ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 4, 2017

UTATA WAZUKA USHAHIDI KESI YA MAUAJI YA BARLOW.

NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza
USHAHIDI wa shahidi wa 16 Vedastus Pius, kesi ya mauji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow umeibua shauri dogo katika kesi kubwa mahakamani hapo.

Kesi hiyo imeibuliwa jana katika Mahakama kuu kanda ya Mwanza mbele ya jaji Sirilius Matupa na wakili wa kujitegemea Maduhu Ngasa baada ya kuonekan kweny baadhi ya nyaraka za ushahidi kufutika kwa tarehe husika jambo ambalo lilizua utata na kusababisha kuwepo kwa kesi ndogo.

Baada ya wakili  huyo kutoa hoja zake mtuhumiwa namba  sita Abdalla Petro Amos Abdalla Ndayi (22) alisimama kizimbani kwa ajili ya kutoa ushahidi wake.

Abdalla ameiambia Mahakama kuwa amefikishwa mahakamani kwa kosa la mauji kesi namba 192/2014   ambapo alikamatwa mnamo Novemba 2 mwaka 2012 saa 12 alfajiri na kwamba anahusika na mauji ya askari.

"Wakati nakamatwa sikuelezwa kosa langu na kupelekwa kituo kidogo cha polisi cha Pamba na nilipofika Pamba niliambiwa kuwa nimekuja kupanga biashara sehemu ambayo hairuhusiwi nikawekwa ndani siku mbili" amesema Abdalla.

Amesema mnamo Novemba 4 mwaka 2012 akatolewa na kupelekwa kituo kikubwa cha Nyamagana  na kuwekwa ndani  na baada ya hapo walifika askari watatu ambao hakuwafahamu na kumuita na kwamba hakuitika.

Amesema hakuitika kwa sababu hayakuwa majina yake na kwamba anaitwa Abdalla Petro  ndipo alitolewa kwa ajili ya kuchukuliwa maelezo.

" Kutokana na shahidi wa 16 hauwahi kuniohoji maelezo aliyokuwa akiyaandika ni ya kwake na baada ya hapo nilisaini kwa shinikizo ili nisiuwawe mnamo Novemba 5 mwaka 2012 na sio Novemba 3 mwaka 2012 kama shahidi alivyoeleza" amesema Abdalla.

Aidha baada ya mtuhumiwa kumaliza ushahidi wake  Jaji matupa aliwaruhusu mawakili wa pande zote mbili kutoa hoja zao kuhusiana na shauri hilo na Jaji aliihairisha kesi hiyo ambapo uamuzi utatolewa asubuhi hii kabla ya kuendelea na kesi kubwa ya mauji.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.