ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 26, 2015

MKUU WA MAJESHI CDF JENERALI DAVIS MWAMUNYANGE YU BUHERI WA AFYA NA YUPO NCHINI ITALIA KIKAZI

 Taarifa zinazosambaa kumhusu Mkuu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) Jenerali  Davis Mwamunyange zilizosambaa kwenye mitandao ya jamii kwamba amekula chakula chenye sumu na amekimbizwa jijini Nairobi nchini Kenya kwa matibabu hazina ukweli wowote.Ni uzushi.

Kwa mujibu wa taarifa za familia ya Jenerali Mwamunyange pamoja na makao makuu ya jeshi ambazo Globu ya Jamii imezisaka na kuzipata, kiongozi huyu wa JWTZ hivi sasa yupo nchini Italia kwa ziara ya kikazi ya siku tisa kama anavyoonekana pichani na hajambo kabisa na yu bukheri wa afya.


Hii ni changamoto kwa wakala wa mawasiliano nchini (TCRA) ambayo imekuwa ikilaumiwa kwa ukimya wake wa kutochukua hatua thabiti kuthibiti uongo kama huu kwa kuwatafiti, kuwabaini na kuwachukulia hatua watu kama hawa wenye nia ya kuleta taharuki na machafuko nchini.

Wananchi wengie waliohojiwa na Globu ya Jamii wanahoji endapo kama kweli TCRA ipo na kama ipo ina vifaa vya kisasa iliyodai wanavyo kuwabaini watu kama hawa, na kwa nini hawajafanya kweli toka sheria ya mitandao (Cyber Law) iliyoanza kutumika.

"Endapo kama TCRA watashindwa kumnasa mhusika wa uongo huu wa kuogofya, inabidi mamlaka husika iangalie upya ajira ya watendaji wake maana kama taasisi nyeti kama JWTZ inaguswa na wao wakae kimya tu basi ujue kuna tatizo ambalo inapaswa Serikali ilifanyie kazi", amesema msomaji mmoja wa Globu ya Jamii katika maoni yake.

Friday, September 25, 2015

Dr. NGELELA (CHADEMA) AKILI KUSHINDWA NA CCM JIMBO LA ULYANKULU PAMKA WAGOMBEA WANGEUNGANA IKIWEMO ACT-Wazalendo

Na PETER FABIAN, KALIUA.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo jipya la Uchaguzi la Ulyankulu kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr Deus Ngelela amewaomba wananchi wa jimbo hilo kufanya mabadiliko kwa kuchaguwa wagombea vyama vinavyounda UKAWA ili kuwatetea na kuwaletea maendeleo.

Dr Ngelela akizungumza na wananchi katika moja ya Kata ya Kona nne jimboni humo, aliwaeleza wananchi kwamba muda wa kufanya mabadiliko ni mwaka huu na wakishindwa kufanya uamuzi wa kukiondoa madarakani Chama Cha Mapinduzi basi watambue awataweza tena kufanya hivyo na itwachukua miaka mingine 20 ijayo kupata mgombea Urais kama Lowassa na ubunge.

“Nawaombeni mumuchague mgombea wa CHADEMA kwa nafasi ya Urais Edward Lowassa ili awaletee maendeleo ya kweli na mimi mnichague kuwa Mbunge wenu lakini pia msisahau kuwachagua madiwani wetu tufanye mbadiliko ya maendeleo na si CCM iliyoshindwa,”alisema.

Katika mukutano huo ambao ulihudhuriwa na wananchi wachache kutokana na mwamuko mdogo wa wananchi wa maeneo hayo wengi wao kutoka maeneo mbalimbali ya miji ya Tabora, Kaliua, Mpanda, Kahama na Ulyankulu kujishughulisha na biashara, kilimo na ufugaji.

Dr Ngelela akijinadi na kuomba kura kwa wananchi hao aliwashangaza na kuibuwa kicheko pale aliposema anawania Ubunge lakini anajua atashindwa na John Kadutu (CCM) kutokana na Chama chake kuwa na ujanja na mbinu ya kuiba kura zenu mtakazonipigia katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu.

“Nijipe Moyo lakini natambua kuwa huyo Kadutu atanishinda lazima nikiri anaonekana kujiamini kunishinda lakini niwaombe msikate tamaa jitokezeni kunipigia kura mimi na Lowassa kwani Dr Ngelela niko kama mbwa wenu mnayemfungia mchana na usiku mnamwachia kuwalinda awalinde hivyo komaeno makamanda inawezekana kikaeleweka na tukachukua jimbo hili CHADEMA,”alisisitiza.

Alisema kwamba wapo mgombea wengine mbali na Kadutu wa CCM pia mgombea mwingine ni Kayoka Nicholaus (ACT-Wazalendo) ambaye ametuharibia kwa kung’ang’ania kugombea na kusababisha mvutano wetu na huenda tukazigawana kura zetu jambo ambalo litampa mtelemuko Katudu kutushinda kilahisi ni vyema wangekubali kuniunga mkono mimi ili nimshinde kutoka na kukubalika kwa wananchi kuliko Nicholaus.

Baada ya mkutano huo uliozua mijadara ya hapa na pale kwa wananchi wa Kata ya Kona nne kuzua mabishano na kumjadili mgombea huyo huku baadhi yao wakiwa katika vikundi tofauti kudai kwamba Dr Ngelela ameshindwa kujikita kwenye sera, kutoa ahadi na kujenga ushawishi kwao ili kumchagua zaidi ya kumsema Kadutu na Nicholaus.

MKANYAGANO WASABABISHA VIFO MAKKA

Katika hali ya kusikitisha mahujaji zaidi ya 500 wafariki dunia nchini Saudi Arabia kufuatia mkanyagano wakati wa ibada ya Hija.

UKAWA WAKWEPA MDAHALO WA WAGOMBEA URAIS

Uongozi wa Ukawa wakataa kushiriki mdahalo wa wagombea uraisi huku ukisisitiza hauna mda kwa sasa.

SERIKALI YA CCM YAAHIDI UMEME VIJIJI VYOTE TANZANIA NDANI YA MIAKA MI 2 MADARAKANI.


Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Kilindi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mkoa wa Tanga. Miongoni mwa ahadi aliyoitoa kwa wanaKilindi ni kulishughulikia suala la upatikanaji wa huduma za maji safi na salama pamoja na ujenzi wa barabara ya kuingia na kutoka katika Wilaya hiyo.

Baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM Kijiji cha Kwediboma wakiwa wamesimamisha msafara wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan kuwasikiliza kilio chao alipokuwa akisafiri kuelekea Wilaya ya Kiteto. Baadhi ya ahadi aliyoitoa Bi. Samia ni pamoja na upimaji wa ardhi ya vijiji na wilaya ili kumaliza migogoro ya ardhi kwa wafugaji na wakulima.  
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga akizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano mdogo wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Kilindi, Tanga.
Mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Chemba, Juma Nkamia akizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa chama hicho, Bi. Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Chemba. Miongoni mwa ahadi kwa wakazi wa eneo hilo alizozitoa ni kushughulikia migogoro ya ardhi suala la ukame na huduma za maji.
Kutoka kulia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Kilindi, Mboni Muhita akiserebuka na baadhi ya viongozi na makada wa CCM walioongozana kwenye kampeni za mgombea mwenza Wilaya ya Kilindi.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimtambulisha mgombea ubunge wa Jimbo la Kilindi, Mboni Muhita kwa wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Kilindi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mkoa wa Tanga.

Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akionesha nakala ya ilani ya chama hicho kwa wananchi kabla ya kumkabidhi, mgombea ubunge wa Jimbo la Kilindi, Mboni Muhita kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mkoa wa Tanga.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kilindi, Mboni Muhita akionesha kwa wananchi nakala ya ilani ya uchaguzi ya chama hicho mara baada ya kukabidhiwa na mgombea mwenza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mkoa wa Tanga.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akimtambulisha mmoja wa wagombea wa udiwani CCM katika mkutano wa hadhara Jimbo la Kilindi.
Baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM Kijiji cha Kwediboma wakiwa wamesimamisha msafara wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan kuwasikiliza kilio chao alipokuwa akisafiri kuelekea Wilaya ya Kiteto. 
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM Taifa, Ummy Mwalimu (kushoto) na Mahadhi Juma wakijadili jambo kwenye moja ya mikutano ya kampeni ya mgombea mwenza. 

Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa hadhara Jimbo la Kilindi kunadi ilani ya CCM.
Baadhi ya wananchi wakiwa wamesimama juu ya kisiki kuweza kumshuhudia mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwasili Jimbo la Kilindi.
Baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM Kijiji cha Kwediboma wakiwa wamesimamisha msafara wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan kuwasikiliza kilio chao alipokuwa akisafiri kuelekea Wilaya ya Kiteto. 
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu kwa heshima na vijana wa UVCCM mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Kiteto ambapo alifanya mikutano ya kampeni kunadi ilani ya CCM. 
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika ofisi za CCM Wilaya ya Kiteto kabla ya kuanzamikutano ya kampeni kunadi ilani ya CCM. 
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Kiteto kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mkoa wa Manyara. Katika ahadi zake alisema ndani ya miaka miwili baada ya kuingia madarakani watahakikisha umeme unawaka katika vijiji vyote vya Tanzania.
Mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian John (kushoto) akitambulishwa kwa wananchi na WanaCCM na Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan.
Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Chemba, Wilaya ya Chemba.
Mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Chemba, Juma Nkamia akizungumza na mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jimboni humo.
Mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Chemba, Juma Nkamia (kulia) akizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa chama hicho, Bi. Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Chemba. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwenye mkutano wa hadhara Jimbo la Chemba.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Chemba kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Wilaya ya Chemba. Picha zote na www.thehabari.com.

CHANGAMOTO ZA JIMBO LA ULYANKULU WANANCHI WATAKA MBUNGE AJAYE AZIMALIZE

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ulyankulu wilayani Kailiua mkoani Tabora akiomba kura ili kumaliza changamoto ya maji safi, barabara, umeme, elimu na afya zinazolikabili jimbo hilo wakati wa mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika Kata ya Kashishi mpakani mwa Mji wa Kahama mkoani Shinyanga na jimbo hilo jana Picha Na Peter Fabian.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ulyankulu wilayani Kailiua mkoani Tabora akiomba kura ili kumaliza changamoto ya maji safi, barabara, umeme, elimu na afya zinazolikabili jimbo hilo wakati wa mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika Kata ya Kashishi mpakani mwa Mji wa Kahama mkoani Shinyanga na jimbo hilo jana Picha Na Peter Fabian.

NA PETER FABIAN, ULYANKULU.

WANANCHI wa Jimbo jipya la Ulyankulu Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora wametakiwa kuvumilia hadi kumalizika kwa uchaguzi ili Mbunge watakayemchagua John Kadutu wa Chama Cha Mapinduzi aweze kuanza kazi ya kuibana serikali juu ya kero na matatizo yanayolikabili jimbo hilo kwa sasa.

Kauli hiyo imetolewa jana na Kadutu (CCM) anayewania kuchagulilwa na wananchi mwezi Oktoba mwaka huu ili awe Mbunge wa Jimbo hilo atakayetekeleza wajibu wake kwa vitendo katika kuwaletea maendeleo wananchi, alipofanya mikutano ya kampeni kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Kata ya Kashishi iliyoko mpakani na Mji wa Kahama (Shinyanga) kwa na lengo la kujinadi na kuomba kura.


Kadutu aliwaeleza wananchi hao kwamba baada ya serikali kukubali kuligawanya jimbo la Urambo Magharibi na kuzaliwa majimbo mawili la Kaliua na Ulyankulu kutasaidia kufikisha huduma za kijamii na maendeleo haraka kwa serikali ya awamu ya tano kuwapatia Wilaya na Halmashauri, lakini pia wakimchagua atapigania uboreshaji wa miundombinu ambayo ni kero kubwa.

“Barabara hazipo na zilizopo hazina ubora katika maeneo mbalimbali kutokana na kutopitika kilahisi, jingine ntakalo lisimamia kuomba serikali itusaidie kwa haraka ni miundombinu ya shule za msingi na sekondari kukabiliwa na changamoto ya upungufu mkubwa wa majengo na nyumba za walimu ikiwemo vyoo kutokuwepo na kupelekea wanafunzi kujisaidia kwenye machaka,”alisema.

Aidha alisema kwamba changamoto nyingine atakayoisumbua serikali akiwa Mbunge ni jimbo hilo kutokuwa Hospitali ya Wilaya kutokana na iliyopo kubaki jimbo la Kaliua, kupigania serikali iendelee kumbana Mkandarasi wa usambazaji umeme vijijini kutoka Grid ya Taifa kwenye maeneo yote ya vijijini ambapo kwa sasa sehemu kubwa wananchi wanatumia umeme wa Nishati ya  jua (Sorla).

“Kata hii ipo jirani na Mji wa Kahama ambapo ni kilomita 80 mkinichagua tu mtanisikia nikimbana Rais na Waziri wa Wizara ya  Maji ili tupate mradi mkubwa wa maji safi kutokea Ziwa Victoria yaliyokwisha fika Mji wa Kahama yafike hadi Ulyankulu kabla ya kuanza kupeleka Mjini Tabora (zaidi kilomita 200),  Mji wa Nzega na Igunga ili kuondoa kero hii,”alisisitiza.

Kadutu aliwahidi wananchi hao kuibana Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika juu ya makato ya fedha za ruzuku ya zao la Tumbaku ili kuwezesha kujiunga na Mfuko wa Bima  ya Afya pamoja na kucheleweshwa kwa fedha za wakulima pamoja na fedha za ruzuku ya serikali ya vijiji na kusababisha kuwepo malalamiko ya wakulima kwa Makampuni ya ununuzi wa zao hilo.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ulyankulu wilayani Kaliua mkoani Tabora, John Kadutu (kulia) akimkabizi Ilani ya Uchaguzi mgombea Udiwani wa Kata ya Kashishi  Silas Masanja (kushoto) mbele ya wananchi na kuomba wamchague ili kurahishisha utakelezaji wake na kumshirikisha katika kumaliza kero na changamoto zinazoikabili Kata hiyo na Jimbo hilo kwa ujumla kwenye mkutano wa kampeni jana Picha Na Peter Fabian.
“Kwa hili wakulima nitapambana kuhakikisha mnalipwa masilahi ya jasho lenu pamoja na kuhakikisha makubaliano ya fedha za makato ili Halmashauri itekeleze kuwaingiza kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya muweze kupata matibabu ikiwemo wazee kupata huduma hiyo bure na wanawake wakati wa kujifungua, lakini pia muweze kunufaika na kukomesha makampuni kuwatapeli wakulima,”alisisitiza.

Kadutu aliwaomba wananchi wamchague mgombea Dk John Magufuli kuwa Rais wa awamu ya tano, yeye pamoja na Madiwani wanaotokana na CCM ili kuyatekeleza yaliyopo kwenye Ilani ya uchaguzi aliyowaahidi huku akiwahasa wananchi kutokubali kudanganywa na wagombea wa vyama vya upinzani kwani wengi wao hawana dhamira njema ya kuwatumikia bali kuwagawa na kuwabagua kwa manufaa yao binafsi.

Thursday, September 24, 2015

AIRTEL YAZINDUA KIFURUSHI CHA 'YATOSHA NYTs'

Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (kulia) na Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki wakionyesha bango kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kama ishara ya kuzindua huduma mpya ya kifurushi cha ‘Yatosha Nyts’ itakayomwezesha mteja kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo pamoja na kupata kifurushi cha internet cha MB 10 kwa kiwango cha shilingi 300 tu. 


Airtel yazindua kifurushi cha “Yatosha Nyts” bila kikomo · 

Wateja kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi bila kikomo· Piga simu bure kila siku kuanzia saa 5 usiku mpaka 12 asubuhi ·

 Kwa shilingi 300 tu. Dar es Salaam,Jumatano 23 Septemba 2015, Kampuni ya simu za mikononi Airtel imewapa sababu nyingine wateja wake kufurahia usiku kwa kuwapatia “Yatosha Nyts” ofa inayowawezesha kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo,pamoja na kifurushi cha internet cha MB 10 kwa kiwango cha shilingi 300 tu.

Ofa hii ya “Yatosha Nyts” inawawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) kwenda mitandao yote kila siku kuanzia saa 5 usiku hadi saa 12 asubuhi hadi siku za wikiendi.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde alisema, “ Tunatambua wateja wetu wanamahitaji tofauti ya huduma za simu. “Yatosha Nyts” ni ofa kabambe na ya kipekee inayo kidhi mahitaji ya wateja wetu. Tumezindua “Yatosha Nyts” ofa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja wetu ya kuwasiliana na kupanga shughuli za siku inayofuata bila hofu ya kupungukiwa na salio kwenye simu zao.

 “Yatosha Nyts” inawawezesha wateja kuwasiliana na familia, marafiki , mpenzi na wafanya biashara wenzake wakati wa usiku kwa bei nafuu zaidi.

Aliongeza kwa kusema, “ikiwa ni mwendelezo wa kutoa huduma za mawasiliano bora zenye gharama nafuu, wateja wetu wanauwezo wa kununua kifurushi cha “Yatosha Nyts” wakati wowote na kuanza kufurahia kupiga simu, kutuma SMS bila kikomo na 10MB za kuperuzi.

Kwa shilingi 300 tu wateja wetu nchi nzima wanaweza kupiga simu bila kikomo Airtel kwenda Airtel , kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo kwenda mitandao yote na 10 MB za kuperuzi katika mitandao ya jamii kila usiku. Kujiunga na “Yatosha Nyts” piga *149*99#, “Yatosha Nyt” ni offa mpya na moja kati ya ofa nyingi zenye ubora ambazo Airtel inawatapia wateja wake chini ya huduma ya kibunifu ya Airtel Yatosha.

Airtel Yatosha inawapatia wateja wetu uhuru wa kununua kifurushi kinachowafaa kupitia huduma ya Airtel Money au kwa kutembelea sehemu za kutoa huduma.

Yatosha pia inawawezesha wateja kutengeneza kifurushi wanachokipenda, huduma ya kibunifu na ya kwanza kutoka Airtel

HAPPY BIRTHDAY BLOGGER FAUSTINE RUTA


Napenda kumshukuru Mungu kwa kunifikisha leo hii Sept. 24, siku yangu ya kuzaliwa. Hakika Mungu ni mwema kwa kila jambo, Pia napenda kuishukukuru familia yangu, ndugu jamaa na marafiki.

Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuishuhudia siku hii. Ni neema kubwa, Napaswa kutambua kwamba kila siku katika maisha yangu ni dhamana niitumie kwa mambo mema.

Napenda kuchukua fursa hii pia kuwashukuru wale wote ambao kwa namna moja au nyingine wameshiriki kunisapoti kwa mambo mbalimbali ili mradi nifikie pale ambapo waliamini ni sehemu bora zaidi katika maisha yangu mpaka sasa. Niwashukuru MABLOGGER wenzangu kwa ushirikiano tulionao.


MAGUFULI APIGWA NA BUTWAA NYOMI LA GEITA, AAHIDI KUSHUGHULIKIA MATATIZO YA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wake wa kampeni  uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Kalangalala mjini Geita leo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Mgombea Urais Huyo amewaambia wananchi wa Geita kuwa mara atakapoingia Ikulu, moja ya changamoto anazotarajiwa kuzipa kipaumbele ni pamoja na suala la kutatua mgogoro wa wachimbaji madini wadogo wadogo.

Magufuli ameasema kuwa akiingia madarakani atawapa maeneo wachimbaji wadogo wa madini nchini ikiwa ni pamoja na kuwakopesha mitaji na kuwapa vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi zao pamoja na mafunzo kwa ajili ya  kuboresha uchimabaji wao ili uwe wa kisasa zaidi na kupandisha  kiwango cha  ufanisi wa kazi zao za uchimbaji.

Dkt. Magufuli leo amehutubia mikutano katika miji ya Runzewe wilayani Bukombe, Katoro wilayani Chato na Geita mjini akiendelea na kampeni zake za kwaomba wananchi kumpa kura za ndiyo ili aweze kuingia Ikulu na kuwafanyia kazi Watanzania kama kiongozi na Amiri Jeshi mkuu wa Tanzania. 
 Sehemu ya umati wa wakazi wa Geita na vitongoji vyake wakiwe kwenye mkutano wa kampeni wa Dkt John Pombe Magufuli uliofanyika jioni ya leo mjini humo. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-GEITA
Wananchi wa mji wa Geita na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Kalangalala,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kumwaga sera zake mbele za wananchi hao ikiwemo pia na kuwaomba ridhaa ya kuwa Rais kwa kushinda kura nyingi ifikapo Oktoba 25 mwaka huu,ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika

 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwandani Wagombea Ubunge wa jimbo la Busanda Mh.Lolensia Bukwimba na Dkt Meedad wa Chato mapema mchana huu alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita, kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,katika mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.Dkt Magufuli atahutubia jioni ya leo mjini Geita kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita mapema leo mchana kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.
Wananchi wa Runzewe wilaya ya Mbongwe mkoani Geita wakimsikiliza kwa makini Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akizinadi sera zake na kuwaomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano,kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,katika mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria. 
 Wananchi wa Runzewe wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa kampeni
 Wananchi wa Runzewe wakimshangilia Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba kurra za ushindi ili aweze kuwa Rais wa Tanzania katika awamu ya tano
 Wakiwa na mabango yao wakishangilia ujio wa Magufuli
 Wananchi wa Runzewe wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba kurra za ushindi ili aweze kuwa Rais wa Tanzania katika awamu ya tano.
Magufuli Style ilitikisa pia ndani ya Geita kwenye mkutano wa kampeni wa Dkt John Pombe Magufuli jioni ya leo????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania   kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akikumbatiana kwa furaha na kijana mlemavu wa ngozi Albino Lazaro Malendeka ambaye alikuwa mtumishi wa kikundi cha Red Briged cha Chadema baada ya kujiunga na CCM mjini Geita leo.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania   kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwapokea  mlemavu wa ngozi Albino Lazaro Malendeka kushoto ambaye alikuwa mtumishi wa kikundi cha Red Briged cha Chadema baada ya kujiunga na CCM mjini Geita leo na William Mabula Msalaba aliyekuwa mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Geita.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania   kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wagembea ubunge wa mkoa wa Geita katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Geita leo.
 Wananchi wa Katoro wakiushangilia msafara wa Dkt Magufuli alipokuwa akielekea kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Msafara wa Mgombea Urais ukielekea kwenye mkutano wa hadhara ndani ya mji Mdogo wa katoro mkoani Geita. 
 Nyomi
 Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania   kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Geita Mama Fatma Mwasa,pichani kati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza na Mjumbe wa kamati ya ushindi ya CCM mjini Geita wakati wa mkutano wa kampeni leo
 Wakazi wa Geita wakishangilia jambo kwenye mkutano huo wa kampeni.

 Wananchi wa Geita mjini wakifuatilia mkutano wa kampeni
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita na mgombea ubunge wa jimbo la Geita vijijini Ndugu Joseph Kasheku a.k.a King Msukuma akihutubia malefu ya wananchi wa Geita mjini kwenye mkutano wa kampeni wa Urais,ambapo Ndugu Joseph aliwaomba wakazi wa Geita na vitongoji vyake kumchagua Dkt John Pombe Magufuli awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka.
 Mgombea Ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Steven Masele akimwombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwa wakazi wa Geita
 Nyomi la watu likishangilia
 Wananchi wa Geita mjini wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Nyakahura,wilaya ya Biharamulo alipokuwa akielekea mkoani Gieta kuendelea na kampeni zake.