ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 15, 2016

ANTHONY MTAKA:- SASA SIMIYU NI YA VIWANDA.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka aeleza namna mkoa huo ulivyojipanga ili kuhakikisha kila bidhaa ya mazao ina kuwa na viwanda vidogo vidogo.

KONGAMANO LA KUMUENZI MWALIMU J.K NYERERE LAFANYIKA WILAYANI IKUNGI

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwa amembeba mmoja ya mwanafunzi wa shule ya Msingi Ikungi mchanganyiko
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikabidhi mahitaji kwa wanafunzi walemavu mara baada ya kuwasili shule ya msingi Ikungi mchanganyiko
 Baadhiya washiriki wa Kongamano wakisikiliza kwa makini mada zikiwasilishwa kwenye mdahalo

“Oktoba 14 KWANGU INA MAANA ZAIDI YA MOJA" - Dk. Kigwangalla

KIGWANGALLA
Sheila akilishwa keki na mdogo wake.
dsc_1428
Sheila akimlisha keki mama yake.
Dk.KigwangallaSheila akimlisha keki Baba yake mzazi, Dk. Hamisi Kigwangalla
dsc_1413Sheila akimlisha mdogo wake keki
dsc_1388dsc_1421Sheila akiwalisha watoto wenzake keki
dsc_1424Dk.Kigwangalla akimlisha mwanae Sheila keki yake hiyo
dsc_1471Sheila akimlisha keki mdogo wake
dsc_1433Sheila akimlisha keki bibi yake
dsc_1455Sheila akiwalisha keki watoto wenzake
dsc_1584Watoto wakifurahia shughuli hiyo na kupata chakula cha pamoja
dsc_1590dsc_1672Dk.Kigwangalla akimpa zawadi maalum mtoto wake kama zawadi ya kutimiza miaka hiyo Nane
dsc_1712Shangazi wa Sheila akimpa zawadi ‘Anty’ yake 
Na Dkt. Hamisi Kigwangalla.

Tarehe ya leo, miaka minane iliyopita alizaliwa binti yangu Sheila. Ni Mtoto wangu wa kwanza. Unaweza kukadiria mshawasha na mcheche niliokuwa nao siku hiyo. 

Kila mwaka tunapomkumbuka baba wa Taifa letu, basi mimi hukumbuka kuwa ni siku ya kuzaliwa mwanangu pia. Mwaka juzi niliandika makala. Nimeitafuta siioni. Nitajaribu hapa leo kurejea, Kwa ufupi, maudhui ya makala ile. Wakati naandika makala ile nilikuwa nimetoka kutangaza nia ya kuchukua fomu ya kuwania Urais. Nilitafakari sana mustakabali wa maisha yangu. Nilipotoka na nilipofikia. Nikahusianisha Tanzania ile na Tanzania ya akina Sheila. Mustakabali umebadilika kabisa! 

Mwanangu Sheila amezaliwa kwenye zama za utandawazi, elimu yake, Kwa mimi mzazi mwenye kuelewa dunia ya sasa na ushindani atakaopaswa kuukabili, naliona jukumu langu la kumuandaa vema. 

Mimi, hadithi yangu, ni tofauti sana na hadithi ya mwanangu. Siyo lazima na yeye apitie madhila yangu. Yeye ninamuandaa. Namuandaa ajue wajibu wake wa kujiandaa kupambana na ushindani. Mimi niliandaliwa na nchi. Hii ni tofauti kubwa ya kwanza. 

Mimi na Ndg. Bashe tulipoingia shule mwaka 1984, pale Shule ya Msingi Kitongo, na kufundishwa kusoma na kuandika na Mwl. Malunde, tulipelekwa kutimiza majukumu ya wazazi kama ambavyo Serikali ilikuwa ikielekeza. Watoto tulikuwa ni hazina nyeti ya Taifa, mali ya jamii nzima. Leo kila mtu na wanaye. Kila mtu na wa kwao. 

Darasa letu lilikuwa na watoto wa kila mtu, bila tofauti ya kipato ama cheo. Tulisoma na watoto wa Mkuu wa Wilaya, Watoto wa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Wilaya, Bwana Tawala, Meneja wa Benki, matajiri wa kiarabu na kihindi nk. Shule zilikuwa ndiyo hizo tu. Sote tulipata fursa sawa na kwa maana hiyo tulikuwa na mustakabali sawa wa maisha yetu ya baadaye. 

Mimi nilipelekwa shule na mama yangu mzazi, bi Bagaile Lumola. Hii ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya kipekee kwenye maisha yangu. Nilifurahia sana shule, japokuwa mara nyingi nilienda shule bila kula, na sare zangu za wasiwasi, miguu peku, lakini sikuwahi kuona tofauti yoyote ile kati yangu na watoto wa Mkuu wa Wilaya. Hata wao mara nyingine walikuja shuleni bila viatu. Sote tuliona sawa tu, kwamba ni 'kawaida' tu. Pengine hayo yalikuwa ndiyo maisha ya nyakati zile. 

Utandawazi umeibadilisha kabisa jamii yetu. Udugu wetu mpana unaanza kupotea. Zamani tatizo la mmoja wetu mtaani lilikuwa letu sote. Furaha yake ilikuwa yetu sote. Nakumbuka jirani na nyumbani kwa bibi yangu Mama Bagaile, aliyenilea, kulikuwa na familia ya Mzee mmoja mkatoliki mwenye kushika dini yake sana, Mzee Kidola, kila akitaka kuchinja, iwe kuku iwe mbuzi, atanoa kisu chake vizuri, atamfuata babu yangu, ambaye alikuwa muislamu. Na kila akichinja sisi ni lazima tuchekelee maana lazima agawe nyama kwa babu yangu. Hivyo hivyo, siku za Eid, ni lazima tuwapelekee sufuria la pilau na nyama. 

Mzee Kidola alipenda kufuturu nasi uji wa pilipili manga na chai ya viungo, enzi hizo tukifuturu nje ya nyumba barazani, na wapita njia wakikaribishwa! 

Upendo na mshkamano uko hatarini kupotea. Leo Ndg. Saidi anatolewa macho mchana kweupe, hadharani, anafanyiwa unyama watu wanatazama tu. Udugu wetu, upendo na mshkamano wetu umeenda wapi? 

Hii ni tofauti ya pili ya maisha ya makuzi yangu na makuzi ya mwanangu Sheila. 

Tanzania yangu mimi ni Tanzania iliyojengwa na baba wa Taifa, Mwl. Nyerere. Ni Tanzania iliyotoa fursa kwa mtoto aliyelelewa na mama ntilie kuota ndoto ya kuwa Daktari na kuitimiza. Ni Tanzania iliyotoa fursa sawa kwa mtoto wa  mama ntilie na mtoto wa Mkuu wa Wilaya kuwa Mbunge. 

Tanzania ya Sheila, mwanangu, ni Tanzania ninayowajibika kuijenga. Kila kukicha natafakari, Je ni Taifa gani ninaloandaa kwa ajili ya mwanangu na wajukuu zangu? 

Kila nikiangalia nyuma ninakotoka. Najiuliza nimefikaje hapa. Ni muujiza. Nikitazama tulipo na nikitafakari tunapokwenda, nabaki na maswali magumu sana kichwani! 

Hivi, Tanzania ninayoijenga mimi leo, itatoa fursa Sawa Kwa Sheila, mtoto wa Mbunge, na kwa mtoto mwingine wa mama ntilie kama mimi? 

Ninapokukumbuka baba wa Taifa moyo wangu unavuja damu kwa uchungu; machozi ya furaha na upendo yananitoka, ndoto zako zimegusa maisha yangu. Naahidi kufanya kila niwezalo kuishi falsafa yako, siyo kwa kutembea na 'kifimbo' tu na kuvaa suti za Mao, bali kwa kutoa uongozi madhubuti wakati wa kutunga sera ili kulinda misingi ya taifa tulilorithi kutoka kwa babu zetu. 

Viongozi wa zama zetu tuna kazi ya ziada ya kufanya. Ni lazima tuweke ubunifu kwenye malengo ya mbali ya Taifa letu, sera zetu na mikakati yetu. Zama zimebadilika, utandawazi umetamalaki, lakini kuna mambo ya msingi tuna wajibu wa kuyalinda kwa nguvu zetu zote kwa kuwa ni tunu za Taifa letu. 

WAANDISHI WA MWANANCHI WAPATA AJALI.

Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Mkoani Mwanza, Peter Saramba na Mpigapicha Michael Jamson wamepata ajali eneo la Kimbu B, Wilaya ya Bariadi wakiwa wanatoka Simiyu kwenye sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julias Kambarage Nyerere zilizoambatana na kuzima mwenge.

Muda mfupi baada ya ajali Saramba alisema  watu wawili wamefariki papohapo katika ajali hiyo wakati yeye akiwa amelazwa katika hospitali ya Mkula Wilaya ya Busega akipatiwa matibabu kufuatia majeraha aliyoyapata..

“Ajali ilikuwa mbaya sana,ila namshukuru Mungu nipo mzima ingawa nimepata majeraha madogomadogo, lakini tumeletwa hapa Busega katika hospitali ya Kikula kwa ajili ya kupatiwa matibabu, na tayari madaktari wanatuhudumia hapa” alisema Saramba.

Friday, October 14, 2016

MBUNGE WA SINGIDA MJINI AMUENZI MWALIMU NYERERE KWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akimkabidhi mganga mkuu wa zahanati ya Mtamaa Bw Godson Charles Swai kifaa maalumu kwa ajili ya kipimo cha ugonjwa wa Malaria
Mashine ya Kupima Maralia (Binocular Microscope) Mega 7 ikiwa imefunguliwa kwenye Boksi maalumu ili wananchi waione kwa karibu
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mtamaa kupitia mkutano wa hadhara

MAMBO YA ZIADA AMBAYO HUKUWAHI KUDHANI JUU YA MWL. JULIUS KAMBARAGE NYERERE.


Hivi unajua pale Butiama chakula cha mwisho alichovuna Mwl. Jk. Nyerere enzi za uhai wake bado kipo hadi sasa (miaka 17) na kimebaki kama kumbukumbu..............!? 


Jeh hivi unajua pamoja na baba wa Taifa kumiliki gari hakuwahi wala hakuthubutu kujifunza kuendesha gari....................................................................................................!?


Basi kijana aliyekuwa chipukizi wa mwisho kumvisha scarf kwenye mapokezi wilayani Bunda Enzi za utawala wake baada ya kung'atuka na kubakia kama Mwenyekiti wa CCM kijana Lawrenti Alphonce maarufu Jicho' atakwenda kusimulia mengi ikiwa ni pamoja na story ya....................................................................................


@prince_arn @mansourjumanne @gsengo #Mchepuko na mikito mikali ya djscopion #NyerereDAyDriveMIXspecial


BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

ZITTO: NYERERE WANGU ALIKUWA HIVI

Mwaka 1984 nilianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kigoma, katika mji wa Kigoma. Nakumbuka kupelekwa Shule siku ya kwanza na mama yangu mzazi Bi Shida Salum (Mungu amrehemu) nikiwa sina viatu yaani pekupeku wala begi la mkononi, nilikuwa nimebeba mfuko wa nailoni. Nakumbuka usiku wa kuamkia siku ya kwanza kwenda shule, sikulala kwa furaha na hamu ya kuwa msomi, nilijisikia fahari kuanza shule japokuwa sikuwa na kitu chochote cha zaida zaidi ya kaptula ya shule na shati liloshonwa kwa kitambaa cha sanda. Pia nilianza shule nikiwa nimechelewa kwa mwaka mmoja maana wenzangu walianza wakiwa na miaka 7. Mwaka 1983 nilipopelekwa shule mkono wangu haukuweza kushika sikio upande wa pili, ambacho kilikuwa kipimo cha kuandikishwa darasa la kwanza.
Hali ya maisha wakati huo ilikuwa mbaya sana. Nakumbuka kwenda shuleni nikiwa sina kitu tumboni au siku nzima nilikunywa uji usio na sukari. Uji wenyewe ulikuwa ni wa unga wa njano uliotokana na mahindi ya njano ambayo tuliambiwa nchi yetu ililetewa kama msaada kutoka nchini marekani.
Shule yetu kama zilivyokuwa shule nyingi za wakati huo hatukuwa na madawati ya kutosha na vyumba vya madarasa vilikuwa vichache sana. Ilikuwa ni kawaida kwa wadogo (darasa la kwanza mpaka la tatu) kusomea chini ya mwembe na kukaa juu ya matofali. Hali hiyo ilipelekea kaptura yangu ya shule kuwekwa viraka vingi maana ilikuwa inachanika mara kwa mara. Nyakati nyingine ilibidi kwenda shuleni na shati likiwa halijakauka hasa siku za alhamis, siku ya usafi na iwapo nikiwa zamu ya mchana kwani nilikuwa nina shati moja tu tena lililotokana na kitambaa cha sanda.

Kwa dhahiri, watoto wa masikini na matajiri tulikuwa shule moja, darasa moja hata wote kukaa kwenye matofali. Watoto watawala na watawaliwa tulicheza mpira pamoja, kuruka dana na hata kuruka kamba. Hatukujisikia wanyonge kwa sababu hatuna viatu au kuvaa kaptura zenye viraka na mashati ya sanda. Kamwe sikumbuki kudharauliwa shuleni sababu ya uduni wa maisha yangu. Heshima ilitokana na uwezo wako darasani na kupitia hilo nilipata marafiki wa kutoka madaraja yote ya maisha. Nakumbuka mtoto wa Mkurugenzi wa Maendeleo Mkoa wa Kigoma ndugu Daniel Masanja ndiye alikuwa rafiki yangu wa karibu na kwa kuwa sikuwa na hata pesa ya kununua bajia wakati wa mapumziko, yeye alikuwa ananinunulia.

Huko baadaye, ada yangu ya kidato cha kwanza ililipwa na Mzee Sebastian Kasomi ambaye mwanaye Kasomi Mabula alikuwa rafiki yangu mkubwa mara alipohamia shuleni kwetu akitokea mjini Shinyanga. Mzee Kasomi alikuwa Mkuu wa idara ya Kodi ya Mapato mkoani Kigoma.

Licha ya uduni wa maisha watoto wengi tuliishi kwa matumaini makubwa sana. Mwalimu wetu Mkuu ndg. Daniel Andulile alikuwa mkali sana kwa watoto wote bila kujali daraja la maisha la wazazi wao. Alikuwa anatucharaza viboko kwa makosa na utundu bila ubaguzi. Alisisitiza sana kusoma kwa bidii ili kujenga Taifa. Dhana hii ya kujenga Taifa iliingizwa kwenye akili zetu na sisi kumeza bila kujali maana yake. Wakati mwingine tulikuwa tunarudi nyumbani huku tukijadili kitoto kuwa tunajenga Taifa. Kila siku mwendo wa kilometa Sita kwenda na kurudi shuleni.

Elimu hii isiyo ya kibaguzi sasa najua ilitokana na sera za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Jitihada zangu darasani ndio ziilikuwa kipimo cha utu wangu na sio uwezo wa kiuchumi wa wazazi wangu.. Elimu iliyompa fursa sawa za kuendelea na kusonga mbele mtoto aliyekuwa kigoma, kantalamba au Dar es salaam. Elimu iliyokuza ndoto, kuinua ari na kujenga matumaini ya kila mtoto wa kitanzania. Elimu iliyovunja na kusambaratisha matabaka ya kiuchumi na dhamana. Elimu iliyojenga uzalendo na hamasa ya kutumikia taifa letu kwa misingi ya haki, uadilifu na upendo.

Sikuwahi kukutana na Mwalimu Nyerere isipokuwa niliwahi kumwona akiwa ndani ya gari nikiwa nimepanga mstari barabarani alipofanya ziara mkoani kwetu mwaka 1987 nikiwa darasa la nne. Lakini nilikuwa kama ninaishi naye kutokana na namna nilivyotaka kuwa kama yeye. Nikiwa darasa la pili nakumbuka katika mkebe wangu ( mathematical set) mkuu kuu niliweka picha ya kukatwa kutoka kwenye gazeti ya Mwalimu na Kawawa. Na nilijisikia fahari kuwa na picha zao, mara zote nilipokuwa nafungua mkebe kutoa kalamu nilijisemea kimoyomoyo, “siku moja nitakuwa kama wewe”

Licha ya maisha magumu tuliyokuwa tunaishi, maisha ya kupanga mawe kwenye mstari wa kununua mahitaji muhimu kama sukari, sabuni na mafuta kutoka duka la ushirika, maisha ya kushindia uji wa yanga na kutembea mwendo mrefu kwenda shuleni, niliishi kwa imani kubwa kuwa mimi na watoto wengine tupo sawa. Usawa katika kupata elimu, usawa katika kucheza na usawa katika ndoto na matumaini. Nimemaliza elimu ya Chuo Kikuu, ndoto niliyoruhusiwa kuwa nayo kwa sababu ya sera za Ujamaa, za Mwalimu Nyerere.

Ujamaa haukuwa katika usawa wa elimu tu ambapo kila mtoto alipata elimu bure na bora katika Shule za umma bila ubaguzi bali pia namna jamii iliishi. Mtoto alikuwa analelewa na jamii nzima. Ukifanya makosa mtaani mzazi yeyote anakuadhibu ili kukurekebisha. Ukifanya jambo jema, mzazi yeyote anakupongeza.

Mwaka 1985 mwezi Novemba nilipokuwa natoka shuleni, karibia na Benki ya Taifa ya Biashara Tawi la Obed Katikaza, nilikutana na Mama Colleta Furugunya tuliyekuwa tunaishi mtaa mmoja na nikimwita bibi Colleta. Aliponiuliza matokeo yangu ya mtihani wa kumaliza muhula wa pili wa darasa la pili kwa kujiamini nikampa karatasi yangu ya matokeo. Nilikuwa nimeshika nafasi ya tatu darasani nyuma ya Ramadhan Kalukula na Haki Manyaga. Bibi Colleta alinishika mkono mpaka duka la Viatu, Bora Shoes na kuninunulia jozi yangu ya kwanza ya viatu. Viatu vile viliitwa Asante Salim, aliyekuwa Waziri Mkuu wa mwisho wa Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa anajaribu kubadili hali mbaya iliyokuwepo. Hivyo ndivyo nilivyopata viatu vyangu vya kwanza vya shule. Shukrani kwa sera nzuri ya ujamaa, mshikamano na upendo.

TUTAKUKUMBUKA KWA MENGI MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE.

Mwalimu alitaka kustaafu mwaka 1975, watu wakamgomea, mwaka 1980 akataka kung'atuka, watu wakamgoea pia wakihofia itakuwaje bila mwalimu,1985 pia pia waka mgomea,mwalimu aka wakatalia akang'atuka kwa lazima.
Mambo matatu yaliyo mfanya mwl. angatuke madarakani.
1.Mwalimu alijua kuwa yeye ni binadamu anaweza kufa wakati wowote.
2.Mwalimu alijua kuwa akifa akiwa madarakani(raisi), yoyote atakae kuja baada yake atakufa akiwa raisi(hatong'atuka).
3.Mwalimu aliamini kuwa Tukibadirishana uongozi,mara tatu nne hivi,tutajenga utamaduni wa kuachiana madaraka.
R I P mwal. J K Nyerere.

Thursday, October 13, 2016

LIVERPOOL HAINA KITETE BALI IMARA KUIKARIBISHA MAN U DIMBA LA ANFIELD.


Golikipa wa Liverpool amefunguka kuwa timu yake haina hofu kwa mchezo ujao dhidi ya amahasimu wao katika Ligi kuu ya Uingereza . 
___________________
Manchester United na Liverpool watakutana uso kwa uso Jumatatu. Wakati golikipa wa Liverpool Loris Karius akisema kuwa haofii chochote na anacho zingatia ni kuhakikisha kuwa anacheza vyema vile anavyopaswa. __________________ Golikipa huyo raia wa Ujerumani ameiambia timu ya Wachambuzi wa Ligi ya Premium kuwa "Manchester United ni wazuri, wana timu imara lakini sisi tuna timu thabiti yenye nguvu na hasa ukizingatia tunachezea dimba la nyumbani" ____________________ Kisha akaongeza: "Tunawaheshimu lakini katu hawatupi hofu, tunachojua ni kushinda mchezo huo. #WeAreLiverpool #lfctz #Liverpoolfc #Anfield #YNWA @lorisk21
#SPORTSRIPOTI
Bibi na uzi wake.
Wanandoa naye Bwana Harusi katupia vazi lake kipenzi.
Nani kuibuka kidedea Jumatatu?

Dk.KIGWANGALLA AOMBEWA DUA NA SHEIKH MKUU WA MABOHORA DUNIANI.

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akipata picha pamoja baadhi ya vijana ambao walipata kufunga ndoa na wake zao ndoa ambazo zaidi ya 50 zimefungwa huku Shehe Mkuu huyo wa Mabohora Duniani pia alipata kuzibariki.

Mbali na kutoa dua kwa Dk. Kigwangalla,   Sheikh Dkt. Syedna ameahidi kuleta wawekezaji wa Kibohora kutoka sehemu mbalimbali Duniani kwa ajili ya kuwekeza kwenye ujenzi wa Mahospitali ikiwemo Hospitali za Rufaa za kisasa pamoja na Viwanda vya Dawa hali ambayo itapunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kufuata matibabu.

Pia viwanda vya dawa vitashusha gharama za dawa nchini na kupunguza ucheleweshaji unaosababishwa na kuagiza dawa nje ya nchi.

Aidha, katika tukio hilo, usiku huu, Dk.Kigwangalla ameweza kushuhudia ndoa za Vijana zaidi ya 50 zikifungishwa na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna.

Mbali na Dk.Kigwangalla kuombewa dua maalum na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna, Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba aliungana katika kuombewa na Shehe huyo.

NEW VIDEO Nukobimeze full HD


Published on Sep 27, 2016
Expensive video than That one for Diamond plantnumz, Big Fizzo, Meddy, even The ben can't rich it ....... is Davidson from burundi- Bujumbura

UHAKIKI WA TIN NAMBA.

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA yasogeza mbele muda wa kuhakiki TIN namba kwa wakazi wa Dar es Salaam.

WATOTO 28 WENYE MATATIZO YA MOYO WANATARAJIWA KUFANYIWA UPASUAJI NA MADAKTARI WA MOYO KUTOKA SAUDI ARABIA.

Zaidi ya watoto 28 wenye matatizo ya moyo wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji na madakitari wa Moyo kutoka Saudi Arabia.

ALIYEJIFANYA AFISA WA JESHI LA WANANCHI ANASWA NA TAKUKURU MWANZA.

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Bw. Erest Makale akitoa taarifa hii leo katika ofisi zake. 
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mwanza, imemkamata Bi. Felister Mathias kwa kosa la kujifanya Afisa wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kujipatia pesa Tshs. 240,00/= badaya ya shilingi laki tano (500,000/=) alizoomba kutoka kwa mwananchi ambaye jina lake limehifadhiwa.

Kwa mujibu wa Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Ernest Makale anasema kuwa Bi. Felister Mathias Mawe aliomba shilingi 500,000/= kutoka kwa mwananchi huyo ili aweze kumsaidia kupata nafasi ya kujiunga na jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) 
BOFYA KUSIKIA TAARIFA HIYO.

Mtuhumiwa Bi. Felister Mathias Mawe akisimulia waandishi wa habari kilichotokea mpaka akaingia kwenye mtego huo wa kutapeli. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.


Mtuhumiwa Bi. Felister Mathias Mawe
Mwanajeshi Mstaafu Bi. Sophia Chacha.
Aidha Mwanajeshi Mstaafu Bi. Sophia Chacha naye amekamatwa na kuhojiwa akitajwa kuwa amekuwa akimsaidia mtuhumiwa huyo kwa kumuunganisha na watu waliokuwa wakihitaji kujiunga na jeshi hilo hasa wasichana. Jeh anamfahamu vipi mtuhumiwa. 
BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.

Bi. Felister alikamatwa na TAKUKURU mnamo tarehe 10/10/2016 katika Hoteli ya Wendele iliyopo Kirumba jijini Mwanza.

Mtuhumiwa tajwa amekuwa akijipatia fedha kwa watu mbalimbali waliokuwa wakihitaji kujiunga na jeshi hilo kwa madai kwamba atawasaidia kupta nafasi kwa kiwango cha shilingi laki tano (500,000/=) kwa kil mmoja.


Aidha kwa mujibu wa ushahidi uliopatikana kitendo cha mtuhumiwa kujifanya Afisa wa Jeshi hakihusiani na Makosa yaliyo chini ya sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Namba 11/2007, hivyo jalada lenye tuhuma hiyo namba PCCB/MZ/ENQ/40/2016 limehamishiwa kwa Wakili wa Seriali Mfawidhi ili Mtuhumiwa aweze kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.





Vipi hali ya Rushwa kwa mkoa wa Mwanza, na Sekta, Vitengo vipi vimekithiri kwa Rushwa? Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Ernest Makale anafunguka zaidi.....BOFYA PLAY KUSIKILIZA.