ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 4, 2016

AIRTEL YATANGAZA WASHINDI WA SHINDANO LA VIDEO BORA IJULIKANAYO KAMA “JICHO LA KITAA”

Jaji wa shindano la jicho la kitaa na mmiliki na mkurugenzi mkuu wa studio ya picha ya I-View,  Raqey Mohamed (katikati) pamoja na jaji na mtayarishaji wa video Hance  Richard (kulia) na Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde, wakiangalia filamu za  washindi wawili kabla ya kutangazwa kuwa washindi.
Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiwapongeza majaji wa shindano la Jicho la Kitaa Raqey Mohamed na Hance  Richard mara baada ya kutangaza washindi wa shindano hilo ambao ni Santos Hillary na Elly EMD

Airtel yatangaza washindi wa shindano la video bora  lijulikanalo kama “Jicho la Kitaa”

·       Washindi wawili wapatikana kila mmoja kajishindia shilingi millioni tano na nafasi ya kwenda kwenye mashindano ya kimataifa nchini Singapore

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza washindi  wawili wa shindano la Jicho la kitaa lililokuwa likiendeshwa kupitia mitandao yake ya kijamii ya faceebook na Instagram na kuwapa nafasi watanzania wenye vipaji vya kutengeneza filamu ya dakika 5 yenye maudhui ya connecting life  yaani kuunganisha jamii kushiriki na kujishindia zawadi nono.

Akitangaza washindi wa jicho la kitaa,  Jaji wa shindano hilo na mmiliki na mkurugenzi mkuu wa studio ya picha ya I-View,  Raqey Mohamed alisema “ shindano la jicho la kitaa limekuwa na ushindani mkubwa,  zaidi ya filamu fupi 120 zimetumwa na tumezipigia zote  na hatimae kupata washindi wawili .  napenda kuwapongeza sana kwa kazi zao nzuri kwa maani huu ndio mwanzo mzuri wa kuinua kazi zao na kuzifikia ndoto zao

Raque aliwataja washindi hao na kusema “ninayofuraha kutangaza washindi wetu ambao ni  Santos Hillary mwenye filamu yake ijulikanayo kama “  uliza kiatu “ na  mshindi wa pili ni  Elly EMD filamu yake inaitwa “Day by Day” nawapongeza sana washindi wetu na wote walioshiriki.”

Kwa upande wake Afisa uhusiano wa Airtel , Bi Jane Matinde alisema “ kila mshindi ataondoka na kitita cha shilingi milioni 5 pesa taslimu pamoja na kupata nafasi ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa yanayotegemea kufanyika tarehe 21 mwenzi huu nchni Singapore.

Nawashukuru vijana wenye vipaji walioshiriki katika shindano hili na kuwahasa kuendelea kuchangamkia fursa kama hizi kupitia program zetu mbalimbali kwani ndio mwanzo mzuri wa kuinua vipaji vyao na kuzifikia ndoto zao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.