ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 30, 2016

BODI YA SHULE YA PAMBA YAVUNJWA.



Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo amevunja bodi ya shule ya sekondari Pamba iliyopo jijini Mwanza na kumvua madaraka mkuu wa shule hiyo Aidan Dotopery pamoja na walimu wengine wawili kutokana na kushindwa kusimamia vyema matumizi ya fedha na mali za shule zao. 

Walimu wengine waliovuliwa nyadhifa zao na mkuu huyo wa mkoa ni pamoja na mkuu wa shule ya sekondari Nyakurunduma January Luganyika na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyamagana Masau Mtakilolwa. 

 Hatua hiyo imechukuliwa baada ya mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza kufanya ziara katika shule hizo na kuonyesha kutoridhishwa na mazingira ya uwekezaji kwenye vitega uchumi vya shule ya sekondari ya Pamba, huku baadhi ya nyaraka pamoja na mikataba ambayo shule hiyo imefunga na wafanyabiashara hao ikiwa imegubikwa na utata.

Moja kati ya masuala yaliyochomoza kwenye kikao kilichofanyika shuleni hapo hata hatua ya yaivunja bodi ya shule ni madai ya tuhuma za kuingiza shule katika mkataba tata wa ujenzi wa maduka 65....CHEKI VIDEO HAPO JUU.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.