ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 6, 2017

TANESCO YAKABIDHI MRADI WA UMEME KWENYE SHULE YA MSINGI GARAGAZA HUKO KIBAHA

 Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu, (kushoto), akipena mikono na Afisa Elimu, (Taaluma), mkoawa Pwani, Bw.Shirley Membi Swai, wakati wa makabidhiano ya mradi wa uwekaji umeme katika shule ya Msingi Galagaza, kata ya Msangeni, Kibaha kwa Mfipamkoani Pwani, Aprili 7, 2017. Mradi huo una thamani ya Shilingi Milioni 10. Anayeshuhudia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw.Shaaban Langweni

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limekabidhi mradi wa umeme kwenye majengo ya shule ya msingi Galagaza iliyoko, kata ya Msangani wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
Akikabidhi mradi huo wenye thamani ya Shilingi Milioni 10, wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo leo Aprili 7, 2017, Meneja wa TANESCO, Mkoani Pwani, Mhandisi Martin Madulu, alisema “mradi ulihusisha utandazaji nyaya za umeme (wiring installation),  ufungaji wa power circuit- breaker, taa, pamona na ufundi kwenye majengo yote ya shule ikiwemo ofisi ya walimu”. Alifafanua meneja huyo.
Akifafanua zaidi, Mhandisi Madulu alisema, “tumeona tuwaunge mkono shule kwenye level ya msingi kwani ni maandalizi mazuri kwa wataalamu wa baadaye kwani sasa mazingira yatakuwa mazuri kwa kusoma, pia mazingira yatakuwa mazuri kwa walimu kuandaa masomo yao na tunaamini italeta matokeo chanya.” Alisema.
Alisema, TANESCO imeamua kusaidia shule hiyo katika harakati za shirika kurudisha sehemu ya faida kwa wananchi, lakini pia kuhamasisha umma kutumia umeme.
“Ni fursa kwenu kutumia vizuri umeme huu, ili muweze kufanya vizuri zaidi katika masomo yenu, tunategemea kiwango cha ufaulu kitaongezeka kwani hivi sasa mnaweza kutumia fursa mbalimbali za kupata elimu kama matumizi ya kompyuta, ambazo zinahitaji uwepo wa umeme.” Alifafanua.
Akipokea mradi huo, Afisa Elimu (Taaluma) wa Mkoa wa Pwaniambaye alimwakilisha Afisa Elimu wa Mkoa huo, Bw.Shirley Membi Swai, aliishukuru TANESCO kwa msaada huo na kuwataka wanafunzi na walimu kutumia vizuri uwepo wa umeme shuleni hapo kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwani sasa mazingira ya kusoma ni mazuri zaidi.
“ Huu ni mchango mkubwa sana katika maendeleo ya elimu nchini, msaada huu umekuja kwa muda muafaka kwani hivi sasa, serikali tayari imeanza kufundisha TEHEMA katika shule na kufundisha kwa kutumia mtandao (digital learning na tayari umeshaanza hapa nchini, ambapo wanafunzi na walimu wameanza kutumia kompyuta ndogo (tablets).” Alisema.
Pia nawashukuru TANESCO kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwapatia wanafunzi elimu bure, msaada huu unaongeza chachu ya kufanikisha azma hiyo ya serikali.

Mhandisi Martin Madulu, akitoa hotuba yake
 Bw.Shirley Membi Swai, akitoa hotuba yake
 Afisa Uhusiano wa TANESCO, Bi. Salama akizungumza wakati wa utangulizi wa hafla hiyo
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Galagaza
 Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Galagaza, Bw. Shaaban Lagweni, akiwatambulisha walimu wenzake
 Sehemu ya majengo yaliyowekewa umeme na TANESCO kama msaada
 Wanafunzi wakipiga makofi kushangilia hotuba
 Mwalimu Echi Mkopi, akisoma risala
 Kwaya ya shule ikiburudisha
 Mgeni rasmina uongoziwa TANESCO wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananfunzi
  Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu, (kushoto), akimuonyesha Afisa Elimu (Taaluma), Bw.Shirley Membi Swai,moja ya vifaa vilivyofungwa na TANESCO katika mradi huo

Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO mkoa wa Pwani waliohudhuria hafla hiyo wakibadilishana mawazo

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.