ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 9, 2016

20% adai ujio wake mpya unawafanya wasanii wengine watamani kujificha.



Msanii wa muziki aliyewai kutamba na wimbo ‘Malumbano’ 20% amedai baada ya kurudi chini ya Label ya ‘Combination Sound’ chini ya producer Man Water, kuna wasanii ambao hawajapenda.


Muimbaji huyo ambaye alishinda tuzo tano za Kilimanjaro Music Award mwaka 2011, amesema kuwa, kurudi kwake Combination Sound kuna wasanii wanaona watakosa nafasi zao katika muziki.

“Nikwambie tu kuna mwanamuziki ambaye hana uwezo wa kuandika mashairi kama 20% hawezi kufurahia muungano kati yangu na Man Water kwa sababu anajua tayari balaa limeshaanza, vumbi linakuja, kwa hiyo huyo huyo msanii alikuwa ana support ugomvi kati ya 20% na Man Water,” alisema 20%

Pia muimbaji huyo alisema tuzo za Kili ndio kitu ambacho kimchanganya na kumfanya apotee kwenye game.



IDD MKWELA ALIVYO MSAMBALATISHA NASSORO MADIMBA BAGAMOYO MKOA WA PWANI

IVO MAPUNDA NA TAULO LAKE KUREJEA LIGI KUU KENYA.





Baada ya kutokuwa na misimu kadhaa yenye mafanikio akichezea vilabu vya Simba SC na Azam FC za Tanzania kipa maarufu nchini ambaye aliwahi kudakia timu ya Yanga SC Ivo Mapunda huenda akarejea nchini Kenya ambako alipata umaarufu akiwa na Gor Mahia.

Kipa Ivo Philip Mapunda aliyemaliza mkataba wake katika klabu ya Azam FC amesema anaimani rekodi aliyoiacha nchini Kenya misimu kadhaa takribani miaka mitatu iliyopita akiwa na mabingwa wa nchi hiyo Gor Mahia maarufu kama Ingwe itambeba katika harakati zake za kusaka maisha mapya katika soka nchini humo.

Ivo ameanza mikakati mizito ya chinichini ili kurejea nchini humo ambako alipata umaarufu mkubwa akidaka huku akiwa na taulo kubwa golini baada ya kumaliza mkataba wake na Azam FC waliomsajili kutoka klabu ya Simba na klabu hiyo kutangaza kutomwongezea mkataba mpya huku ikishusha makipa wawili wakimataifa toka Hispania na Ivory Coast ambao tayari wameanza majaribio na timu hiyo katika viwanja vya Chamazi jijini Dar es Salaam.

Aidha Mapunda mzaliwa wa jiji la Mbeya mwenye asili ya Songea ambaye kabla ya kutua Gor Mahia alianza maisha ya soka nchini Kenya akiwa na klabu ya Bandari ya Mombasa aliyojiunga nayo akitokea kwa mabingwa wa Tanzania Yanga SC amesema mipango yake ya kwanza ni kurejea kucheza ligi kuu ya Kenya ambayo kwa sasa bado inaendelea ila kwa kipindi hiki anataraji kujisajili kwa timu ambayo itampa kandarasi [mkataba] ya muda mfupi.

Akimalizia Mapunda amesema yeye bado anauwezo mkubwa kama awali na umeongezeka mara dufu na kimsingi kuwekwa benchi katika klabu ya Azam si kwamba uwezo wake ulikuwa mdogo ila ni mipango ya kocha wa timu hiyo kuamua mtumia zaidi kipa kinda mwenye kipaji kikubwa Aishi Manula na yeye na mwenzake Mwadini Ally kubadilishana benchi wakati kinda huyo aliyeibukia katika michuano ya Uhai Cup akitamba mpaka katika timu ya taifa Stars.

CAMPUS VYBEZ YA TIMESFM YAKUTANISHA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU KUJADILI CHANGAMOTO YA AJIRA NCHINI.

Watangazaji wa Kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa na Kituo cha redio cha TimesFm ya jijini Dar, Sandra Temu na Raheem wakiongoza mjadala maalumu wa utakaoibua hoja ya kutatua changamoto ya ajira nchini, ambapo mjadala huo umeandaliwa na Kituo cha Timesfm redioni ndani ya kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 kamili usiku. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
  BAADHI ya wanafunzi wa elimu ya Juu kutoka katika vyuo mbalimbali jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza kwa makini Mtangazaji wa kipindi cha Campus Vybez katika mjadala maalumu wa utakaoibua hoja ya kutatua changamoto ya ajira nchini, ambapo mjadala huo umeandaliwa na Kituo cha Timesfm radion ndani ya kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 kamili usiku.
  Mc Pilipili akitoa kibwagizo mara baada ya kukaribishwa.
 Mc Pilipili akijitambulisha kwa vijana, pembeni yake ni Ron Fidanza, Naibu waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Mavunde.
Msimamizi Mkuu wa radio ya TimesFm  Ron Fidanza.
 Mhadhiri wa Lugha wa Chuo cha Ualimu DUCE, Mhe. Ruben Ndimbo akijitambulisha.
 Mmoja wa waalikwa akijitambulisha.
 Meza mkuu.