ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 24, 2017

MKUU WA KAMPUNI INAYOUNDA SIMU ZA BEI NAFUU INDIA AKAMATWA.

Bw Mohit Goel

MKURUGENZI wa kampuni ya Ringing Bells, kampuni ya India ambayo imedai kwamba inauza simu ya bei nafuu zaidi duniani, amekamatwa kwa madai ya ulaghai.

Mohit Goel alikamatwa baada ya kampuni moja inayosambaza simu hizo kwa wauzaji kudai kwamba ilikuwa haijapokea simu ambazo ilikuwa imelipia.

Simu hiyo ya Freedom 251, ambayo bei yake ni rupia 251 ($3.70; £3), ilianza kuuzwa Februari 2016.



Lakini ingawa wateja wengi walipokea simu walizoagiza, Ringing Bells imedaiwa kutotimiza maombi yote ya ununuzi wa simu hizo.

Kampuni ya Ayam Enterprises, imesema ililipa rupia 3m ($45,000; £35,800) baada ya Bw Goel kuishawishi ifanye biashara ya kusambaza simu hizo.

Lakini inadai ilipokea simu za thamani ya rupia 1.4m pekee na wafanyakazi wake walitishiwa walipodai "pesa tena na tena".

Msemaji wa polisi Rahul Srivastava amethibitishia BBC kwamba Bw Goel amekamatwa na atafikishwa kortini baadayek Ijumaa.

"Malalamiko mengine kadha sawa na hayo yamewasilishwa kutoka maeneo mengine ya jimbo. Tunataka kuyachunguza kwa kina," amesema.

"Ni muhimu kwetu kufichua sakata hizi kwa sababu watu wasio na hatia hupoteza pesa zao walizotolea jasho."

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.