ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 31, 2017

POLISI MWANZA YAPIGA STOP MABASI MABOVU 22.



NA ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGOBLOG

Zaidi ya abiria mia tano waliokuwa wakitarajia kusafiri kwenda mikoa mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, leo wamejikuta wakikabiliwa na adha ya usafiri, baada ya Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza kupitia kikosi cha usalama barabarani, kuzuia mabasi 22 kati ya 79 yaliyokaguliwa kutoendelea na safari kutokana na ubovu.

Jeshi hilo limelazimika kuendesha Oparesheni hiyo ya kustukiza katika vituo vikuu vya mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi vya Buzuruga na Nyegezi, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa abiria kuwa baadhi ya mabasi, yamekuwa yakikwamisha safari zao na kuwalaza barabarani kutokana na ubovu.

Kutokana na Oparesheni hiyo mabasi 57 kati ya sabini na tisa yametozwa faini, baada ya kubainika kuwa na makosa mbalimbali, huku ishirini na mbili yakizuiwa kabisa kutoendelea kutoa huduma kutokana na ubovu, hatua ambayo inalenga pia kupunguza ajali za barabarani zitokana na ubovu wa Magari.   

Kamanda wa polisi mkoa wa Ahmed Msangi, amesema kuwa zoezi la ukaguzi wa mabasi yaendayo mikoani litakuwa endelevu, ili kudhibiti mianya ya madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani kwa kuendesha mabasi mabovu, yanayochangia kuwepo na ajali za barabarani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.