ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 16, 2017

RAIS MAGUFULI ATOA SALAMU ZA POLE KWA WAZIRI MWAKYEMBE.

Rais Dkt. Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kufuatia kifo cha mkewe Bi. Linah George Mwakyembe kilichotokea usiku wa kuamkia leo na kusema ameshtushwa na taarifa hizo.

Katika salamu hizo, Rais Magufuli ameelezea kushtushwa na kusikitishwa na kifo hicho, na kusema yeye na familia yake wanaungana na familia ya Dkt. Mwakyembe katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

“Nakupa pole sana Dkt. Mwakyembe kwa kuondokewa na mkeo mpendwa Bi. Linah, natambua hisia za maumivu ulizonazo wewe na familia nzima, nyote nawaombea Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Namuombea Marehemu Linah George Mwakyembe apumzishwe mahali pema peponi, Amina”, amesema Mhe. Rais Magufuli.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.