ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 28, 2016

GSM FOUNDATION NA MOI WAANZA KAMBI ZA UPASUAJI BUGANDO.

 Na Mwandishi Wetu
Jumla ya watoto 120 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza, kufuatia tatizo la kichwa kikubwa walilozaliwa nalo chini ya udhamini wa taasisi ya GSM ambayo imedhamini zoezi hilo litakalofanyika katika mikoa mitano ikiwa ni awamu ya kwanza kati ya nne zinazotarajiwa kufanyika tanzania nzima. 

Akiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi wa zoezi hilo linalojumuisha madaktari Bingwa 10 kutoka Taasisi ya mifupa na Upasuaji MOI, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Profesa Kien Mteta aliishukuru taasisi ya GSM kwa kuamua kulichukua tatizo hilo ambalo ameliita kuwa ni kubwa ukilinganisha na jinsi linavyochukuliwa na jamii ya watanzania.

Dk Kien aliwaambia wanahabari kwamba jumla ya watoto 2000 huzaliwa na vichwa vikubwa katika kanda ya Ziwa peke yake, na mtaalamu wa kuhudumia wagonjwa wa namna hii ni mmoja tu ambapo pia kwa Tanzania nzima, wataalamu wa upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa wako tisa tu.

Cha kusikitisha ni kwamba kati ya hao, ni wachache sana hurudi kwa ajili ya matibabu bali wengi wao hufariki kwa kufichwa ndani na wazazi wao aidha kwa imani za kishirikina ama kushindwa kwa wazazi kumudu gharama za matibabu.

PICHANI JUU: Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Profesa Kien Mteta(kushoto) akiongea na wanahabari huku akisikilizwa kwa umakini na Halfan Kiwamba(kulia) na Mkurugenzi wa taasisi ya Mifupa na upasuaji Dk Othman Kiloloma(katikati)

 Mtaalamu wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya Fahamu, Dk Gerald Mayaya akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kuhusiana na kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa katika Hospitali ya Bugando
 Meneja Mkuu wa taasisi ya GSM, Shannon Kiwamba (katikati) akiongea na wanahabari kuhusiana na sera yao mpya ya kusaidia watanzania katika masuala ya elimu na Afya, kulia kwake ni Mkuu wa Hospitali ya Bingando, Prof Kien Mtena na kushoto kwake ni Mkuu wa mawasiliano wa Taasisi ya GSM, Halfan Kiwamba
 maelezo ya ufafanuzi yakiendelea kutolewa na Halfan Kiwamba(Wa pili kutoka kushoto) kutoka GSM Foundation
 Mkuu wa kitenngo cha Upasuaji na Mifupa ambaye ndio mratibu wa kambi ya tiba ya watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi akifafanua jambo kwa wanahabari(hawapo pichani)
 Baadhi ya wahudumu wanaoshiriki kambi ya watoto wenye vichwa vikubwa wakisikiliza viongozi wao wakatiwakiongea na wanahabari
 Wanahabari kazini

 Ufafanuzi ukiendelea...
 Picha ya pamoja ya wawezeshaji wa zoezi la kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi 
 Mkuu wa Hospitali ya Bingando, Prof Kien Mtena (kulia) katika picha ya pamoja na mwanahabari wa Jembe Fm Mwanza G. Sengo.
Taarifa kwa umma kupitia mabango ya Hospitali ya Rufaa Bugando. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.