ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 6, 2016

MAJAMBAZI YATIKISA TENA KATA YA KISHIRI/IGOMA JIJI LA MWANZA, YAPORA MADUKA MAWILI NA KIBANDA CHA M-PESA YAMJERUHI MMILIKI WAKE KWA RISASI AJIJARIBU KUYATOROKA.


NA MWANDISHI WETU, MWANZA.

JIJI la Mwanza lazidi kutikiswa na majambazi ambapo safari hii ilikuwa ni maeneo ya Kata ya Kishiri zamani Igoma ambapo walivamia na kupora fedha huku wakibuni stahili mpya ya kuimba wimbo “tumekuja kuchukua pesa zetu hatutaki kuuwa” hali iliyoleta wasiwasi kwa wananchi jijini Mwanza.
 
Tukio hilo lilitokea siku ya Alhamis Mei 6 majira ya kati ya saa 3 hadi 4 usiku ambapo watu wanaodhaniwa majambazi wakiwa na silaha za moto waliweza kuzingila kwa muda eneo la Kishiri kwenye maduka zinapogeuzia dalalala na kufanya uporaji wa fedha kutoka katika maduka mawili ya bidhaa mbalimbali na kisha kuhamia kibanda cha jirani cha M-Pesa.
 
Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo huku wakiomba majina yao kutotajwa walieleza kwamba majambazi hao wakiwa wamevalia makoti marefu na kufunika nyuso zao yakitumia silaha walivamia maduka mawili na kuamuru kupatiwa fedha bila ubishi kwa kuwa lengo lao ni fedha si kuuwa .
 
“Waliku na wimbo wao walioimba “tumekuja, tumekuja kuchukuua fedha zetu hatutaki kuuwa towa pesa” huku baadhi wakitoa bunduki na kuwatishia wamiliki na wauzaji kuwapatia pesa bila kufanya ubishi na baada ya kupora waliondoka katika maduka hayo na kuelekea eneo ambalo kulikuwa na kibanda cha mihamala ya fedha cha M-Pesa huku yakifyatua risasi hewani kutishia wananchi,”alieleza mmoja wa mashuhuda. 
 
Alieleza kwamba baada ya kukaribia kibanda cha M-Pesa huku aliyekuwa ndani ya kibanda hicho akiwa tayari amefunga baada ya kusikia mlio wa risasi kwa majirani zake wa maduka ya alihisi hali si shwari na kufunga haraka ili kuondoka katika eneo hilo ambalo tayari hata hivyo lilikuwa limeisha zingilwa na watu hao waliokuwa wakiimba na kufyatua risasi hewani.
 
“Ilikuwa kama sinema hivi na baadhi hawakujua kinachoendelea na wananchi wengine walianza kukimbia baada ya kusikika milio ya risasi haku mmiliki wa kibanda cha M-Pesa akiamuliwa kusimama na majambazi hayo akijaribu kukimbia kutoroka lakini yalifanikiwa kumpiga rirasi ya muguni na kumjeruhi vibaya,”alisema. 

Aliongeza kuwa watu hao ambao ni majambazi walionyesha dhalau kubwa kwa kufanya uhalifu huo huku wakiimba nyimbo mithili ya kutokuwepo vyombo vya ulinzi na usalama na kusababisha wananchi wengi kuwa na hofu ya usalama wa maisha yao pamoja na mali zao kutokana na watu hao kufanya matukio mapema na kuondoka bila hata Polisi kufika pamoja na taarifa kutolewa na wananchi juu ya matukio yanapotokea hata kusikia kuwa wamekamatwa baada ya kutokea matukio ya uhalifu jambo ambalo wananchi wameanza kuhoji kazi ya Polisi nini kwa sasa?.

 
Kufatia tukio hilo ikiwa ni siku chache tangu kutokea tukio jingine la ujambazi katika eneo la Ibungilo Wilaya ya Ilemela ambapo watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa na silaha walivamia duka la kufanya mihamala ya fedha (M-Pesa) na wakala wa benki ya CRDB na kumuua mmiliki wake huku watu wengine watatu wakijeruhiwa kwa risasi.
 
GSENGO BLOG ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC), Hemerd Msangi, kwa njia ya simu ya mkononi haikuwa hewani na kuamua kumtafuta Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO), Augustine Senga naye simu yake ya mkononi haikupatikana ili kuweza kutoa taarifa za tukio hilo na hali ya ulinzi na usalama kwa wananchi na mali zao kuwa shakani.
 
Kwa upande wake alipotafutwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kwenye simu yake ya mkononi majira ya saa 9:30 alasiri alipokea na kuomba apigiwe tena badae kwa kuwa alikuwa kwenye kikao ambacho yeye ndiyo alikuwa akikiendesha kwa wakati huo na kushindwa kupata kauli ya viongozi hao juu ya tukio hilo ambalo kwa linadaiwa kuwa la kumi nne kutokea kwa muda wa kuanzia Januari hadi Mei mwaka huu.
 
Huku baadhi ya wananchi wakiomba serikali ya Mkoa kupitia kwa RC Mongella kuubana Uongozi wa Polisi Mkoa na Wilaya zake kuhakikisha wanawasaka watu hao wanaoendesha uporaji wa mali, fedha na kuuwa pamoja na kuwajeruhi kwa risasi watu wengine ili kukomesha mitandao hiyo mkoani Mwanza ambayo imeshika kasi kwa sasa.
 
Imedaiwa kwa yapo makundi ya mitandao mitano kati ya saba ambayo kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (Mbunge-Misungwi) kueleza hivi karibuni katika matukio ya ujambazi jijini Mwanza Polisi ilibai kuwepo mtandao wa makundi saba ya uhalifu ambapo mawili kati yao yalikuwa tayari yamesambaratishwa huku Polisi ikihangaika kuyasaka makundi matano ya uhalifu.
 
Baadhi ya wananchi wamedai kuwa pengine kuendelea kwa matukio ya uhalifu wa kutumia silaha ni dalili tosha kuwa makundi matano bado hayajabainika, huku wakitaka juhudi zaidi ziongezwe na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi watakaoweza kutoa taarifa za siri ili kuwezesha kukamatwa watu walio ndani ya makundi hayo wakiwemo wamiliki wake na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, na wengine wakitaka Jeshi hilo kuwafatilia nyendo za watu walioachiwa huru kutoka katika Magereza mbalimbali hivi karibuni kwa msamaha wa Rais Dk John Magufuli, alioutoa kuazimisha sherehe za Muungano wa tanzania na Zanzibar.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.