ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 2, 2016

SHEHENA ZA SAMAKI ZAKAMATWA JIJINI MWANZA.


 Msako unaoendeshwa na maafisa wa uvuvi mkoani Mwanza, wa kuwakamata watu wanaojihusisha na uvuvi haramu ziwa Victoria, umefanikiwa kakamata shehena ya samaki aina ya Sangara tani tano zenye thamani ya Sh. Milioni 26.

Msako huo unakuja baada ya hivi karibuni, Waziri wa Kilimo, Mifungo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba, kuwatupia lawama maofisa wa uvuvi kanda ya ziwa kushindwa kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu.

Oparesheni hiyo inayoendeshwa katika ziwa Victoria, imekamata sangara ambao hawapaswi kuvuliwa chini ya sheria ya 22 ya mwaka 2003 inayozuia Sangara wachanga centimita 50 na centimita 85 ambao ni wazazi.

Akizungumza na Gsengo BLOG mara baada ya kukamata samaki hao, Afisa Mfawidhi wa usimamizi na uvuvi kanda ya Mwanza, Lameck Mongo, alisema samaki hao, walikamatwa katika eneo la sabasaba Kata ya Pasiansi mjini hapa.

Mongo alisema kuwa samaki hao, kilo 520 sawa na tani tani, wametaifishwa katika kiwanda kinachomilikiwa na mfanyabishara, Oswald Hakimu, anaefanya biashara ya kuchakata, kuuza na kuhifadhi samaki.
Alisema samaki centimita 50 ni samaki wachanga ambao bado wanatakiwa kukuwa ili waweze kuzaa huku wale wa centimita 85 ni samaki wakubwa wasioruhusiwa kuvuliwa wanapaswa kuendelea kuzaa.

"Tumekamata samaki wachanga kilo 4,809 na wakubwa ni kilo 410, ambao hawapaswi kuvuliwa kwa mjibu wa sheria ya 22 ya mwaka 2003 na hatutakubali kuona watu wakiendelea kuvua samaki wasioruhusiwa, "alisema Mongo.









Mongo alisema kuwa baada ya kuzitaifisha samaki hizo, watazigawa kwa taasisi za umma, ikiwemo gerezani na vituo vya watu wasiojiweza na watoto yatima baada ya kupata kibari kutoka mahakamani.

Hata hivyo, alisema pamoja na kukamata samaki hao, watamchukulia hatua za kisheria mmiliki wa kiwanda hicho, ambae hata hivyo, alikimbia baada ya kuwaona maofisa hao wa uvuvi kiwandani kwake.

NA ZEPHANIA MANDIA WA GSENGOBLOG.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.