ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 3, 2016

SHEHENA YA MBAO NA MAGOGO YANASWA TONGWE MASHARIKI.

Usiku wa kiasi cha saa 5 mwishoni mwa juma lililopita Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano akiambatana na Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mhe. Salehe Mhando walikuwa kwenye oparesheni ya kukamata utoroshaji wa mbao na magogo ktk msitu wa mbao wa Tongwe Mashariki ambapo asubuhi yake ilithibitika kukamatwa kwa shehena kubwa ya Magogo pamoja na mbao.

Mhe Salehe Mhando Mkuu Wa wilaya ya Tanganyika akiwa na Waziri Wa Nchi ofisi ya makamu Wa Rais (mazingira na muungano) akimuonyesha njia za vichochoro ambazo hutumiwa na watoroshaji wakati akiwa ziarani wilayani hapo mwishoni mwa wiki.

PSehemu ya shehena ambayo ilikuwa imefichwa porini tayari kupakiwa na kusafirishwa.
Mhe Salehe Mhando Mkuu Wa wilaya ya Tanganyika akitia msisitizo juu ya katazo la serikali na suala la ulinzi shirikishi.
Pia tumekamata malori mawili kati ya matano yaliyopo msituni. Tunaendelea kuyasaka mpaka yapatikane. Kuna ufisadi wa kutisha ktk misitu yetu.

Watu wachache waliigeuza wilaya ya Tanganyika kama shamba la bibi! Sasa kazi tu!

"Kwa tathimini ya haraka huu mzigo tulioukamata unathamani ya zaidi ya sh.Mil 123"
"Unaweza kujiuliza kwa miaka miwili mitatu nyuma ni kiasi gani cha fedha kimenufaisha Mafisadi wachache na kuwaacha watanzania wenzao wakiendelea kukosa huduma za Jamii. Hapa hakuna namna naomba tuombeane sana ktk shughuli hii nzito!"

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.