ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 17, 2016

MAMA SAMIA ATETA NA WANA UKEREWE KUEPUKA UJENZI WA NYUMBA ZISIZO NA HUDUMA ZA VYOO.

Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu akisalimiana na wananchi mara baada ya kuingia wilayani Ukerewe.
PICHA NA ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO BLOG.
Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu akipata picha na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Gerson Rwenge mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji na usafi wa mazingira wa Ziwa Victoria Mjini Nansio Ukerewe.


Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Mkoa wa Mwanza Injinia Athony Sanga akitoa ufafanuzi wa mradi wa maji wilaya ya Ukerewe mbele ya Makamu wa Rais Serikali awamu ya 5.





Ukerewe. Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan  amewataka wakazi wa mji wa Nansio  katika wilaya ya Ukerewe mkoani  hapa kuepuka ujenzi wa nyumba ambazo hazina  huduma za vyoo vya ndani.


Lengo la agizo hilo ni pamoja na kupunguza kiwango cha uchafuzi wa maji ya ziwa,kutokana na tabia ya baadhi ya wananchi kuchimba vyoo vya shimo ambavyo  alisema mara nyingi miundombinu yake siyo rafiki kwa usafi wa mazingira,hasa kandokando ya ziwa.

MamaSamia alitoa agizo hilo wakati akihutubia  mamia ya wakazi wa mji huo  kwenye  hafla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa majiisafi na usafi wa mazingira ziwa Victoria awamu ya pili ambao umetekelezwa kwa gharama ya sh10.9  bilioni.

Makamu huyo wa Rais ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mradi huo ambao umefadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika,kupitia nchi wanachama wsa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Licha ya kutumia muda mwingi wa hotuba yake kujibu mabango ya wananchi,Makamu wa Rais pia aliiagiza Wizara ya maji na umwagiliaji kushirikiana na uongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Jijini Mwanza kushirkiana na wakazi wa mji huo kulinda miundombinu ya mradi.

Vilevile,Makamu wa Rais ambaye alikuwa amefuatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Emmanuel Kalobelo pamoja na mwakilishia wa Kamisheni ya Bonde la ziwa Victoria, Dk Ally Matano aliwataka wakazi wa mji wa Nansio na vijiji jirani kutambua kwamba mradi huo ni mali yao,hivyo wana wajibu wa kulinda na kuutunza.

Akisoma taarifa mbele ya Makamu sa Rais,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Emmanuel Kalobelo alisema mradi utawanufaisha wakazi zaidi ya 80,000 wa mji wa Nansio pamoja na vijiji vya Nantare, Kakerege, Hamkoko, Bukongo, Nkilizya, Kagera, Nakatunguru, Malegea na Bulamba.

Alisema mradi huo ni miongoni mwa miradi mingine miwili inayotekelezwa kitaifa  katika miji ya Sengerema na Geita mkoani.

Kwa upande wake,mwakilishi wa Kamisheni ya Bonde la ziwa Victoria,Dk Matano aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kukamilisha mradi huo kwa wakati, na kwa kiwango cha hali ya juu ikilinganishwa na miradi mingine 12 inayotekelezwa katika nchi nyingine tano ambazo ni wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Makamu wa Rais juzi alihitimisha ziara ya siku tatu mkoani Mwanza ambapo alitembelea  na kuweka mawe ya misingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Sengerema, Misungwi, Kwimba na Magu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.