ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 26, 2017

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA ASHIRIKI UZINDUZI WA JENGO LA HUDUMA ZA MATIBABU YA BIMA YA AFYA BUGANDO

 Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula leo ameshiriki Uzinduzi wa Jengo la Huduma za Matibabu ya Bima ya Afya lililojengwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando Jijini Mwanza zoezi mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela

Akizungumza katika Uzinduzi huo Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kusifu uongozi wa hospitali ya Bugando kwa hatua kubwa ya maendeleo waliyoyafikia kwa haraka na muda mfupi  amewaasa watumishi wa hospitali hiyo kuongeza uadilifu na uwajibikaji huku akiwahakikishia utayari wa Serikali katika kuunga mkono na  kuisaidia hospitali hiyo.



‘… Bugando ya sasa si ile ambayo tulikuwa tumeizoea huduma nyingi na bora zinapatikana hapa kama tunavyoona  tiba ya saratani inafanyika, magonjwa ya moyo inafanyika,  upasuaji unafanyika na hata yale ya ubongo kwa hiyo hakuna kitachobaki au kupungua, Mimi kama mwakilishi na kama msaidizi wa Mhe Rais nitakuwa shuhuda wakuyasemea na kushawishi namna bora ya kuiona Bugando kwa jicho la pili ili huduma zinazoihelemea hospitali yetu ya Muhimbili na Ocean Road  zianze pia kutolewa hapa hospitali ya Bugando …’ Alisema

Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula ametumia hadhara hiyo kuwasilisha salamu za Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula aliyeshindwa kuhudhuria uzinduzi huo kutoka na vikao vya kamati za bunge vinavyoendelea

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Mhe Raymond Mwamgalwa  amesema kuwa kilichofanyika ni utekelezaji wa  Ilani ya chama chake kinachounda Serikali hivyo anaridhishwa na utekelezaji huo wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kunakoenda  sambamba na ile sera ya HAPA KAZI TU

Nae mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya Bugando na baba askofu mkuu wa jimbo katoliki  Mwanza Thadei Rwai’ chi amemuhakikishia mgeni rasmi utayari wa kanisa katika kuhakikisha linasaidia wananchi kwa utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kijamii

Uzinduzi huo wa la huduma za matibabu ya bima ya afya hospitali ya kanda Bugando ulihudhuriwa na wabunge mbalimbali wa mikoa ya kanda ya ziwa, wawakilishi wa wakuu wa mikoa, wawakilishi wa wakuu wa wilaya, wataalamu wa wizara ya afya na viongozi wa dini

‘Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ’

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.