ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 13, 2016

ALIYEMKATA MATITI MWANAMKE MKOANI KILIMANJARO ANAPETA KITAANI.

Serikali mkoani Kilimanjaro imeliagiza Jeshi la Polisi kumkamata mtuhumiwa aliyemfanyia ukatili mwanamke mjamzito Mery Lyimo  mkazi wa kijiji cha Ghona kwa kumkata matiti yake mawili na kisha kutoweka nayo.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw.Said Meck Sadick ametoa agizo hilo mara baada ya kumtembelea mwanamke huyo ambaye amejifungua na kushindwa kumlea mtoto huyo  ambaye mkuu huyo wa mkoa amelazimika kumchukua na kumpeleka kwenye kituo cha kulelea watoto cha upendo.

Amesema inasikitisha kuona mtuhumiwa huyo ambaye amemfanyia ukatili mwanamke huyo bado yupo mitaani huku akitishia familia na hiyo licha ya kukamatwa na kuachiwa kwa dhamana.

Baba mzazi wa msichana huyo  Bw.Aloyce Lyimo analaani kitendo hicho na kusema kuwa kwa sasa hana uwezo wa kumtunza msichana huyo na mtoto wake baada ya kutumia gharama kubwa ikiwemo kuuza mali zake kwa ajili ya kumpatia matibabu.

Nao baadhi ya majirani wanaiomba serikali kumchukulia hatua mtuhumiwa huyo ambaye yuko mtaani kwa kuwa wananchi wa kijiji hicho wanaishi wa wasiwasi mkubwa.

Msichana huyo ambaye pia ana ugonjwa wa akili anamweleza mkuu wa mkoa kuwa hali yake kwa sasa inaanza kuimarika jambo kidondo hakijapona.

HUU HAPA USHINDI WA 1-0 YANGA DHIDI YA BEJAIA.


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema walikuwa na nafasi ya kuimaliza Mo Bejaia ya Algeria kwa mabao mengi zaidi.

Yanga imeitwanga Mo Bejaia kwa bao 1-0 katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Pluijm raia wa Uholanzi amesema walikuwa na nafasi nyingi za kufunga, lakini hawakuzitumia.

"Tungezitumia, basi lingekuwa jambo jema sana. Lakini hatukufanya hivyo," alisema.

"Ninaamini tuna kikosi kizuri, lakini bado tunahitaji kurekebisha mambo kadhaa, pia hilo suala la umaliziaji," alisisitiza.

Yanga imeitwanga Bejaia kwa bao la Thabani Kamusoko lililofungwa kwa kichwa kipindi cha kwanza akiunganisha krosi ya Juma Abdul.

Katika mechi ya kwanza kabisa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi, Yanga ililala kwa bao 1-0 ikiwa ugenini dhidi ya Bejaia.

Hii ni mechi ya kwanza Yanga kushinda baada ya kucheza mechi tano, ikiwa imefungwa tatu, sare moja na kushinda moja ambayo ni ya leo.

Sasa Yanga ina pointi nne na inaendelea kubaki mkiani huku Bejaia inabaki na pointi tano sawa na Medeama ya Ghana huku TP Mazembe ya DR Congo ikiwa imejihakikishia kufuzu kwa kubaki kileleni na pointi 10.

UWANJA WA NDEGE WA DODOMA RASMI UMEKAMILIKA.

Baada ya serikali kuamua kuamisha Makao Makuu ya Serikali kutoka Dar es Salaam na kuwa Dodoma tumeendelea kuona harakati hizo zikiendelea kwa kasi ya ajabu ambayo inaleta matumaini kuwa nikweli Serikali Imeamua Kuamishia Makao Mkuu Mjini Dodoma.

Kwa muda mfupi tu tangu Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa aamuru uwanja wa ndege wa Dodoma Utanuliwe ili uweze kukidhi, leo hii uwanja huo unaonekana tayari usha kamilika na muda sio mrefu uwanja huo utaanza kutumika rasmi..


Friday, August 12, 2016

HAYA NDIYO MAAMUZI YA MZEE YUSUF.

Gwiji wa mziki wa taarabu nchini Mzee Yusuf amethibitisha kuwa ameachana na kazi hiyo takribani miezi miwili iliyopita.

Taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii zimeeleza kuwa mwanamziki huyo ameachana na mziki na kuamua kumrudia Mungu.

Akizungumza na Mwananchi Digital kwa njia ya simu usiku huu, mmiliki huyo wa bendi ya Jahazi Modern Taarab amethibitisha kuwa taarifa hizo ni kweli na kuongeza:

“Nashangaa taarifa hizi zinasemwa leo. Ni suala la muda mrefu….takribani miezi miwili iliyopita na sababu ni kuwa nimeamua kumrudia Allah,”

Mwanamziki huyo mzaliwa wa Zanzibar alipoulizwa kuwa ni suala gani lililomsukuma hata achukue maamuzi hayo magumu, alijibu kwa kifupi, “ndivyo tunavyofundishwa na viongozi wa dini.”

Yusuph aliyetamba na vibwagizo kama “Nichumu, nikisi….mwaaaa,” katika baadhi ya nyimbo zake, amesema familia yake imeupokea uamuzi wake kwa mtazamo chanya na kwamba inamuunga mkono.

“Kwa sasa nitaimba kaswida zenye mafundisho ya dini,” amesema nyota huo huku akiahidi kufanya mkutano rasmi kuelezea suala hilo.

Mfalme huyo aliyeonekana kuwa ni gwiji wa taarabu ya kisasa (modern taarab) amezaliwa visiwani Zanzibar mwaka 1977. Aidha amejihusisha na sanaa nyingine kama maigizo.

Ni mshindi wa tuzo katika tasnia ya muziki wa taarab zikiwemo ya Kilimanjaro Music award 2014-15.

Mpambano wa tuzo za Kili ulivyokuwa msimu wa 2014-15

1. Kikundi bora cha mwaka taarab - Jahazi Modern Taarab

2. Mtayarishaji bora wa mwaka bendi - Enrico

3. Mtunzi bora wa mwaka taarab- Mzee yussuf

4. Mwimbaji bora wa kiume taarab - Mzee Yussuf

5. Mwimbaji bora wa kike taarab - Isha Mashauzi

6. Wimbo bora wa taarab (mapenzi hayana dhamana)- Isha Mashauzi

NAIBU WAZIRI WA AFYA Dk. Kigwangalla akutana na Ujumbe kutoka taasisi ya Touch Foundation.

DSCDD_5035Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisikiliza jambo kutoka kwa wageni (Hawapo pichani) wakati wa mazungumzo juu ya uwekezaji wa katika sekta ya Afya.
DSC_5031
Mwanzilishi na Rais wa Taasisi ya Touch Foundation ambae pia ni mstaafu kutoka katika kampuni ya McKinsey, Bwana. Lowell Bryan akimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani).
DSC_5044
Ugeni katika mkutano huo
DSC_5057
Majadiliano yakiendelea
DSC_5029Bwana. Lowell Bryan akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla wakati wa mkutano huo uliofanyika ofisini kwa Naibu Waziri, Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema siku ya Agosti 11.2016 amekutana na wadau wa Sekta ya Afya kutoka taasisi Touch Foundation kuangalia namna ya kusaidia sekta ya Afya hasa kwa maeneo ya pembezoni mwa Nchi ili kuimalisha hudumm hizo.

Ugeni huo kutoka katika Taasisi ya Touch Foundation ya nchini Marekani umeonyesha nia yake ya dhati ya kuendelea kusaidiana na Wizara ya Afya ya Tanzania ikiwemo huduma za akina mama Vijijini.

Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla amekutana na ugeni huo ofisini kwake ukiongozwa na Mwanzilishi na Rais wa Taasisi ya Touch Foundation ambae pia ni mstaafu kutoka katika kampuni ya McKinsey, Bwana. Lowell Bryan ambaye pia alishawai kuwa mshahuri kwa miaka mingi huko kipindi cha nyuma katika masuala ya Afya ya Tanzania.

Ujumbe wa ugeni huo una miradi mbalimbali kama kuzalisha wataalam wa afya, kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto kwa kuboresha mfumo wa rufaa kutoka kijijini kuja mpaka mahala watakapopata huduma na kwa sasa wameanza na wilaya mbili za Sengerema na Shinyanga Mkoani Shinyanga.

Akielezea muda mfupi baada ya majadiliano na ujumbe huo Dk. Kigwangalla alibainisha kuwa Wameonyesha nia ya kuendelea kuisaidiana na Tanzania katika masuala ya Afya hivyo mikakati ya itaendelea kuwa endelevu hasa katika miradi ya kusaidia kupunguza vifo kwa akina Mama Wajawazito.

“Mradi wao wa kupunguza vifo vya wakinamama wajawazito pamoja na watoto, unatekelezwa kwa kuboresha mfumo wa rufaa kutoka kijijini kwa wakinamama wajawazito kuja mpaka wanapoweza kupata huduma za kiafya hii ni pamoja na Kituo cha Afya ama Hospitali kubwa.
Wametengeneza utaratibu wa usafiri, mawasiliano ya simu na kuwapatia wahudumu posho katika Wilaya ya Sengerema na shinyanga wakishirikiana na Vodafone Foundation.

Watatusaidia kutengeneza mikakati ya kiufundi ya namna ya kuboresha huduma za afya ya msingi, huduma hizi za msingi ni kama vituo vya afya na zahanati ikiwa ni pamoja na kutupa utaalam katika eneo la kufanya tathmini ya rasilimali watu katika sekta ya afya, kuanzia gharama za kuajiri madaktari ama kada za chini” aliongeza Naibu Waziri Dk. Kigwangalla.
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).

MHE. GODFREY ZAMBI APOKEA KADI YA MFUMO WA "WOTE SCHEME" KUTOKA MFUKO WA PENSHENI WA PPF

PPF Kadi ya Wote Scheme
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akipokea kadi ya Mfumo wa "Wote Scheme" kupitia Mfuko wa Pensheni wa PPF kutoka kwa Meneja wa PPF kanda ya Kusini Ndg. Kwame Temu.

PPF Kadi ya Wote Scheme

Meneja wa PPF kanda ya Kusini Ndg. Kwame Temu akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi wakati wa kumkabidhi Kadi ya Mfumo wa "Wote Scheme".

PPF Kadi ya Wote Scheme
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akitoa neno la shukrani kwa Meneja wa PPF (Hayupo pichani) wakati wa kupokea kadi ya Mfumo wa "Wote Scheme" kupitia Mfuko wa Pensheni wa PPF.


Na. Fungwa Kilozo, Lindi
Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi ameweza kupokea Kadi ya Mfumo wa "Wote Scheme" kupitia Mfuko wa Pensheni wa PPF. 

Mhe. Zambi amepatiwa kadi hiyo ikiwa ni Siku nne tu zimepita baada ya Kujiunga na Mfumo huo katika Banda la PPF lililokuwa katika maonyesho ya Kilimo na Biashara Nane nane yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Lindi katika Viwanja vya Ngongo.

Katika Hafla hiyo ya makabidhiano ya Kadi hiyo Mh. Zambi ameutaka Mfuko wa PPF kutanua wigo na kuwafikia wananchi wengi zaidi hasa wale wa vijijini kwani amesema kuwa mfuko huo unafaida nyingi ambazo wananchi hao ambao hawajabahatika kufika katika banda la maonyesho ya Nane nane watazikosa hasa mfumo wa "Wote Scheme" ambao hata yeye amefurahishwa nao na akaamua kujiunga.

MSIKILIZE HAPA AKIELEZEA....

YALIYOJIRI KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI LEO August 12, 2016


Mgodi wa dhahabu wa GGM watekeleza agizo la Rais John Magufuli la kuwapa vijana mabaki ya mawe ya dhahabu.

Walimu wa shule za msingi na sekondari za jijini Dar es Salaam watatumia usafiri wa Treni bila ya kulipa nauli.

Thursday, August 11, 2016

RAIS DKT MAGUFULI AHUTUBIA MAELFU YA WANANCHI WA JIJI LA MWANZA UWANJA WA FURAHISHA LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi wa mkoa wa Mwanza na maeneo ya kanda ya ziwa katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Furahisha, Kirumba.
RAIS Dk. John Magufuli, sasa amegeukia utumbuaji majipu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku akituma salamu kwa viongozi wa chama hicho ngazi ya taifa, mikoa, wilaya, kata na matawi.
Kutokana na hali hiyo, amesema hivi sasa mafisadi ndani ya CCM hawana nafasi na anataka kukirudiusha chama hicho kwenye misingi ya uadilifu na nidhamu, kama ilivyokuwa enzi za  Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere.
Kauli hiyo aliitoa leo  jijini Mwanza, alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi katika Uwanja wa Furahisha, ambapo alisema ili kuhakikisha nidhamu inarudi ndani ya CCM mali zote za chama hicho zitakaguliwa ili mapato yake yaweze kujulikana na si kuwaachia viongozi  wachache ambao wamekuwa wakizitumia kwa masilahi yao binafsi.
Rais Magufuli, alisema hawezi kuhamasisha wananchi wawe na nidhamu wakati chama chake hakina nidhamu jambo ambalo atahakikisha analirudisha kwa nguvu zake. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Alisema lazima wasimamie mali za chama na kuonya kuwa chini ya uongozi wake kamwe viongozi watakaowania nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa chama watakaobainika kutoa rushwa atawakata majina yao ili kuwaengua kugombea.
Kutokana na hali hiyo alisema mafisadi wakae chonjo kwani atawatia mbaroni na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria ili rasilimali za Watanzania ziendelee kudumu.
Alisema hadi sasa Serikali imetenga Sh bilioni 1.2 kwa ajili ya kuanzisha Mahakama ya Mafisadi ambayo itawachukulia hatua watendaji wote watakaobainika kutumia fedha za umma vibaya.
Alisema, kutokana na hali hiyo, viongozi wanapaswa kufanya kazi na kuwachukulia hatua wale watakaobainika kwenda kinyume na majukumu yao na kwamba watakaobainika wanataka kuwakwamisha, wawachukulie hatua ili waweze kukwama wenyewe.
Rungu kwa Polisi
Alisema hadi sasa Jeshi la Polisi limeweza kutimiza majukumu yake ipasavyo hasa katika uamuzi wa kupambana na majambazi.
“Kazi mliofanya ya kupambana na majambazi wale ni kubwa, nawasisitiza anayetaka kuchezea moto muwasheni hapo hapo…tumechoka kubembelezana lazima watu wafanyekazi na si ujambazi,” alisema.
MACHINGA
Akizungumzia kuhusu wamachinga, Rais Magufuli aliwaagiza viongozi wa Mkoa wa Mwanza kuacha kuwaondoa wamachinga katikati ya Jiji na kuwataka kukaa nao  ndani ya kipindi cha miezi miwili au mitatu ili waweze kuangalia sehemu nzuri ya kuwapeleka kwa ajili ya kufanya shughuli zao.
“Huwezi kuwapeleka wamachinga mlimani, wanakwenda kumuuzia nani? Hawa ndiyo walionichagua mimi, ninaomba muwaache hapo halafu mkae na kujadiliana nao ndani ya miezi miwili au mitatu ili mjue wapi wataweza kwenda kufanya shughuli zao ili waweze kupata faida kwa sababu na wenyewe wanatafuta pesa,” alisema.
Aliongeza, lakini wamachinga wanapaswa kutambua kuwa, Serikali inataka kodi, hivyo basi wasikubali kutumiwa na wafanyabiashara wakubwa ambao ndiyo wakwepa kodi kwa kuwapa bidhaa bila ya stakabadhi hali inayoweza kusababisha kukamatwa.
“Mkienda kununua bidhaa lazima wawape risiti ya EFD, kwa sababu wafanyabiashara wamekuwa na tabia ya kuwapa bidhaa zao na kwenda kuuza huku wakijua kuwa wanakwepa kodi,” alisema.
Simon Group kuchunguzwa
Kiongozi huyo wa nchi alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,  John Mongella, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. CharlesTizeba pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuzirejesha mali za Chama Kikuu cha Ushirika cha Nyanza (NCU LTD)  kikiwemo Kiwanda cha New Era kilichouzwa kwa Kampuni ya Simon Group inayomilikiwa na Simon Kisena.
Simon Group chini ya mwenyekiti wake mtendaji, Simon Kisena ndiyo walipewa tenda ya kuendesha Shirika la Usafiri Jiji la Dar es Salaam (UDA), ambapo suala hilo bado giza nene limetanda.
Hatua hiyo ilimfanya Rais Magufuli, kusema kuwa NCU iliwahi kutangazwa kuwa miongoni mwa vyama vikubwa vya ushirika barani Afrika kutokana na kufanya vizuri, lakini sasa iko hoi huku mali zake zilizoenea kila sehemu zikiwemo Ginnery zikiuzwa kwa bei ya kutupa.
Kutokana na hali hiyo aliiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (Takukuru), vyombo vya ulinzi na usalama kuanza uchunguzi haraka ili mali hizo za NCU zilizouzwa zirejeshwe huku akikitaja kiwanda cha New Era ambacho alisema kimeuzwa kwa Simon Kisena wa Kampuni ya Simon Group Ltd nacho kirejeshwe.
“Ninaifahamu Nyanza maana mimi nimefanya kazi New Era, sasa imeuzwa kwa Shilingi milioni 32 badala ya Sh bilioni 1, vyombo vya usalama vipi, Takukuru ipo sasa sijui mnachunguza nini kama siyo haya, mali zipo nataka zirejeshwe kwa wakulima.
“Najua aliyeuziwa ni Simon Group, mimi huwa sifichi sasa nataka mlisimamie hili na hizo mali zirejeshwe kwa wakulima kama ulivyoeleza Mkuu wa Mkoa,” alisema Rais Magufuli.
Pamoja na hali hiyo alimtaka Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba, kusimamia jambo hilo  huku akimuonya kutoogopa kupoteza kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwani yeye kama Rais anavyo viti vya ubunge na atamteua tena kushika nafasi hiyo.
Uvuvi haramu
Rais Magufuli amemuagiza Waziri Tizeba kuanzisha oparesheni ya kusaka nyavu haramu na makokoro kwa kuyachoma moto ili kuliokoa Ziwa Victoria kwa faida ya kizazi kijacho.
Alisema kabla ya kuwa rais aliwahi kuwa Waziri wa Uvuvi na kwamba alichoma moto na kuteketeza makokoro hivyo kumtaka kuanzisha oparesheni ndani ya Ziwa Victoria ikiwa ni pamoja na kukamata magari yanayosafirisha nyavu haramu ikiwa ni pamoja na kutaifisha magari yanayozisafirisha kuziingi hapa nchini.
Utekelezaji wa ahadi
Akizungumzia ahadi alizotoa wakati wa kampeni za  Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, alisema alihaidi kutoa elimu bure na kwamba mara baada ya kushinda aliamua kusaka fedha za kukamilisha mpango wake kwa kuanza kusimamia ukusanyaji wa mapato bandarini ambako alifanikiwa kukusanya mabilioni na kuanza mfumo wa utoaji elimu bure.
Alisema katika bajeti ya mwaka huu serikali yake imetenga fedha Sh trilioni moja za kununulia meli moja mpya ya kubeba abiria 1000 na tani 400 za mizigo itakayotoa huduma Ziwa Victoria na ikiwa ni pamoja na kuanza ujenzi wa reli ya kiwango cha Standard Gage.
Alisema pia kutokana na kubana matumizi na kuzuwia safari za nje ya nchi kwa watumishi wa Serikali ameweza kupata fedha za kununulia ndege mbili nchini Canada ambapo kwa sasa zinatarajia kuwasili  mwezi Septemba mwaka huu na kuanza kutoa huduma huku ndege nyingine ikiendelea kutengenezwa.
Hata hivyo aliagiza mkandarasi anayeshughulika na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza kuendelea mara moja ili uwanja huo ukamilike na kuwa wa kisasi utakaotoa huduma ya ndege kubwa hivyo kuufanya mji wa mwanza kuwa kitovu cha nchi za maziwa makuu.
Mongela
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema katika moja ya mipango yake Mkoa wa Mwanza amedhamiria kufufua kilimo cha zao la pamba ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanarejesha mali za Chama Kikuu cha Ushirika cha Nyanza ambazo ziliuzwa kwa bei ya kutupa.
Mongella alisema NCU waliuza majengo yake manne likiwemo la jengo la makao makuu ya chama hicho pamoja na hosteli za Pamba huku akibainisha kuwa kiwanda cha New Era kiliuzwa kwa Sh milioni 32 pamoja na uuzwaji wa viwanja vinne kwa Sh milioni 70 vyote vikiwa ni mali ya ushirika.
Mongella, alisema NCU imeliwa na sasa wameanza kusimamia urejeshaji wa mali zake kwa kushirikiana Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. CharlesTizeba na kuomba awaunge mkono ili kuhakikisha mali hizo zinarejea na ushirika unakuwa na hadhi yake.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Angelina Mabula akiwasilisha utekelezaji pamoja na maombi yake kwa Serikali.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula akiwasilisha utekelezaji pamoja na maombi yake kwa Serikali.
Nao wananchi walikuwa na yao ya kuwasilisha.
Elimu.....
Mwanamuziki mahiri wa muziki wa dansi nchini Christian Bella akitumbuiza umati uliofika kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano wake hii leo katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Baada ya kufanya vyema jukwaani mwanamuziki Christian Bella alipata fursa ya kupeana mkono na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Sasa ni zamu ya Mama Janet Magufuli.
Kutoka Jukwaa kuu hawa ni JJ Band Wakali wa Town.
Jembe Fm imeruka LIVE toka eneo la kusanyiko.
Pamoja sana watangazaji toka Jembe Fm Mwanza, kutoka kushoto ni Juma Ayoo, Mbaba Vc na Mansour Jumanne.
Taswira kusanyikoni.
Mkusanyiko.
Kutoka kushoto ni Zarry Edosha, Johari Ngassa, Oxy Okeleky na Coooly Chata.
On Air LIVE ni Gsengo, Mdau wa TANROAD Mwanza na Mansour Jumanne
Rais alipita hapa.......
Umma uliojitokeza.
Another angle.