ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 1, 2017

Ripoti: WANAJESHI WA ISRAEL WAMEUA WATOTO ELFU 3 WA KIPALESTINA.

Wizara ya Habari ya Palestina imesema, watoto zaidi ya elfu tatu wa Kipalestina wameuliwa na jeshi katili la Israel tangu ilipoanza Intifadha ya Pili mwezi Septemba 2000.

Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa leo na wizara hiyo kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Kuwalinda Watoto ambayo huadhimishwa Juni Mosi kila mwaka kote duniani, mbali na watoto elfu tatu kuuawa, wengine zaidi ya 13 elfu wamejeruhiwa na wanajeshi hao.
Ripoti hiyo imebainisha kuwa, watoto wasiopungua 72 wameuliwa na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel tangu mwezi Oktoba 2015, wakati ilipoanza Intifadha ya Tatu ya Quds.
Wizara ya Habari ya Palestina imefichua kuwa, mtoto mdogo zaidi aliyeuliwa shahidi na wanajeshi wa Israel ni Ramadan Mohammad Faisal Thawabta, aliyekuwa na miezi minane tu, ambaye alifariki dunia Oktoba 30, 2015 baada ya kuvuta gesi ya kutoa machozi iliyofyatuliwa na wanajeshi Wazayuni katika maandamano yaliyofanyika mjini Beitul Fajjar, kusini mwa Beitul Lahm.
Watoto wa Kipalestina katika jela za Israel.
Kadhalika ripoti hiyo ya Wizara ya Habari ya Palestina imebainisha kuwa, watoto zaidi ya 12 elfu wa Kipalestina wametekwa nyara na askari wa Israel na kuzuiliwa chini ya mazingira magumu, katika kipindi cha miaka 17 iliyopita.
Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za wafungwa wa Palestina la Addameer, wanajeshi katili wa Israel wamewahukumu vifungo jela watoto 300 wa Kipalestina tangu mwezi Aprili mwaka huu hadi sasa, vikiwemo vifungo vya hadi miaka 20 jela. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.