ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 17, 2017

UN: SERIKALI YA SUDANI KUSINI YALAUMIWA KWA BAA LA; INGALI INANUNUA SILAHA.

SERIKALI ya Sudan Kusini ndiyo inayobeba lawama kubwa kwa baa la njaa linaloshuhudiwa katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo iliyoharibiwa na vita huku Rais wa nchi hiyo Salva Kiir akiendelea kutumia mamilioni ya dola zinazotokana na mauzo ya mafuta kuimarisha vikosi vyake vya ulinzi.
Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya siri ya Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la umoja huo na jopo la waangalizi wa vikwazo dhidi ya nchi hiyo.
Waangalizi hao wa UN wamesema, asilimia 97 ya mapato yanayotangazwa rasmi ya serikali ya Sudan Kusini yanatokana na mauzo ya mafuta huku asilimia isiyopungua 50 ya mapato hayo ikitumika kwa masuala ya usalama.
Jopo hilo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa limefafanua katika ripoti yake hiyo kuwa mapato yaliyotokana na mauzo ya mafuta yaliyouzwa kuanzia mwishoni mwa mwezi Machi hadi Oktoba 2016 yalikuwa karibu dola milioni 243, lakini licha ya ukubwa wa matatizo ya kisiasa na hali mbaya ya kibinadamu na kiuchumi iliyopo serikali ya Rais Kiir imeendelea kununua silaha kwa ajili ya jeshi lake la Ukombozi la Wananchi wa Sudan (SPLA), vikosi vya huduma za usalama wa taifa, vikosi vingine tanzu pamoja na wanamgambo watiifu kwa serikali hiyo.
Raia wa Sudan Kusini wanaokabiliwa na ukame.
Umoja wa Mataifa ulitangaza baadhi ya maeneo ya taifa hilo changa zaidi duniani kuwa yamekumbwa na baa la njaa ambapo watu wapatao milioni tano na nusu, ikiwa ni takriban nusu ya raia wote wa nchi hiyo wanakabiliwa na uhaba wa chakula.
Machafuko na vita vya ndani vilizuka nchini Sudan Kusini Desemba mwaka 2013 baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamu wake, Riek Machar kwamba amehusika na jaribio la kutaka kupindua serikali yake

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.