ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 21, 2017

IDADI YA WALIOKUFA KUTOKANA NA MAPOROMOKO YA UDONGO SIERRA LEONE YAFIKIA WATU 500

MAOFISA wa serikali ya Sierra Leone wamesema kuwa idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na maporomoko ya udongo na mafuriko yaliyotokea Jumatatu iliyopita nchini humo imekaribia 500.

Ripoti iliyotolewa na serikiali ya Freetown imesema 156 kati ya waliofariki dunia ni watoto wadogo.

Shirika la Hilali Nyekundu la Sierra Leone limetangaza kuwa watu wasiopungua elfu tatu wamepoteza makazi yao kutokana na maafa hayo ya maporomoko ya udongo na mafuriko katika mji wa milimani wa Regent nje kidogo ya Freetown na kwamba watu wengine 500 hawajulikani waliko. 

Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone ameomba misaada ya kimataifa kwa ajili ya wahanga wa maafa ya hayo. 

Mazishi ya wahanga wa maporomoko ya udongo, Sierra Leone
Duru za hospitali za Sierra Leone zinasema kwamba, kuna upungufu mkubwa wa suhula za tiba na huduma za afya kwa majeruhiwa wa maafa hayo na hata mochari na nyumba za kuhifadhia maiti.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.