ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 27, 2017

RAIS WA ANGOLA AAFIKI UCHAGUZI MKUU UFANYIKE AGOSTI 23


Rais Jose Eduardo dos Santos wa Angola amesaini dikrii inayoruhusu tarehe 23 Agosti mwaka huu kuwa siku ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini humo. 
Taarifa iliyotangazwa na idhaa ya serikali hapo jana imesema kuwa, uchaguzi mkuu utafanyika Agosti 23, ambapo Dos Santos anatazamiwa kuachia ngazi baada ya kuwa rais wa nchi hiyo kwa karibu miongo minne.

Hata hivyo taarifa hiyo imesisitiza kuwa, Dos Santos ambaye ameiongoza nchi hiyo ya Kiafrika yenye utajiri wa mafuta ghafi atasalia kuwa kinara wa chama tawala cha MPLA


Angola ni mzalishaji namba 2 wa mafuta ghafi Afrika, na uchumi mkubwa wa 3 barani humo
Uamuzi huu wa Dos Santos unajiri chini ya saa 48 baada ya Baraza la Uongozi la Rais wa Angola ambalo hutoa ushauri kuhusu maamuzi ya nchi kupendekeza tarehe 23 Agosti kuwa siku ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini.


Itakumbukwa kuwa, chama tawala nchini Angola cha MPLA mwezi Disemba mwaka jana kilimchagua Joao Lourenco mwenye umri wa miaka 63 kuwa mgombea wa kiti cha urais wa chama hicho.

Jose dos Santos aliye na umri wa miaka 74 ni kiongozi wa pili barani Afrika aliyesalia madarakani kwa muda mrefu zaidi, na mwezi Februari mwaka huu alisema kuwa hatagombea tena kiti cha urais katika uchaguzi ujao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.