ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 18, 2017

WANANCHI MTAA WA MTAA WA KAGOMU MAHINA WATAKA MKURUGENZI KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI WA ARDHI

Na PETER FABIAN, MWANZA.
WAKAZI wa Mtaa wa Kagomu na maeneo ya Kata ya Mahina Wilaya ya Nyamagana wamemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomon Kibamba kuacha kutengeneza migogoro ya ardhi katika maeneo yao na badala yake apeleke watalaam wake kupima maeneo yao kama alivyoagizwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi hivi karibuni alipokuwa katika ziara yake ya kikazi.

Hayo yalijitokeza jana wakati wa mkutano wa hadhara wa Diwani wa Kata ya Mahina, James Bwire (CCM) ambaye ni Meya wa Jiji la Mwanza uliofanyika katika mtaa wa Kagomu wakimuomba Meya huyo afatilie agizo la Waziri William Lukuvi alilolitoa wakati alipofanya mkutano wa hadhara kwenye viwanja hivyo kutokana na muda aliotoa wa upimaji shirikishi kuwa mdogo ili hali bado wataalamu awajafika kuwapimia.

Martine Magoma akihoji wakati wa maswali kwa Diwani Bwire alisema kwamba muda uliotolewa na Waziri Lukuvi wa Jiji kupima maeneo ya wananchi ni mdogo ambapo mwisho ni Juni 6 mwaka huu lakini hadi sasa wataalamu wa Idara ya Mipango Miji kitengo cha upimaji hawajawahi kuonekana na wananchi hawajui nini kinaendelea na wananchi wako tayari kulipia gharama za Sh 150,000/- za upimaji shirikishi.

Akijibu maswali ya wananchi Meya Bwire alisema kwamba atalifikisha kwa Mkurugenzi ili wataalam wafike kuja kuwapimia na kinachotakiwa ni kujiandaa kulipia gharama hizo kwa kuwasiliana na wenyeviti wa mitaa yenu na Mtendaji wa Kata na hili litasaidia kuanza utaratibu wa kumilikishwa maeneo ya makazi yenu kama alivyoagiza Waziri Lukuvi.

Meya akihutubia wananchi wa mtaa huo alikataa la Mwenyekiti wa mtaa wa Igelegele, Dancan Nyamgoncho (CHADEMA) kwa kuwa ni Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) na maswali yake anatakiwa kuuliza huko na kumtaka akaye chini awachie wengine, akieleza  kusikitishwa kwake na Mkurugenzi wake wa Jiji kutaka kutengeneza mgogoro wa ardhi hilo akitumia mwenyekiti mmoja (hakumtaja) kudai eneo langu ninalojenga Hospitali kuwa ni mali ya wananchi.

 “Kuna mambo yanaendelea pale Jiji ambayo baadhi ya wataalam na watumishi wamekuwa na tabia ya kutafuna fedha za Halmashauri ikiwemo kufanya mambo ya hovyo, sasa tangu nimechaguliwa kuwa Meya nilikaa na Madiwani wenzangu na kukubaliana kukataa Jiji letu kuwa shamba la bibi kwa kuchotwa fedha za walipa kodi kutumika kinyume cha utaratibu kamwe hili sitokubaliana nalo,”alisema.

Bwire alieleza kuwa nachojua Mkurugenzi ni Mtendaji siyo mwanasiasa hivyo ache kutuingilia wanasiasa na kutufatafata kwa kutaka kutuchonganisha na kuturetea migogoro ya ardhi badala yake afanye kazi ya kupima maeneo yetu kama alivyoagizwa na Waziri na kama anahitaji eneo langu basi anilipe fidia na kulichukua awape watu anaowahitaji lakini siyo kuanza kutengeneza visa baada ya kumkatalia ulaji kule Jiji.

Naye Mwalimu Steven Machunda akijitokeza katika mkutano huo na kueleza kuwa eneo analojenga Meya Hospitali ni eneo lake halali kwa kuwa baba yake mzazi na yeye waliamua kumuuzia mwaka 2009 ili kupata fedha wakati anashinda kwenda Chuo cha Ualimu Mrutunguru kutokana na kukosa fedha mwanzoni ndipo familia ikamua kumuuzia kihalali na kumukabidhi nyaraka zote.

Machunda alisema kwamba hata baada ya kumaliza Chuo na kupata ajira  amekuwa akipata msaada kutoka Meya kama mtu ambaye alimpatia mwanga hivyo kama kuna mtu anadai eneo hilo ni lake ajitokeze hapa ili ni muone na kumuhoji hali iliyoibua shangwe kwa wananchi na kumuonya mkurugenzi huyo kuacha kumchonganisha na kiongozi huyo mpenda maendeleo na badala yake atafute njia nyingine ya kumchafua.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.