ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 27, 2016

ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIRUSHA TOKA JUU YA MNARA KISA SUKARI.

Kijana Mmoja Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka juu ya mnara wa simu wenye urefu wa takribani mita 30. 

Tukio hilo limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo ambae alipanda katika mnara huo tangu majira ya alfajiri na kukataa kata kata kushuka toka juu ya mnara huo hadi ilipofika majira ya saa sita mchana baada ya kughasiwa vya kutosha na kuamua kujirusha.

Jamaa huyo ambaye alikuwa akisikika kulaumu ugumu wa maisha pia kwenye kauli zake aliligusia suala la kupanda bei na kuadimika kwa sukari akimtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufika mahala hapo kabla ajafanya maamuzi mabaya ya kujiachia.



Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, ametoa rai kwa makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika maeneo yote yanayozunguka minara yao ili kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa, ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa ikimuongezea morari kijana huyo na hivyo kufanya kweli.

Baada ya kijana huyo kujirusha chini, alipoteza fahamu huku baadhi ya maeneo ya mwili wake yakitoka damu kiasi na kukimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure kwa ajili ya huduma ya zaidi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.