ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 18, 2016

MAMA SAMIA AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI MWANZA.










Halmashauri zimetakiwa kuacha kuilalamikia  serikali kila mara kuhusu ufinyu wa bajeti na badala yake ziongeze bidii ktk ukusanyaji wa mapato, kuzuia upotevu wake na kubuni vyanzo vipya vya mapato.

Akizungumza na viongozi na watendaji mbali mbali wa chama na serikali katika majumuisho ya ziara yake ya siku nne mkoani Mwz Makamu wa Rais Mama SAMIA SULUHU HASSAN ameutaka mkoa wa Mwz kuhakikisha inamaliza tatizo la uhaba wa madawati.

Makam wa rais Mama SAMIA SULUHU HASSAN amehitimisha ziara yake mkoani Mwz kwa kutembelea machinjio ya jiji la MWZ ambayo yako katika ukarabati Mkubwa na kuweka jiwe la msingi kabla ya kutembelea na kuzindua Makao Makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Ilemela
Akihubia mamia ya wakaazi  wa Mandu nyakato jijini MWZ SAMIA ameitaka halmashauri ya jiji kutumia teknolojia ya kisasa huku akihadharisha  halmashauri ya jiji kuhusu usimamizi wa mradi huo.

Awali akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya halmashauuri hiyo Mkurugenzi wa Halmashari ya jiji la Mwz KIOMONI KIBAMBA aliitaka serikali kusaidia ununuzi wa vifaa vya kisasa.

Akifanya majumuisho ya ziara yake mkoani Mwz Makamu wa Rais Mama SAMIA SULUHU HASSAN amemtaka mkuu mkoa wa Mwz JOHN MONGELA kuhakikisha anamaliza tatizo la uhaba wa madawati ifikapo Januari mosi 2017.

Makamu wa rais Mama Samia Suluhu Hassan amehitimisha ziara yake ya siku nne  mkoani Mwz ambapo amekagua, amezindua na kuweka jiwe la msingi katika mabweni ya wasichana, kituo cha afya, mradi wa maji , machinjio ya kisasa, na kuhutubia mikutano ya hadhara.

ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGOBLOG.

MBUNGE ESTER BULAYA ASHINDA KESI YA UCHAGUZI DHIDI YA WASSIRA.

MARA: Mbunge Ester Bulaya (CHADEMA) ameshinda rufaa ya kupinga matokeo yake ya ushindi iliyokatwa na aliyekuwa mgombea wa Jimbo hilo na Waziri Mstaafu, Steven Wassira.

Kesi hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, lakini ilikuwa ikisikilizwa mjini Musoma, Mara.

Moja ya madai ya Wassira kupinga ushindi, alidai kuwa Bulaya hakujaza fomu ya kuonyesha gharama za kampeni kulingana na sheria ya uchaguzi.

MAJAMBAZI WAVAMIA DUKA MWANZA, WAMUU MAMA WA KIHINDI KWA RISASI.


WATU wanaosadikia kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za moto, wamevamia duka moja lililopo Mtaa wa Nkurumah (Katikati ya jiji la Mwanza) na kumuua kwa kumpiga risasi mama mmoja mwenye asili ya Kihindi kisha kupora kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana bado.

Duka hilo linauza bidhaa mchanyanyiko Mini Supermarket pia hutoa huduma za miamala ya kifedha kwa njia ya mitandao ya simu za mkononi..

VIDEO YA TUKIO.
Imeelezwa kuwa wakati majambazi hao wakiwa kwenye harakati hizo, aliingia mama mmoja mwenye asili ya Kihindi kwa ajili ya kununua dawa za kutuliza maumivu, panadol, ndipo majambazi hayo yalipomfyatulia risasi tatu na kusababisha afariki dunia papo hapo kisha yenyewe kutoweka kusipojulikana.
Tukio hili limetokea kwenye duka na matukio ya kuporwa kwa watoa huduma za miamala ya pesa kwa njia ya simu imekuwa sugu kwenye Jiji la Mwanza huku majambazi wakitekeleza uharifu huo kwa hutumia silaha za moto hivyo kuleta hofu na amani kutoweka miongoni mwa wakazi wa Mwanza.

.KAULI ZA MAKONDA ZAIBUA MASWALI 5, MAWAKILI WATOANA JASHO KESI YA LEMA, MREMA AWASHA MOTO SERIKALINI, MESSI KUZEEKA BARCELONA.


Kauli za Makonda zaibua maswali 5, Mawakili watoana jasho kesi ya Lema, Mrema awasha moto serikalini, Messi kuzeekea Barcelona. 


JPM amwaga wino sheria huduma za habari 2016, Wakuu wa mikoa 7 hatarini kutumbuliwa, Mwanamke afa akiombewa kwa nabii usiku. 


 Ofisa TRA kizimbani kwa rushwa ya Mil.15, Mbunge Lema akamatwa tena, Uhakiki wav yeti waacha kilio mbeya. 

.TAASISI YA VIJANA YA TYVA NA IRI ZATOA MAFUNZO KWA VIJANA KUHUSU MCHAKATO WA MABADILIKO YA KATIBA


Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akitoa elimu kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na historia ya mchakato huo kwa vijana wa wilaya ya Chamwino mkoani  Dodoma.
Afisa wa IRI, Tony Alfred akizungumza jambo wakakati wa mafunzo ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba kwa vijana wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Makamu mwenyekiti wa TYVA, Kamala Dickson akizungumza jambo kwenye mkutano huo
Baadhi ya Vijana wa wilaya ya Chamwino wakiwa kwenye mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba.

Katibu Mtendaji wa TYVA Saddam Khalfan akitoa ufafanuzi kuhusu shirika hilo wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya Vijana wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akitoa elimu kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na changamoto zake kwa vijana wa wilaya ya Tanga Mjini mkoani  Tanga.

Mmoja wa washiriki akichangia mada
Kijana mwenye ulemavu wa ngozi akisoma katiba ya Tanzania kwa makini sana wakati wa  mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba yaliyofanyika Mjini Tanga.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo yaliyofanyika Tanga wakifuatilia mada

Na Mwandishi Wetu
Asasi Ya Vijana, Tanzania Youth Vision Association kwa Kushirikiana Na International Republican Institute zimetoa mafunzo ya kuboresha Uwezo wa Vijana kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini katika Mikoa mitatu ilijumuisha Wilaya Nne, ikiwemo Kinondoni, Dodoma Mjini, Chamwino Na Tanga Mjini.

Mafunzo hayo yameweza kufikia vijana 500 kwa njia ya Warsha na Vijana aa wananchi zaidi ya 100,000 kupitia mitandao ya kijamii.

Lengo kuu la Mafunzo hayo ni kuongeza uelewa na ushiriki wa Vijana katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Katibu Mtendaji wa TYVA ndugu Saddam Khalfan alisema, TYVA inaamini Katiba ni Sheria mama na mwongozo ambao una uhusiano wa moja kwa moja na maisha yetu ya kila siku.

Alibainisha watu wengi wamekua wakisoma au kuisikia Katiba, na wengine wakidhani Katiba ni maalumu kwa ajili ya wanasheria au wasomi tu. Kuna uhusiano mkubwa kati ya Katiba bora ya Nchi, Demokrasia na Maendeleo ya Jamii.

Mwanaharakati Na Mtetezi wa HAKI za Binadamu ndugu Deus Kibamba alipata kuwaelezea washiriki wa mafunzo hayo historia ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba, Ushiriki wa wananchi katika mchakato wa Katiba, hatua muhimu katika Mchakato wa utengenezaji Katiba, Mambo ya Msingi yaliyomo katika Katiba inayopendekezwa na Mambo muhimu kuelekea kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa.

Alidokeza pia, katika mchakato wa Katiba, hasa katika hatua ya Bunge la Katiba ulikosa maridhiano ya Kitaifa. kuna haja ya kuwepo mkutano wa kitaifa utajaowaleta wadau na jopo la wataalamu mbalimbali kwa ajili ya kunyambua yale mambo yanayoendelea kuleta ukakasi linapaswa kufanyika.

Ndugu Dickson Kamala ambaye ni Mtetezi wa HAKI za vijana na Makamu Mwenyekiti Wa TYVA aliwasilisha mada ya umuhimu wa Vijana kushiriki na kushirikiana katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba ili kupata Katiba itayojali maslahi yao na ya Taifa kwa ujumla.

Afisa kutoka IRI, Tony Alfred aliwatarifu Vijana washiriki kusoma kuhusu Katiba na wanaweza kupata habari na taarifa zaidi kuhusu Katiba kwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi kwa kutuma Neno "Katiba yetu" Kwenda 0684996494.

Thursday, November 17, 2016

MAMA SAMIA ATETA NA WANA UKEREWE KUEPUKA UJENZI WA NYUMBA ZISIZO NA HUDUMA ZA VYOO.

Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu akisalimiana na wananchi mara baada ya kuingia wilayani Ukerewe.
PICHA NA ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO BLOG.
Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu akipata picha na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Gerson Rwenge mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji na usafi wa mazingira wa Ziwa Victoria Mjini Nansio Ukerewe.


Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Mkoa wa Mwanza Injinia Athony Sanga akitoa ufafanuzi wa mradi wa maji wilaya ya Ukerewe mbele ya Makamu wa Rais Serikali awamu ya 5.





Ukerewe. Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan  amewataka wakazi wa mji wa Nansio  katika wilaya ya Ukerewe mkoani  hapa kuepuka ujenzi wa nyumba ambazo hazina  huduma za vyoo vya ndani.


Lengo la agizo hilo ni pamoja na kupunguza kiwango cha uchafuzi wa maji ya ziwa,kutokana na tabia ya baadhi ya wananchi kuchimba vyoo vya shimo ambavyo  alisema mara nyingi miundombinu yake siyo rafiki kwa usafi wa mazingira,hasa kandokando ya ziwa.

MamaSamia alitoa agizo hilo wakati akihutubia  mamia ya wakazi wa mji huo  kwenye  hafla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa majiisafi na usafi wa mazingira ziwa Victoria awamu ya pili ambao umetekelezwa kwa gharama ya sh10.9  bilioni.

Makamu huyo wa Rais ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mradi huo ambao umefadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika,kupitia nchi wanachama wsa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Licha ya kutumia muda mwingi wa hotuba yake kujibu mabango ya wananchi,Makamu wa Rais pia aliiagiza Wizara ya maji na umwagiliaji kushirikiana na uongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Jijini Mwanza kushirkiana na wakazi wa mji huo kulinda miundombinu ya mradi.

Vilevile,Makamu wa Rais ambaye alikuwa amefuatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Emmanuel Kalobelo pamoja na mwakilishia wa Kamisheni ya Bonde la ziwa Victoria, Dk Ally Matano aliwataka wakazi wa mji wa Nansio na vijiji jirani kutambua kwamba mradi huo ni mali yao,hivyo wana wajibu wa kulinda na kuutunza.

Akisoma taarifa mbele ya Makamu sa Rais,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Emmanuel Kalobelo alisema mradi utawanufaisha wakazi zaidi ya 80,000 wa mji wa Nansio pamoja na vijiji vya Nantare, Kakerege, Hamkoko, Bukongo, Nkilizya, Kagera, Nakatunguru, Malegea na Bulamba.

Alisema mradi huo ni miongoni mwa miradi mingine miwili inayotekelezwa kitaifa  katika miji ya Sengerema na Geita mkoani.

Kwa upande wake,mwakilishi wa Kamisheni ya Bonde la ziwa Victoria,Dk Matano aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kukamilisha mradi huo kwa wakati, na kwa kiwango cha hali ya juu ikilinganishwa na miradi mingine 12 inayotekelezwa katika nchi nyingine tano ambazo ni wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Makamu wa Rais juzi alihitimisha ziara ya siku tatu mkoani Mwanza ambapo alitembelea  na kuweka mawe ya misingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Sengerema, Misungwi, Kwimba na Magu.

MARIE STOPES TANZANIA KUADHIMISHA SIKU YA KUFUNGA UZAZI KWA WANAUME KWA KUTOA HUDUMA HIYO BURE KWENYE MIKOA MITANO BURE NCHINI.

Marie Stopes Tanzania (MST) inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuhamasisha Wanaume Kufunga Uzazi yaani World Vasectomy Day, ili kusaidia wanaume na familia zao kuhamasika kufanya maamuzi sahihi. 

Kufunga uzazi kwa mwanaume yaani Vasectomy, ni njia rahisi, salama na yenye gharama nafuu, lakini imani potofu, vikwazo vya kimila na desturi vimesababisha matumizi ya njia hii ya uzazi wa mpango kuwa chini sana huku baadhi ya wanaume wakiihusisha na kupungua kwa nguvu na hamu ya kufanya mapenzi, au hata kuifananisha na kuhasiwa. 


Utafiti uliyofanyika hivi karibuni na Marie Stopes inaonyesha kuwa baadhi ya wanaume wa kitanzania hawaafiki kufunga uzazi kwa sababu tu ya kukosa elimu stahiki ama kwa uwoga wa njia hii ya uzazi wa mpango, na pengine labda maudhi yatokanayo (kwani wanaume wengine hufikiri kufunga uzazi ni jambo gumu na hatari) au hata kwa kupingwa na wenza wao. 

Pia ilibainika kwamba kuna baadhi ya wanaume wanaogopa mtazamo hasi kutoka kwa jamii inayowazunguka, ikiwa ni pamoja na kutaniwa, kuchekwa, kuonekana kama wamehasiwa, na hawana thamani au nguvu. Hizi zote ni mila potofu.

Ili kuondoa imani hizi potofu na kuongeza uelewa juu ya faida nyingi za njia hii ya uzazi wa mpango, MST imepanga kutoa elimu na huduma za kufunga uzazi bure kwa wanaume katika mikoa mitano ya Tanzania, kama sehemu ya maadhimisho haya ya kimataifa yenye lengo la kuhamasisha wanaume kusimama imara kwa ajili ya watoto, wake zao, pamoja na maisha yao ya baadaye. Huduma hii ya bure itatolewa na timu za mkoba za MST zinazofanya kazi Zanzibar, Kagera, Mwanza na Makambako, pamoja na hospitali ya Mwenge iliyopo jijini Dar es Salaam.

“Vasectomy siyo tu ni moja ya njia bora na uhakika zaidi za uzazi wa mpango, na haisababishi tatizo lolote linalohusiana na nguvu ama hamu ya tendo la ndoa, au nguvu ya mwili wa mtu. Mbinu mpya ya upasuaji bila kutumia wembe na kushonwa iliyobuniwa Marie Stopes International (MSI) hutumia chini ya dakika 15 na ni ya uhakika kwa zaidi ya asilimia 99. Mara nyingi suala la kupanga uzazi limekuwa likionekana kama ni jukumu la wanawake pekee. 


Hata hivyo, wanaume wengi wanhitaji fursa ya kupanga idadi ya watoto wanaowataka, na wanawake wengi wanahitaji washirikiane na wenza wao katika jukumu la kupanga uzazi wa mpango. Marie Stopes Tanzania inapenda kuwahamasisha wanaume ambao wametumia njia hii salama ya kufunga uzazi kuwa mabalozi na kueneza habari wa njia hii ya uzazi wa mpango yenye uhakika na salama pamoja na jinsi ambavyo wamepata amani moyoni mwao,” anasema Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes Tanzania, Bw. Anil Tambay.

Tunapoadhimisha siku ya Vasectomy duniani, MST inaahidi kuwa katika kipindi cha kuanzia sasa hadi 2020, itaongeza jitihada zake katika maeneo makuu yafuatayo:

• Kuzifikia jamii za pembezoni zaidi na vijijini kwenye mahitaji ya huduma za uzazi wa mpango kwa wanawake na wanaume hasa wale wanaoishi kwa kipato cha chini ya Dola 1.25 (Shilingi 2,730).

• Kufanya kazi na mamlaka za serikali katika ngazi ya taifa, mkoa hadi wilaya ili kuboresha huduma. Zaidi ya watoa huduma 600 wa sekta ya umma wamepatiwa mafunzo katika mwaka 2015 na wanaendelea kutoa huduma. Watoa huduma wengine zaidi wanatarajiwa kupewa mafunzo ikiwa ni sehemu ya mchango wetu katika kujengea uwezo sekta ya umma.

Takwimu za mfumo wa taarifa za afya za wilaya nchini (DHIS 2) kwa miaka mitano iliyopita, zinaonyesha kuwepo kwa ongezeko la wanaume wanaofanyiwa njia ya kufunga uzazi, kutoka wanaume wawili (2) mwaka 2011 hadi 905 mwaka 2015, na 1079 kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu. Takwimu hizi pia zinaonyesha kuwa mkoa wa Kigoma umekuwa ukifanya vizuri kwa kuwa na mwitikio mkubwa wa wanaume kufunga uzazi, ukifuatiwa na mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma na Kagera.

Wakati huo huo, takwimu za mfumo wa taarifa za afya za Marie Stopes Tanzania pia zinaonyesha kuwepo kwa ongezeko la wanaume wanaokubali kufunga uzazi ambapo jumla ya wanaume 598 wamepatiwa huduma hiyo kati ya mwaka 2012 na October 2016, katika Zahanati na huduma za mkoba za Marie Stopes katika maeneo mbalimbali hapa nchini.za kijinsia, afya ya uzazi na uzazi wa mpango katika maeneo ya mijini.

MAENDELEO YA DIMBA LAKO LA NYAMAGANA.

VIDEO.
Usimikaji nyasi uwanja wa Nyamagana Mwanza wafikia awamu ya uwekaji mchanga mweusi, hii ni awamu ya mwisho kabisa kuelekea kukamilika lakini changamoto iliyosalia ni ile ile = Majukwaa.




Tutaendelea kukupatia taswira za uwanja wa Nyamagana hadi pale utakapo kamilika.

SAKATA LA WADIWA SUGU MIKOPO YA ELIMU YA JUU NA RUNGU LILILOTOLEWA KUWAADHIBU.

Tazama mazungumzo kuhusu kuhusu mikopo ya elimu ya juu na hatma ya wadaiwa wanaodaiwa na bodi ya mkopo.

MAKALA YA HIFADHI YA TAIFA YA KATAVI

Mmoja wa Simba akiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi
Baadhi ya Mamba wakiwa wamepumzika katika hifadhi ya Taifa ya Katavi
Hawa ni Punda milia wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi
Kama kibao kinavyo onekana hili ni Eneo la Tambiko ambapo watu huja kusali na kutoa sadaka mbalimbali
Simba akiwa na mzoga wa Kiboko
Twiga akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Katavi


  Na  Walter  Mguluchuma wa Katavi yetu Blog
   
  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi  inapatikana  kusini  Magharibi  mwa  Tanzania   karibu na  Ziwa  Tanganyika   katika  Wilaya za  Mpanda  ,Tanganyika  na  Mlele    Mkoa wa  Katavi  inapatikana  katika  latitude 6.63.7.34 kusini na   na  longitude  3.74.31.84  Mashariki.

  Hifadhi  hii  ilitangazwa  kuwa  Hifadhi ya  Taifa   mwaka 1974 ikiwa  na  ukubwa  wa  kilometa za   mraba  2253 iliongezwa  ukubwa  mwaka  1996 na kufikia  ukubwa  wa kilometa za  mraba  4471 na kuifanya kuwa   Hifadhi  ya tatu  kwa ukubwa  Tanzania  baada ya Ruaha na   Serengeti .

 Ilipata  jina   lake  kutokana  na  mzimu  wa  kabila la Wabende  aliyejulikana kwa  jina  la  Katabi  ambapo mpaka  leo watu  mbalimbali  wamekuwa wakifika ndani ya  Hifadhi ya  Katavi na kwenda  kwenye  mti  ulioko  kwenye  Ziwa  Katavi  wakiamini kuwa  mzimu  Katabi alikuwa  akiishi  hapo  zamani   kabla ya kuwepo  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi .

Jina la  Hifadhi hii  lilijulikana   kama   Katabi  kutokana  na imani  ya  jamii   hizo kwa  mzimu  Katabi  inaaminika  kwamba  mzimu  Katabi  una uwezo  wa  kufanya miujiza  ikiwemo  kufanya mvua  inyeshe , kuzuia  magonjwa  ya mlipuko  kama vile ndui na kutatua shida za watu mbalimbali .
Hifadhi hii  inafikika  mwaka mzima  kwa kupitia  Mikoa ya  Dares,salaam,Mwanza , Kigoma   Arusha     hadi  Mpanda  kupitia  Tabora kwa kutumia  usafiri wa  ndege  za kukodi    Chartered planes  au kwa njia ya  barabara kwa kupitia  Mbeya   na  Sumbawanga pia kwa kutumia usafiri wa  Treni kutokea  Tabora .

Katavi   'National  Park'  inawanyama wengi na  adimu  na wakubwa kuliko  wanyama  wanaopatikana  kwenye  Hifadhi  nyingine  hapa   Nchini  kutoka  na  hari ya uoto wa  asili  uliopo  kwenye   Hifadhi hii ambayo kwa sasa imeanza kupata watalii tofauti na  hapo  awali .

Mbali ya kuwepo  kwa  wanyama  wengi   madhari yake ni  pana  kuanzia  uwanda  tambarare wa  nyasi  katika  mkondo  wa  bonde  la ufa   hadi  kwenye miteremko  mikali  ambayo ni  matawi  mawili  sambamba na bonde la ufa la    Mashariki   maarufu  kama  bonde la ufa la   Rukwa .
Uoto uliopo unavutia  unavutia sana kuanzia  kuanzia  Misitu  iliyofunga  mpaka misitu ya wazi  ,vichaka  uwanda wa  nyasi  maziwa  ya msimu ya   Chada  na  Katavi  mabwawa na uoto  kando ya mito .

 Wakati wa kipindi cha  mvua  kuna   aina  nyingi za  maua   aina ya  'species' mbalimbali  za miti na majani  aina za  'species' 226 za miti zimeisha tambuliwa  zikiwemo  aina  tatu   zenye   mvuto  wa kisayansi .

  Uhai  wa  Hifadhi  ya  Katavi  unategemea  mto  Katuma   ambao  humwaga  maji  yake   ziwa   Katavi  upande wa  kaskazini ,Ziwa  Chada  na  mbuga  yenye  eneo la  kilometa za  mraba  425 ambayo  hutuamisha   maji  Floodplain katikati ya  Hifadhi  ziwa   Chada  hupokea  pia  maji  kutoka  mto  Kapapa   ambao  mkondo wake  hutokea   Kaskazini  mwa  Hifadhi ya  Taifa   Katavi .

  Kuna  aina  mbalimbali  za   wanyama pori ,idadi  kubwa  ya vipepeo  na  ndege  wa   aina   mbalimbali  katika  Hifadhi ya   Katavi  ni kivutio  vikubwa  kwa wageni   idadi ya   watalii  na   shughuli za   maendeleo    ndani ya   Hifadhi   bado ni   ndogo   hivyo  kufanya  mazingira  kuwa  asilia  zaidi .

Baadhi ya  wanyama  wanaopatikana  kwenye   Hifadhi ya    Katavi  ni  makundi  makubwa ya   Tembo ,  Nyati,  Simba ,  Pundamilia ,  Mbwa  mwitu ,  kongoni  Swala  pala ,   Nyemela  na  wanyama  wengineo .

Pia  kwenye  eneo la  mto   Stalike  na   Iku  utakuta  kuna  makundi makubwa  sana ya  viboko na  mamba  ambapo kumekuwa na  mapigano  ya  mara kwa  mara  na  kufanya  eneo hilo kuwa  kivutio kikubwa kwa watalii.

Upande wa   Hotel  hifadhi hiyo  inayo hotel nzuri za kufikia wagani ndani ya  Hifadhi  iiingawa  bado  ni  chache  pia   hotel nyingine   zinapatikana   katika   Kijiji cha  Stalike  ambacho kipo  jirani na  Hifadhi  na  pia   katika   Mji wa  Mpanda        makao  makuu ya  Mkoa wa Katavi  uliopo  umbali wa kilometa   40 kutoka   Hifadhi ya  Katavi .

 Hivi  karibuni   kaimu   Mkuu wa  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi    Elias   Manase  aliwaambia   wandishi wa  Habari wa  vyombo  mbalimbali wa   Mkoa wa  Katavi  kwamba  Hifadhi  hiyo  inakabiliwa  na   changamoto  mbalimbali .

Baadhi ya   changamoto hizo ni   ujangili   wa  wanyama  hasa  Tembo   ambao  unasababishwa na kuwepo kwa  kambi za wakimbizi   za    Mishamo na  Katumba  ambazo wanaishi  Raia wa  Burundi na  Kongo .

  Ilidai   kuwa  watu wanao ishi kwenye  makazi  hayo wamekuwa  wakiingiza   silaha za  kivita  na kuziingiza  nchini kisha wamekuwa wakifanya ujangili wa kuuwa  Tembo  na kisha  wanachukua  meno ya  Tembo na kuyasafirisha  kwenye  soko  la  nchi  jirani.

Changamoto  nyinginei ni  uhaba wa miundo  mbinu  ndani ya   Hifadhi kwani  bado  haiku  mizuri  sana  ingawa   barabara  zake zinapitika  karibu  mwaka  mzima .

Manase  alitowa  wito kwa  watanzania  kujenga utamaduni wa kutembelea  Hifadhi za Taifa kwani   gharama ya kutembelea  Hifadhi  za  Taifa ni  ndogo kuliko  gharama ya  mtu  anayoitumia  kwenye   Bar  kunywa  pombe . 

Askari wa   Hifadhi   ya  Katavi  Joseph  Mhina aliielezea  Hifadhi ya  Katavi  kuwa     ni   hifadhi  ambayo  ipo  tofauti     kabisa  na  Hifadhi  nyingine kwani  watalii wanaotembelea   Hifadhi  hiyo  huwa  wanawaona wanyama kiurahisi  kabisa kwani  watalii  huwa ni wachache hivyo   huwa   hakuna kugombania kuwaona  wanyama  kama  Hifadhi  nyingine .

Imeandaliwa na Blogs za Mikoa kupitia Katavi yetu Blog

WAJASIRIAMALI KIGOMA WANUFAIKA NA MAFUNZO YA TPSF

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Yuda Thadeus Mboya (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya wajasiriamali iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation),(Kulia) Meneja wa SIDO mkoa Kigoma, Gervas Ntahamba na (wa pili kushoto) Mwenyekiti wa chama cha Wafanyabiashara na wenye viwanda mkoa Kigoma (TCCIA), Ramadhani Gange.
 Mwenyekiti wa chama cha Wafanyabiashara na wenye viwanda mkoa Kigoma (TCCIA), Ramadhani Gange (wa pili kushoto aliyesimama) akitoa neno la shukrani kwa mgeni Rasmi wakati wa ufunguzi wa semina kwa wajasiliamali iliyotayarishwa na taasisi ya sekta binafasi Tanzania (TPSF)
Baadhi ya wajasiliamali wa Manispaa ya  Kigoma Ujiji wakijadiliana mada mbalimbali zilizotolewa na wawezeshaji  wakati wa semina ya wajasiriamali iliyoandaliwa na taasisi ya sekta  binafasi Tanzania (TPSF).
Baadhi ya wajasiliamali wa Manispaa ya  Kigoma Ujiji wakijadiliana mada mbalimbali zilizotolewa na wawezeshaji  wakati wa semina ya wajasiriamali iliyoandaliwa na taasisi ya sekta  binafasi Tanzania (TPSF).

---
Wajasiriamali waliopo mkoani Kigoma wametakiwa kutumia raslimali mbalimbali zilizopo mkoani humo na fursa zinazojitokeza kwa sasa kuibua miradi ya biashara na kuendesha biashara yao kitaalamu wakiwa na malengo ya kujikwamua kutoka katika hali ya umaskini.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji , Yuda Thadeus Mboya, wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalumu ya mbinu za kuendeleza wajasiriamali yaliyoandaliwa na taasisi ya Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) na kufanyika katika ukumbi wa St.Martha mjini Kigoma.

Alisema serikali imefungua milango ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kwa kutumia fursa zilizopo hivyo aliwataka kushiriki mafunzo mbalimbali ya mbinu za biashara na kuibua miradi ya biashara na kuwa na utayari wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika biashara kwa kipindi hiki mojawapo ikiwa ni ushindani mkubwa na kufanya biashara kwa kufuata njia halali zinazotakiwa ikiwemo kulipa kodi za serikali kwa mujibu wa sheria.

“Hivi sasa biashara zinafanyika katika mazingira ya ushindani na wateja wanahitaji bidhaa zenye ubora hivyo haitakiwi ubabaishaji wa aina yoyote kwa mfanyabiashara anayetaka mafanikio”.Alisema Mboya.

Aliipongeza taasisi ya TPSF kwa kuendesha miradi ya mafunzo kwa wajasiariamali sehemu mbalimbali nchini “Nawapongeza kwa kuwafikishia mafunzo wajasiriamali wa ngazi za chini katika ngazi ya mikoa na wilaya kwa kuwa wafanyabiashara wakipata mafunzo kama haya kwa vyovyote wataweza kupata mafanikio katika shughuli zao”.Alisema .

Kwa upande wake Meneja Mradi wa Mafunzo kutoka taasisi ya TPSF,Celestine Mkama alisema kuwa taasisi hiyo inaendesha mradi wa kuwapatia mafunzo wajasiriamali kuhusiana na mbinu mbalimbali za kufanya biashara kwa lengo la kupata mafanikio.

“Mafunzo haya yamelenga kuwapatia maarifa wafanyabiashara wadogo ili yawajengee uwezo wa kukabiliana na changamoto zilizopo katika biashara “Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa wafanyabiashara wengi wadogo wamekuwa wakikosa mbinu za kufanya biashara kutokana na kukosa elimu ya biashara ndio maana tumeona tuwasaidie katika eneo hili la kuwajengea uwezo kupitia kuwapatia elimu ya ujasiriamali”.Alisema Bw.Mkama.

Mkama alisema baadhi ya masuala yanayofundishwa kupitia mafunzo haya ni utunzaji wa mahesabu ya biashara,nidhamu katika matumizi ya fedha,utunzaji wa kumbukumbu za biashara na jinsi ya kupanga miradi.

Alisema mafunzo haya tayari yameishafanyika katika mikoa mbalimbali na kuwafikia wajasiriamali wengi na tathmini ya awali inaonyesha kuwa waliopata mafunzo haya wameanza kuendesha biashara zao kwa ufanisi na kutoa mchango katika pato la taifa kupitia kulipa kodi.