ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 18, 2017

WANACHAMA MWANZA WAANDAA SHEREHE YA UBINGWA VILLA PARK MWANZA KUIPONGEZA YANGA AFRICANS


PICHA KUTOKA MAKTABA:- Aliyekuwa Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (ambaye ni mbunge sasa wa Jimbo la Nyamagana) wakati akikabidhiwa na wanachama wa Yanga Kombe la Ubingwa lililonyakuliwa na timu hiyo katika msimu wa 2012-2013 kama ishara ya kombe hilo kuingia jijini Mwanza ni katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo kulikuwa na mechi ya kirafiki baina ya Mabingwa Yanga na Mabingwa KCC ya Uganda. Matokeo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Na PETER FABIAN, MWANZA.
WANACHAMA na mashabiki wa timu ya Yanga Africans Jijini Mwanza wameandaa sherehe na chakula cha usiku baina yao, wachezaji na viongozi wa juu wa Klabu hiyo watakaoambatana na timu eneo la Villa Park Resort baada ya mchezo wa mwisho wa Ligi kuu ya Vodacom (VPL) utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Akizungumza na GSENGO BLOG Mjini Mwanza, msemaji wa tawi la Mwanza lililopo mtaa wa Rufiji, Sele Yanga  maarufu kama 'Lialia' alisema kwamba uamuzi huo umefikiwa na wanachama na mashabiki wa timu hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru wachezaji, benchi la ufundi na viongozi kwa ushirikiano na umoja uliowezesha kutwa ubingwa wa Ligi kuu kwa mara ya tatu mfululizo.


Sele alisema kwamba baada ya sherehe hiyo siku ya Jumapili wachezaji, benchi la ufundi na viongozi walioambatana na timu jijini Mwanza watashiriki katika uzinduzi wa matawi mawili ya Mwanza mjini na Mecco majanini lililopo Nyakato ikiwa ni sehemu ya pili ya mashabiki kupiga picha na wachezaji wa timu na viongozi sanjari na kuongeza hamasa na kuwaaga kabla ya kurejea jijini Dar es salaam.


“Tunataraji kuwa na mapokezi makubwa pale uwanja wa ndege wa Mwanza siku timu itakapowasili kuja kucheza na timu ya Mbao FC ya Jijini Mwanza katika mechi ya mwisho ya kufunga msimu wa Ligi kuu ya VPL 2016/2017 ambayo Yanga Africans inatwa taji la Uchampioni kwa mara ya tatu mfululizo, rai yangu kwa wanachama na mashabiki wajitokeze kwa wingi siku ya Jumamosi katika uwanja wa CCM Kirumba,”alisema.


Naye Meneja wa Burudani wa Villa Park Resort, Ramadhan Maganga alikiri kuwa na program ya kuandaa chakula cha usiku (Dinner) kwa viongozi, wachezaji, benchi la ufundi, wanachama na mashabiki wa timu ya Yanga Africans ambapo kwa wanachama na mashabiki watakaotaka kujumuika kwa chakula na wachezaji na viongozi watachangia gharama kidogo.


Maganga alisema kutakuwa na eneo maalum limeandaliwa kwa ajili ya kutoa fursa kwa mashabiki na wanachama ya kupiga picha ya pamoja na wachezaji na viongozi ambapo mlangoni wataingia kwa kuchangia Sh 3,000/- na kutakuwa na burudani ya muziki kutoka katika bendi ya Villa Park ya Super Kamanyola .


Meneja huyo alisema kwamba tayari wameisha toa taarifa kwa barua kwa viongozi wa Klabu hiyo Makao Makuu na kupewa rukusa hiyo ambapo watashirikiana na viongozi na wanachama wakiwemo baadhi ya mashabiki kuanda shughuli hiyo na kutoa wito kwa mashabiki kuzikiliza utaratibu kupitia vituo mbalimbali vya redio na magazeti kujua nini watafanya kabla ya kujumuika na wachezaji na viongozi katika sherehe.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.