ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 29, 2017

SIMBA U20 YAAGA MASHINDANO YA HISANI YA ATF YATOLEWA NA TANZANIA PRISONS KWA PENATI

 BEIKI wa Simba U20, Jacob Jalala (kulia) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Mohamed Rashid, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani
 BEKI wa Tanzania Prisons, Michael Ismail (kushoto) akijaribu kumpita mchezaji wa Simba U20, Rashid Juma, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani
 BEIKI wa Simba U20, Abdallah Rashid (kulia) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Kassim Hamis, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani
 KIPA wa Tanzania Prisons, Aron Kalambo, akiokoa moja ya hatari langoni kwake wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani
 WACHEZAJI wa Tanzania Prisons, wakimdhibiti mshambuliaji wa Simba U20, Abilay Issa, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani
  MSHAMBULIAJI wa Simba U20, Said Hamis (kulia) akichuana kuwania mpira na beki wa Tanzania Prisons, Sharif Shaban, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani
 BEKI wa Simba U20 Erick Costantine (kulia) akijaribu kumzuia mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Cleophace Anthony, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani
 MCHEZAJI wa Simba U20, Abilay Issa (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Tanzania Prisons, Sharif Shaba, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani


TIMU ya Vijana wa Simba chini ya umri wa miaka 20, jana walishinda kuungana na wenzao wa Yanga katika fainali ya Mechi za Hisani kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI baada ya kufungwa na Tanzania Prisons kwa mikwaju ya penati 6-5 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu wa Sokoine jijini Mbeya.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote kutoka uwanjani bila kupata bao, huku timu zote zikicheza kwa taadhari na kufanya mashambulizi ya kushitukiza.

Katika mchezo huo Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 69 kupitia kwa mshambuliaji wake, Dadi Mbarouk, baada ya kuwatoka mabeki wa Tanzania Prisons Aron Kalambo, aliyekuwa ametoka golini akijaribu kuwahi kumzuia na  kupishana na mpira uliotinga wavuni.

Bao la kusawazisha la Tanzania Prisons, lilifungwa na Kassim Hamis, kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 79, baada ya mchezaji wa Simba U20, kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari na kufanya dakika 90 kumalizika timu hizo zikiwa sare kwa kufungana 1-1.

Baada ya sare hiyo timu hizo zilikwenda katika hatua ya matuta, ambapo zilipigwa jumla ya penati 8, na Tanzania Prisons wakikosa 2 na kupata penati 6 na Simba wakikosa 3 na kupata penati 5.

Simba wameungana na wenzao Mbeya City Kikosi cha kwanza ambao walitolewa na Kikosi cha Yanga U20 kwa kukubali kichapo cha mabao 3-0 katika mechi hizo za Hisani zilizoandaliwa na Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS, na kushirikisha jumla ya timu Nne za Yanga U20 na Simba U20 kutoka jijini Dar es Salaam, Mbeya City na Tanzania Prisons vikosi vya kwanza Ligi Kuu Bara.

Mchezo wa fainali unachezwa leo jioni kwenye Uwanja huo wa Sokoine kati ya Yanga U20 na Tanzania Prisons.

Akizungumzia matokeo hayo Kocha wa Simba U20, Nico Kiondo, alisema kuwa kwa upande wao hali ya hewa ilichangia kwa kiasi kikubwa kupata matokeo hayo lakini pia maandalizi yao hayakuwa ya kutosha kwani wachezaji wengi ni wageni ndani ya Kikosi chao.

''Kwa kweli hali ya hewa imetugharimu kupoteza mchezo wa leo lakini pia hatukuwa na mazoezi ya kutosha kabla kwani wachezaji wengi ni wageni waliojiunga na timu msimu huu''. alisema Kiondo

Kwa upande wake Kocha wa Tanzania Prisons, Abdalla Mohamed, alisemakuwa timu yake imejitahidi kupata matokeo hayo japo imecheza na kikosi cha pili cha Simba kutokana na timu zote kucheza kwa uangalifu kwani hawakuwa na maandalizi ya kutosha baada ya usajili wa wachezaji wapya ambao wengi wao ndiyo walicheza ili kuwajaribu ili kuona mapungufu, huku wengine wakitarajia kucheza katika mchezo wa leo dhidi ya Yanga.

''Nimeona mapungufu kwa wachezaji wangu na hasa kwa safu ya ushambuliaji, nitayafanyia kazi ili kupata matokeo mazuri katika mechi zijazo kwani wachezaji wangu wengi ni wageni ambao tumewasajili msimu huu bado hawajazoea hali ya hewa, na wengini nitawajaribu katika mchezo wa leo dhidi ya Yanga''. alisema Mohamed

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.