ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 20, 2017

TIMU YA PAMOJA YACHANJA MBUGA

NA ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza

TIMU ya mpira ya Pamoja Sport Club imeingia mitini kwa kushindwa kuonekana kwenye mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 15 yanayoendelea kwenye uwanja wa Nyamagana kwa ajili ya kuibua vipaji vya vijana hao

Mashindano yaliyoandaliwa na Chama cha Mpira wa miguu Wilaya ya Nyamagana kwa ajili ya kuibua vipaji vya vijana wenye umri chini ya miaka 15 ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika soka hapo baadae
.
Akizungumza na Gsengo blog Mwenyekiti wa Mashindano hayo Selemani Makasi amesema timu hiyo imeshindwa kuhudhuria leo kwenye mechi hiyo baada ya kuwaondoa vijana watatu  hapo jana waliokuwa wamezidi umri hatua iliyopelekea kutoleta timu yao leo kwa ajili ya kuendelea na mashindano hayo.

“Changamoto tulionayo katika kuibua vipaji kwa watoto ni  umri wa miaka 15,timu nyingi zinazoshirki mashindano haya zinalenga ushindi tu lakini lengo letu ni kuibua vipaji,sasa kilichotokea kwa timu ya pamoja ni baada ya jana kuwaondoa vijana wao 3 waliozidi umri  wameamua kuzila mashindano”amesema Makasi.

Amesema Viongozi pamoja na makocha wa timu hizo wanatakiwa kuwa wa kweli kwani mashindano yanalenga kuibua vipaji na kuleta soka lenye ubora kwa watoto.

Timu ya Pamoja Sport Club  ilitakiwa kuchuana leo na Alliance kwenye uwanja huo hatua iliyowafanya wapinzani wao kujizolea pointi tatu baada ya kushindwa kuonekana.

Awali akizungumza na G sengo Mwenyekiti wa Mashindano timu ya Allince  Yusuph Budodi ameeleza kuwa huenda timu hiyo imehofia kufungwa, baada ya kushuhudia msululu wa magoli 18 kwenye mchezo wa pili kutoka alliance dhidi ya  ElCT S.A .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.