ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 18, 2016

LIVERPOOL YAITUPA NJE MAN UNITED ULAYA

LIVERPOOL imekwenda Robo Fainali ya michuano ya UEFA Europa League baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, Manchester United usiku wa Alhamisi Uwanja wa Old Trafford.Manchester United walitangulia kwao bao la kwaju wa penalti la Anthony Martial dakika ya 32, kabla ya Philippe Coutinho kuisawazishia Liverpool dakika ya 45.

Liverpool inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya awali kushinda 1-0 wiki iliyopita Uwanja wa Anfield.  


Tottenham Hotspur nayo imeaga michuano hiyo baada ya kufungwa 2-1 na Borussia Dortmund Uwanja wa White Hart Lane, London. Mabao yote ya Dortmund yamefungwa na Mwanasoka Bora wa Afrika, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 24 na 70, wakati la Spurs limefungwa na Heung-Min Son dakika ya 73.


Dortmund inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-1, baada ya wiki iliyopita kushinda 3-0 Ujerumani. 


Sevilla imeifunga 3-0 FC Basel, mabao ya Adil Rami na Kevin Gameiro mawili Uwanja wa Ramon-Sanchez Pizjuan, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-0 baada ya awali kutoa sare ya 0-0 ugenini.


Shakhtar Donetsk imeshinda ugenini 1-0 dhidi ya RSC Anderlecht, bao pekee la Eduardo Alves da Silva dakika za majeruhi Uwanja wa Constant Vanden Stockstadion, hivyo inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1 baada ya awali kushinda 3-0 nyumbani.

Sporting Braga imeifunga 4-1 Fenerbahce, mabao ya Ahmed Hassan, Josue Filipe Soares Pesqueira,  Nikola Stojiljkovic na Rafael Alexandre Fernandes Ferreira Silva, huku la wageni likifungwa na Alper Potuk Uwanja wa Estadio Municipal de Braga.

Valencia CF imeshinda 2-1 dhidi ya Athletic Club, mabao yake yakifungwa na Santiago Mina Lorenzo na Aritz Aduriz Zubeldia Uwanja wa Mestalla. Lakini ni Athletic Club, inayosonga mbele kwa faida ya bao la ugenini baada ya sare ya jumla ya 2-2, kufuaia kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza.


Sparta Prague imelazimishwa sare ya 0-0 na Dully Sukes, wakati Bayer 04 Leverkusen imelazimishwa sare ya 0-0 na Villarreal BayArena




Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.