ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 12, 2016

HAYA NDIYO MAAMUZI YA MZEE YUSUF.

Gwiji wa mziki wa taarabu nchini Mzee Yusuf amethibitisha kuwa ameachana na kazi hiyo takribani miezi miwili iliyopita.

Taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii zimeeleza kuwa mwanamziki huyo ameachana na mziki na kuamua kumrudia Mungu.

Akizungumza na Mwananchi Digital kwa njia ya simu usiku huu, mmiliki huyo wa bendi ya Jahazi Modern Taarab amethibitisha kuwa taarifa hizo ni kweli na kuongeza:

“Nashangaa taarifa hizi zinasemwa leo. Ni suala la muda mrefu….takribani miezi miwili iliyopita na sababu ni kuwa nimeamua kumrudia Allah,”

Mwanamziki huyo mzaliwa wa Zanzibar alipoulizwa kuwa ni suala gani lililomsukuma hata achukue maamuzi hayo magumu, alijibu kwa kifupi, “ndivyo tunavyofundishwa na viongozi wa dini.”

Yusuph aliyetamba na vibwagizo kama “Nichumu, nikisi….mwaaaa,” katika baadhi ya nyimbo zake, amesema familia yake imeupokea uamuzi wake kwa mtazamo chanya na kwamba inamuunga mkono.

“Kwa sasa nitaimba kaswida zenye mafundisho ya dini,” amesema nyota huo huku akiahidi kufanya mkutano rasmi kuelezea suala hilo.

Mfalme huyo aliyeonekana kuwa ni gwiji wa taarabu ya kisasa (modern taarab) amezaliwa visiwani Zanzibar mwaka 1977. Aidha amejihusisha na sanaa nyingine kama maigizo.

Ni mshindi wa tuzo katika tasnia ya muziki wa taarab zikiwemo ya Kilimanjaro Music award 2014-15.

Mpambano wa tuzo za Kili ulivyokuwa msimu wa 2014-15

1. Kikundi bora cha mwaka taarab - Jahazi Modern Taarab

2. Mtayarishaji bora wa mwaka bendi - Enrico

3. Mtunzi bora wa mwaka taarab- Mzee yussuf

4. Mwimbaji bora wa kiume taarab - Mzee Yussuf

5. Mwimbaji bora wa kike taarab - Isha Mashauzi

6. Wimbo bora wa taarab (mapenzi hayana dhamana)- Isha Mashauzi

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.