ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 12, 2017

JARIBIO LA KUTAKA KUMUUA KIONGOZI WA KOREA KASKAZINI NI TANGAZO LA VITA.


Korea Kaskazini imelaani tena jaribio la kutaka kumuua kiongozi wake ambalo limetekelezwa na mashirika ya kijasusi ya Marekani na Korea Kusini na kulitaja jaribio hilo kuwa sawa na tangazo la vita.
 Ubalozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa umetoa taarifa na kusema nchi hiyo itaanza oparesheni dhidi ya magaidi ambao walihusika na njama ya kutaka kumuua kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un.

Taarifa hiyo imesema Pyongyang ina azma imara ya kuwasaka bila huruma na kuwaangamiza magaidi wote wa shirika kuu la kijasusi la Marekani CIA na shirika la kijasusi la Korea Kusini waliohusika na njama hiyo.

Taarifa hiyo imetoa wito kwa nchi za Umoja wa Mataifa kuunga mkono jitahada za Korea Kaskazini katika kukabiliana na magaidi hao waliotumwa na CIA.
Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilitoa taarifa na kusema kuwa, CIA na Idara ya Intelijensia ya Korea Kusini zinapanga kutumia silaha ya kemikali kumuua kiongozi wa nchi hiyo.

Haya yanajiri katika hali ambayo, hali ya taharuki ingali imetanda katika Peninsula ya Korea haswa baada ya Marekani kufanyia majaribio kombora lake la "Minuteman III" lenye uwezo wa kupiga umbali wa karibu kilomita elfu sita na 760.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.