ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 10, 2017

MAHAKAMA YAMUONDOA MADARAKANI RAIS WA KOREA KUSINI.


MAHAKAMA ya Katiba ya Korea Kusini imeafiki uamuzi wa bunge wa kumuondoa madarakani rais wa taifa hilo Park Geun-hye. 
Katika uamuzi wa kihistoria leo Ijumaa, Mahakama hiyo ya Katiba, ikiwa na jopo la majaji wanane, imesema kuwa bi Park alikiuka sheria na kuvuruga demokrasia 
.
Park ambaye alikuwa mwanamke  wa kwanza kuwa rais wa Korea Kusini alihusishwa na kashfa ya ufisadi kutoka makampuni makubwa nchini kwa kushirikiana na rafiki yake mkubwa Choi Soon-Sil. Wawili hao wanakabiliwa na shtaka la kuchukua hongo kutoka mashirika makubwa 
.
Bi Park ameomba radhi kutokana na taathira za kashfa hiyo lakini amekanusha kukiuka sheria. Rais huyo alipokonywa mamlaka yake mwezi Desemba wakati bunge lilipomuuzulu lakini amekuwa akishikilia rasmi cheo chake akisubiri uamuzi wa Mahakama ya Katiba. Hivi sasa kuna uwezekano wa Park kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi 
.
Uamuzi huo ulipokelewa kwa shangwe katika maeneo mbali mbali yaliyo na wapinzani wa rais huyo 

Wananchi wa Korea Kusini wakifurahia kuuzuliwa Rais Park.
Hukumu hiyo imepokelewa kwa shangwe na wananchi ambao walitokeza mitaani kuunga mkono uamuzi wa mahakama. Wafuasi wake pia walionekana na kumekuwa na mzozano kati ya makundi hayo mawili. Uchaguzi wa urais sasa utafanyika katika kipindi cha siku 60 
.
Wakati huo huo Waziri wa Ulinzi Han Min-koo amelitaka jeshi la nchi hiyo kuwa katika hali ya tahadhari kwani nchi jirani ya Korea Kaskazini inaweza kutumia vibaya hali iliyojitokeza. Korea hizo mbili zimekuwa zikihasimiana kwa muda mrefu

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.