ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 18, 2017

MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA AWATAKA POLISI WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka askari polisi wanawake kutoka kwenye Shirikisho la Majeshi la Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) washiriki kikamilifu katika oparesheni mbalimbali ambazo zinafanyika kwenye ukanda huo kama hatua ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu.

Samia Suluhu Hassan, amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka nchi wanachama wa SARPCCO katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia amewahimiza askari polisi wanawake kufanya kazi kwa bidii na kujituma, hatua ambayo itawasaidia kupanda vyeo kama askari wanaume katika maeneo yao ya kazi, na kusisitiza kuwa, muda wa kulalamika kuwa hawapandishwi vyeo umeshapitwa na wakati bali kwa sasa wachape kazi na waonyeshe kuwa wanaweza majukumu yao wanayopangiwa ili waweze kupanda vyeo.
Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania
Kuhusu utendaji kazi wa polisi wanawake, Makamu wa Rais Bi Samia Suluhu Hassan amewataka polisi hao kutumia mkutano huo wa siku tatu kujadili kwa kina namna ya kuondoa changamoto hizo zinazorudisha nyuma utendaji wao wa kazi.
 
Amesema kama polisi wanawake wataacha majungu na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwao watafikia malengo yao haraka hasa katika kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu ikiwemo biashara ya dawa za kulevya.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amesema ana imani kubwa kuwa mafunzo hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa polisi hao wanawake kuimarika ipasavyo katika utendaji wao wa kazi

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.