ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 21, 2016

JEMBEKA FESTIVAL USIKU HUU NDANI YA UWANJA WA CCM KIRUMBA NI NOWMER.

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akitoa neno la ufungua wa Tamasha la pili la JEMBEKA FESTIVAL.
Katika kusherekea mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa redio ya Jembe FM iliyo na makazi yake jijini Mwanza, Mei, 21 kumefanyika tamasha lililopewa jina la JembekaFestival ambalo lilikutanisha mashabiki wa redio hiyo walio mikoa ya kanda ya ziwa kwa kupata burudani ya aina yake kutoka kwa msanii wa muziki wa miondoko ya R& B kutoka nchini Marekani, Shaffer Chimere Smith almaarufu kama NE-YO
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella,  Waziri Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba, Mbunge wa jimbo la Nyamagama jijini Mwanza, Stanislaus Mabula pamoja na Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye wakimsikiliza Dr. Sebastian Ndege ( pichani chini).
Licha ya msanii NE-YO pia kulikuwapo na wasanii wa nchini wakiongozwa na Diamond Platinumz ambaye aliambatana na timu yake kutoka lebo yake ya Wasafi (WCB), wasanii wengine ni Fid Q, Baraka Da Prince, Ney wa Mitego, Maua Sama, Mo Music, Stamina, Juma Nature a.k.a Kiroboto, Ruby na wengine wengi.
Tamasha hilo lilifanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo pia lilihudhuriwa na Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye na Waziri Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba pamoja na Mwanamitindo wa Kimataifa nchini, Flaviana Matata ambao kwa pamoja walionekana kufurahia tamasha hilo la kihistoria kuwahi kufanyika jijini Mwanza.

Kufanyika kwa tamasha hilo kulisimamiwa na mikono ya Vodacom Tanzania ambao ndio wadhamini wakuu, Coca Cola, FastJet, SYSCORP, EF Outdoor, Ndege Insurance Brokers, Jembe FM, Double Tree, KK Security na Mo Entertainment ambao ndiyo waliowezesha kufanyika kwa tamasha hilo.

















DONDOO ZA MAGAZETI>JPM KAEPUSHA VITA ASEMA MAKINDA. CUF YAMKANA LOWASSA. ULEVI WAMPONZA KITWANGA.


SIMU.TV:  JPM kaepusha vita asema Makinda. Mapokezi ya Yanga Mafuriko, Dar yasimama. CUF yamkana Lowassa. Ulevi wamponza Kitwanga.


SIMU.TV:  Aliyetabiri kuuawa kwa Dkt. Shein mbaroni. Magufuli  amtumbua Kitwanga kwa ulevi. Mtoto wa miaka 10 anaswa ugaidi.

Friday, May 20, 2016

NEYO APOKELEWA KAMA MFALME JIJINI MWANZA

Neyo check out from the hotel Hyatt Regency
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo akiondoka katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kiliamanjaro kueelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa safari ya jiji Mwanza kutumbuiza kwenye Jembeka Festival 2016 ambapo wadhamini wakuu ni Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe FM. Kulia ni Meneja wa Hoteli hiyo, Timothy Mlay.
IMG_5465
Attu Mynah and Neyo
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group, Attu Mynah ambao wamedhamini usafiri uliotumika kumwendesha msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo gari aina Mercedes Benz GLE 350 D ya mwaka 2016 katika picha ya kumbukumbu na Msanii huyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Neyo ta Hyatt Regency-The Kilimanjaro
Msanii wa kimataifa Neyo aki-show love na walinzi maalum kabla ya kuelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa safari ya Mwanza.
Neyo official car Mercedes Benz GLE 350 D of 2016
Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo akielekea kwenye gari maalum aina ya Mercedes Benz GLE 350 D ya 2016 lilitolewa na kampuni ya CFAO Motors Group.
Neyo Sorrounded by Tanzanian Bodyguard
Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere akiwa amezungukwa na walinzi maalum alipokuwa akielekea jijini Mwanza.
Neyo at Julius Nyerere International Airport
Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na mlinzi wake wakielekea jijini Mwanza leo jioni.
Costantine Magavilla and Neyo
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla (t-shirt ya blue) na Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakijianda kupanda ndege ya Shirika la Fastjet katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kuelekea jijini Mwanza. Shirika la Ndege la Fastjet ni miongoni mwa wadhamini wa tamasha hilo.
Neyo Crew to Mwanza
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akiwa na 'crew' iliyoambatana na msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakipanda ndani ya ndege ya Shirika la Fastjet ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Jembeka Festival 2016 kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza.
Jembeka Festival 2016 boarding Fastjest Airline
Neyo arrived in Mwanza
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege na Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakishuka kwenye ndege ya Shirika la Fastjet ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Jembeka Festival 2016 mara baada ya kutua jijini Mwanza. Kampuni ya simu mkononi Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na Coca Cola.
IMG_5597
Baadhi ya wapiga vyombo waliombatana na msanii wa Marekani, Neyo wakishuka kwenye ndege ya shirika la Fastjet katika uwanja wa ndege wa jijini Mwanza jioni. Kampuni ya simu mkononi Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na Coca Cola.
Sebastian Ndege
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla, Afisa Habari wa Jembe Media Group, Gsengo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege katika picha ya pamoja.
Neyo on Maasai Shuka
Balozi wa Umoja wa Mataifa mtoto mwanabadiliko wa mazingira, Getrude Clement akimvisha shuka la kimasai Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo baada ya kuwasili jijini Mwanza leo jioni.
Getrude Clement na Neyo
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo aki-'show love' na Balozi wa Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Umoja wa Mataifa, Getrude Clement aliyefika uwanjani hapo kumlaki na kumvisha shuka la Kimasai. Kampuni ya simu mkononi Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe FM.
Bujora Cultural Troup Mwanza entertain Neyo
Msanii wa kikundi cha ngoma cha Bujora Cultural Troupe cha jijini Mwanza akimshikisha nyoka aina chatu msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza jioni hii.
Neyo playing with a snake in Mwanza
Jembe FM Journalist Interviewing Neyo
Watangazaji kutoka Jembe FM Bonz Balaa (kushoto) na Jacquline Shuma (kulia ) wakifanya mazungumzo na Mwanamuziki Neyo kutoka nchini Marekani mara baada ya kuwasili jijini Mwanza kwaajili ya Tamasha kubwa la burudani linalokwenda kwa jina la Jembeka Festival chini ya Udhamini mkuwa wa Vodacom Tanzania.
IMG_5666
Wakazi wa jijini Mwanza wakisalimana na msanii Neyo kwa shangwe na furaha waliofika kumlaki katika uwanja wandege wa jijini Mwanza.
IMG_5667
Neyo geke......(kwa lafudhi ya Kisukuma pale kati)
IMG_5662
Neyo says - "Wawoooooooooo.......its You"
Msafara katikati ya jiji la Mwanza "The Rock City"
Jembe Family wanapokutana.....ni matatizo pale kando....siri yako lakini.
IMG_5305

Msafara wa msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo ukielekea hotelini baada ya kuwasili jijini Mwanza.
Neyo at Malaika Resort

Msanii Neyo alipowasili kwenye hoteli ya Malaika Resorts ya jijini Mwanza akiwapungia wafanyakazi pamoja na wateja katika hoteli hiyo.
Justine Ndege and Neyo
Mwanasheria wa Jembe Media Group, Justine Ndege katika picha ya pamoja na Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo katika hoteli ya Malaika Resort.
Sebastian Ndege na Neyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akibadilishana mawazo na msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo anayetarajiwa kutumbuiza kesho katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 Neyo na akiwa na Meneja wa kampuni ya kusafirisha watalii Kanda ya Ziwa ya Exotic Expeditions Mr. Junaid...wakipata ufoTo na Gsengo Blog.
Me (GsengoBlog) na Mo Entertainment toka Marekani 
Wananchi hawakutaka kupitwa na jambo ......
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Neyo amewasili jijini Mwanza jioni hii akitokea Dar es Salaam na kupokelewa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji hilo kama Mfalme katika Uwanja wa Ndege wa jijini Mwanza.

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na Coca Cola.

Msanii huyo anatarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo kwa kupiga 'Live Music' katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo msanii wa kimataifa kutoka nchini, Diamond Platnumz, FID Q, Stamina, Mr. Blue, Ney wa Mitego, Maua Sama, Rubby, Baraka Da Prince, Juma Nature, MO Music na wengine wengi watapanda jukwaa moja na msanii Neyo.