ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 26, 2016

JENERALI ULIMWENGU APATA AJALI YA GARI, AKIMBIZWA MOI.

Taarifa iliyotufikia inaeleza kuwa, Mwandishi Mkongwe nchini na Mwenyekiti wa Bodi ya Gazeti la Raia Mwema, Jenerali Ulimwengu amepata ajali mapema asubuhi ya leo, na kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa Moi kwa matibabu.

Ajali hiyo imehusisha gari alilokuwa akiendesha yeye aina ya Benz na gari nyingine iliyoigonga gari hiyo upande wa Ubavuni.
Habari za hivi punde zinapenya zikisema kuwa Ulimwengu anaendelea vizuri na kwa chochote kitakachoendelea tutaendelea kukutaarifu mdau.

CHAMELEONE AVUNJA NDOA YA WATU UGANDA.

Mwanamke nchini Uganda amepewa talaka baada ya kulia jina la Chameleone wakati akishiriki mapenzi na mumewe

– Chameleone ameweka kisa hicho kwenye Instagram baada ya kuchapishwa na gazeti moja la Uganda

Mwanamke mmoja Uganda amepewa talaka baada ya kuliita jina la msanii msifika Jose Chameleone wakati wakishiriki mapenzi na mumewe.

Habari hizo zimeenea kote Uganda baada ya mume huyo kuapa kumfurusha mkewe alipomlia mwimbaji huyo wa kibao maarufu Valu Valu.
Msanii wa Uganda Jose Chameleone. Picha: Instagram/jchameleone

Chameleone alionekana kufurahishwa na tukio hilo kiasi cha kupiga picha za habari zenyewe kwenye gazeti moja la hapo.

“Mume amfukuza mke kwa kumite Chameleone wakati wakishiriki mapenzi,” msanii huyo aliandika kwenye maelezo ya picha hiyo.

Kisa hicho kinajuia siku chache tu baada ya mwimbaji huyo maarufu wa Uganda kushirikiana na kundi la Elani katika kolabo ya “My Darling”, wimbo unaoangazia mapenzi, changamoto na kutoelewana kunakowakumba wapenzi.

MBUNGE WA RUFIJI AHAHIDI KULIVALIA NJUGA TATIZO SUGU LA WAKULIMA NA WAFUGAJI(2)

Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akiwa anachangia hoja.
NA VICTOR MASANGU, UTETE RUFIJI
MBUNGE  wa jimbo la Rufiji Mkoani Pwani Mohamed Mchengerwa ameahidi kulivalia njuga suala la migogoro ya ardhi inayotokana na jamii ya wafugaji na wakulima ambao wamekuwa wakigombania maeneo ya mashamba na kusababisha kutokea kwa mapigano ambayo wakati mwingine yanapelekea uvunjifu wa amani.

Kuwepo kwa hali hiyo ya migogoro ya ardhi kwa wakulima na wafugaji  katika halmashauri ya Rufiji kunatokana na  baadhi ya wafugaji kuamua kuvunja sheria na taratibu zilizowekwa na   kwenda kulisha mifugo yao katika maeneo yaliyotengwa maalumu kwa ajili ya shughuli mbali mbali za kilimo.

Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa wa viongozi katika halmashauri hiyo mpya ya ya rufiji, ambapo alisema mesema hawezi kuwavulilia wale wote ambao wataonekana wanakwenda kinyume cha sheria za nchi, na kuhakikisha kila mfugaji na mkulima anatengewa maeneo yao rasmi kwa ajili ya kufanyia shughuli zao lengo ikiwani  kuepukana na migogoro na  mapigano ambayo yamekuwa yakijitokeza kutokana na kugombania ardhi.

Aliongeza kwamba nia yake kubwa ni kuhakikisha naweka mikakati kabambe ambayo itaweza kuwawasaidia wananchi wake wakiwemo wafugaji na wakulima kwa kushirikina na viongozi wa halmashauri katika kuwatenge maeneo yao maalumu ambayo yataweza kusaidia kuepukana na migogoro hiyo ya ardhi.

“Mimi kama mbunge wa jimbo hili la rufiji ninatambua kuwepo kwa changamoto kubwa na  mogogoro katika ya wakulima na wafigaji, laki I dhamora yangu kubwa nataka nione wanachi wangu wa jimbo la rufiji wanakaa kwa amani bila ya kuwepo kwa mapigano yoyote kwa hiyo ili nitalivalia njuga na kuhakikisha kwamba sula la amani na utulivu linakuwepo,”alisema Mchengerwa.

Aidha alisema kwamba anatambua wananchi wa jimbo lake wanategemea sana shughuli za kilimo hivyo kwa sasa wameshaweka utaratibu wa kutenga maeneo ya wafugaji ili wasiweze kuingia katika mashamba ya wakulima na kupelekea vurugu z amara kwa mara kitu amabcho sio kizuri na kinarudisha nyuma maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Saidina Malenda mara baada ya kushindakatika uchaguzi huo  alisema  atahakikisha nasharikina bega kwa began a viongozi wenzake kwa lengo la kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi wa Rufiji.

Malenda aliongeza kuwa anawashukuru madiwani wenzake kwa kuweza kumchagua kuwaongoza na kubainisha kwamba atafanya kazi bidii zote na kwa kushirikina katika mambo mbali mbali ya kimaendeleo  bila ya kuwa na ubaguzi wa aina yoyote wa itikadi ya vyama  ili kuweza  kuwatumikia wananchi katika huduma mbali mbali wanazozihitaji.

Katika uchaguzi huo wa halmashauri mpya ya Wilaya ya Rufiji,uliofanyika utete nafasi ya Mwenyekiti ilikwenda kwa Saidani Malenda ambaye alipata kura 11 kati ya kura 19 zilizopigwa, ambapo nafasi ya Makamu mwenyekiti ilikwenda kwa Hawa Mtopa  ambaye aliyepata kura 10 katika ya kura 19 zilizopigwa.

LEMA AKAMATWA NA POLISI.



Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA)
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA)

CHANZO:- Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema(CHADEMA)  amekamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake alfajiri  ya leo. Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro amethibitisha tukio hilo, lakini hakutaja sababu za kukamatwa kwa mbunge huyo.
Jana Jeshi la Polisi mkoani Kigoma liliwakamata viongozi waandamizi wanne wa Chadema mkoa wa Kigoma na jimbo la Kigoma mjini kwa kile kinachodaiwa ni kujihusisha na vitendo vya uchochezi.
Waliokamatwa na kuwekwa mahabusu ni mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Kigoma, Ally Kisala, Katibu wa Baraza la vijana Chadema mkoa (Bavicha), Omary Gindi, Katibu wa chama jimbo la Kigoma mjini, Frank Ruhasha na Mwenyekiti wa mtaa wa sokoni katika Kata ya Katubuka, Moses Bilantanye. 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna msaidizi wa Polisi (DCP) Ferdinand Mtui alikiri viongozi hao wanne kushikiliwa kituoni hapo kwa muda lakini walipata dhamana, hivyo kuruhusiwa kuondoka na kutakiwa kuripoti kituoni hapo leo Ijumaa.

MAGAZETI YA LEO;- AMANI KWANZA, VUGUVUGU LA UKUTA: VIONGOZI WA DINI KUTINGA KWA JPM, MUUAJI WA POLISI MBANDE AJULIKANA: JPM APEWA MASHARTI KUVUNJA UKUTA:


Thursday, August 25, 2016

AIRTEL YAWAPA SEMINA MAWAKALA MKOA WA MWANZA JUU YA HUDUMA MPYA YA AIRTEL MONEY TIMIZA.

Msimamizi mkuu wa uelimishaji wa huduma ya Airtel Money Timiza, Rwebu Mutahaba akitoa semina kwa Mawakala wa mihamala ya fedha za mtandao jijini Mwanza juu ya mikopo hiyo ya mtando wa Airtel ambayo imekuja kama sehemu ya maboresho ya huduma na kuwarahisishia wananchi wa Tanzania linapokuja suala la mtaji. 
Mawakala wa mihamala ya fedha za mtandao jijini Mwanza kwa umakini wakisikiliza mafunzo juu ya mikopo hiyo ya mtando wa Airtel ambayo imekuja kama sehemu ya maboresho ya huduma na kuwarahisishia wananchi wa Tanzania linapokuja suala la mtaji. 
Msimamizi mkuu wa uelimishaji wa huduma ya Airtel Money Timiza, Rwebu Mutahaba akitia msisitizo zaidi katika semina kwa Mawakala wa mihamala ya fedha za mtandao jijini Mwanza juu ya mikopo hiyo ya mtando wa Airtel ambayo imekuja kama sehemu ya maboresho ya huduma na kuwarahisishia wananchi wa Tanzania linapokuja suala la mtaji. 
Mawakala toka viunga mbalimbali ndani ya jiji la Mwanza wamekusanyika hapa ndani ya ukumbi wa Gold Crest Hotel kwa nia ya kupata mafunzo.
Somo limekolea na Airtel Money Timiza.
Airtel Money Timiza ni mikopo nafuu isiyo na masharti magumu zaidi ya namba ya mteja ya mawasiliano na historia ya utumiaji wa huduma ya Airtel Money Timiza.
"Ili mteja apate kukopeshwa kiwango kikubwa cha fedha, Airtel Money Timiza itatizama Je ni mteja anatumia vipi mahamisho na uchukuaji wa fedha kupitia Airtel Money yake...?
Kadri mteja anavyotumia Airtel Money zaidi ndivyo anavyopata nafasi ya kukopeshwa zaidi nacho kiwango kikipanda...." Somo la semina likiendelea
Washiriki kwa umakini na semina ya Airtel Money Timiza.
'MUDA NI MALI' = Jinsi Airtel Money Timiza inavyokomboa muda huku ikimkuza na kumnyanyua mwananchi toka lindi la umasikini.
Msimamizi mkuu wa uelimishaji wa huduma ya Airtel Timiza, Rwebu Mutahaba akitoa semina kwa Mawakala wa mihamala ya fedha za mtandao jijini Mwanza juu ya mikopo hiyo ya mtando wa Airtel ambayo imekuja kama sehemu ya maboresho ya huduma na kuwarahisishia wananchi wa Tanzania linapokuja suala la mtaji. 
David Wankuru ambaye ni Meneja wa Airtel Mkoa wa Mwanza akifafanua kilichofanyika ndani ya semina kwa mawakala, masharti na masuala yote juu ya Airtel Money Timiza.
 BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.

Ni sifa zipi zitampa mteja fursa ya kuweza kukopeshwa na Airtel Money Timiza? Joel Laizer ambaye ni Meneja wa Mauzo Airtel Mwanza anafunguka zaidi.
 BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Mawakala - Kalunde Kafiti na wenzake hapa wanafunguka mengi juu ya
1.Wazo la Airtel Timiza linamanufaa gani kwa wenye kufanya kazi ya miamala?
2. Nini Tahadhari kwa matapeli wanaoweza kuitumia Airtel Money Timiza kufanya yao?
3.Jeh Mikopo itawasaidiaje wajasiliamali ambao suala la mtaji limekuwa changamoto kubwa kwao?
BOFYA PLAY KUSIKILIZA WALICHOSEMA.

RATIBA KWA MAKUNDI UEFA CHAMPIONS LEAGUE HII HAPA.

Ratiba kamaili ya hatua ya makundi ya Uefa champions League imetoka. Timu za Uingereza zinaonekana kuwa na ahueni kwenye hatua hii kutokana na kutokuwa kwenye makundi ya vifo huku Leicester wakiwa kwenye kundi ambalo unaweza kuliita nyanya zaidi.
Kwa ratiba hii unatakiwa kuwa na matarajio ya kushuhudia moja ya hatua 16 bora nzuri na yenye ushindani zaidi kwa uwezekano wa vilabu vikubwa kubaki kwenye hatua ya makundi ni mdogo sana.

NAIBU WAZIRI WA AFYA DK. KIGWANGALLA AKAGUA MAABARA YA HOSPITALI YA KISHAPU


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla amezitaka Maabara Nchini kuhakikisha zinafuata misingi na kanuni sahihi katika kuzingatia ubora  na ufanyaji.

Akiwa katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Shinyanga, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla aliweza kukagua Maabara ya Hospitali ya Wilaya ya Kishapu  ambapo alibaini mambo mbalimbali yakifanywa bila kuzingatia taratibu sahihi za Mabara huku akiagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanarekebisha mapungufu hayo katika Maabara hiyo.

Miongoni mwa mambo ambayo alikuta katika Maabara hiyo ni pamoja na kutokuwa na taratibu za kiutendaji hasa kwa wafanyakazi wenyewe wa Maabara ambao walishindwa kuzingatia vigezo na msharti ambayo taratibu za Maabara zinahitaji.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akikagua Maabara hiyo ya Hospitali ya Wilaya ya Kishapu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akiangalia moja ya mashine ndani ya Maabara hiyo ambayo wataalamu wa Maabara hiyo hawajaweza kuweka viambata vya kuonyesha kama imefanyiwa matengenezo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akitoa maagizo namna ya Maabara inavyotakiwa iwe na taratibu zake.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akiagana na wafanyakazi wa Hospitali hiyo ya Kishapu
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akiagana na wafanyakazi wa Hospitali hiyo ya Kishapu