ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 3, 2017

RIPOTI YA HUMAN RIGHTS WATCH: MAKUMI YA RAIA WAMEUAWA KATIKA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI.


Makumi ya raia wameuawa katika Jamhuri ya Afrika Kati kufuatia kuzuka mapigano yanayoendelea kushuhudiwa nchini humo kati ya makundi ya wabeba silaha.
Hayo yamo katika ripoti ya Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch ambayo imefichua kuwa, raia wapatao 45 wameawa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kutokana na machafuko yanayoendelea kuikumba nchi hiyo.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa,  mapigano hayo yameyakumba zaidi maeneo ya miji ya Bambari, Ouaka, mkoa wa katikati na Makoum, kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Inaelezwa kuwa, mbali na mapigano hayo kusababisha mauaji makubwa yamepelekea pia wakazi wengi wa maeneo hayo kuwa wakimbizi.
Kikosi cha kusimamia amani cha UN katika Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika mgogoro, mwaka 2013 baada ya kuzuka mapigano ya kikaumu yaliyopelekea kuondolewa madarakani serikali ya rais François BozizĂ©. 
 
Hivi karibuni Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitaka kukomeshwa haraka iwezekanavyo, mapigano na vitendo vya utumiaji mabavu vya makundi ya wabeba silaha, Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Taarifa iliyotolewa na baraza hilo la usalama la Umoja wa Mataifa mbali na kuonyesha wasiwasi wake juu ya mapigano hayo nchini CAR, liliyataka makundi ya wabeba silaha hususan 'Harakati ya Kitaifa kwa Ajili ya kufufua nchi FPRC' na kundi la 'Umoja kwa ajili ya Amani ya Afrika ya Kati UPC' kukomesha uhasama na mapigano yao nchini humo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.