rangi wanaoongoza Tanzania na Afrika Mashaririki kwa kuendelea kuboresha ili kuweza kufikia mahitaji ya wateja wetu yanayobadilika kila siku na kubakia washindani katika soko. “Soko la Tanzania wanaweza kutarajia kuanza kutumia application ya simu ya Plascon Visualizer, ambayo itawaruhusu watu kucheza na kufanya majaribio ya rangi kwaajili ya nyumba zao na miradi yao kabla ya kwenda kwa wauzaji kutoa oda zao.”

Sadolin imefurahia nafasi yake na kushikilia soko la rangi katika kanda hii. Ununuzi huu utaongeza mapato ya Kansai Plascon na nafasi yake kama ambavyo inataka kuimarisha nafasi yake kama kampuni ya rangi inayoongoza Afrika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.