ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 22, 2015

JEMBE FM MWANZA YAFUNGUA MILANGO KWA VYAMA VYA SIASA KUTANGAZA MIKUTANO LIVE.

 Mbio za kampeni ya uchaguzi mkuu 2015 tayari zimeanza. Ni wasaa sasa kwa wagombea wa vyama mbalimbali kupishana huku na kule vijiji kwa vijiji, kata kwa kata, wilaya kwa wilaya, mkoa kwa mkoa wakifanya mkutano ya kampeni za siasa kutambulisha wagombea wao na kuzinadi sera zao al-muradi wapate ridhaa ya wananchi. 

Zoezi hilo ni gumu ila sisi kama jEMBe fM tunalirahisisha!! Sasa ili upate kuwafikia wananchi wengi ndani ya muda mfupi jEMBe fM imefungua milango kwa kutoa huduma ya matangazo ya moja kwa moja yaani LIVE toka viwanja vya mikutano tena full kiwango (HATUBAHATISHI) kwa maelezo zaidi piga simu kitengo cha masoko katika namba ±255282506068 au fika katika ofisi zetu zilizopo jengo la PPF ghorofa ya 6.
@jembenijembe

CAROLINA CHILELE AIBUKA MSHINDI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015

Hatimaye Shindano la Mama Shujaa wa Chakula  linaloendeshwa na Shirika la Oxfam kupitia Programu yake ya Grow ambapo kauli mbiu ni Wekeza kwa wakulima wanawake wadogo wadogo inalipa lafika tamati ambapo kulikuwa na mchuano mkali kati ya washiriki 15 ambao walikuwa katika Kijiji cha Kisanga Wilayani Kisalawe Mkoani Pwani wakiwa na shughuli mbalimbali za Kilimo ambazo zililenga hasa katika kuwakomboa wakulima wadogo wadogo wanawake.  Washiriki hao walikaa kijijini kwa muda wa siku 21  hatimaye kufikia kumpata mshiriki mmoja ambaye amejishindia kiasi cha Tsh 20,000,000 fedha ambazo zitanunua pembejeo za Kilimo. Fainali hizo zilifanyika katika Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam
 Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 msimu wa nne akitoa neno la Shukurani kwa ushindi alioupata , Ameshukuru shirika la Oxfam kwa kuendesha shindano hilo na kuahidi kuwa atakwenda kuwa Balozi mzuri na kusema kuwa washiriki wote ni washindi na yeye amepata zawadi hiyo kuwawakilisha wote.
 Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa Nne 2015 Bi. Carolina Chilele(Kulia) akikabidhiwa Ngao yake ya Ushindi na Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam
 Afisa Kilimo Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Dkt. Kissa Kajigili , akiwapongeza Oxfam kwa kuandaa shindano la Mama Shujaa wa Chakula na washiriki wote kwa ujumla walioshiriki katika Shindano hilo, Pia alimpongeza Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2015 Carolina Chilele na kumtaka awe mfano bora pia akawe chachu ya kuinua kilimo na kuwasaidia wenye uhitaji yaani wakulima wanawake wadogo wadogo, Mwisho aliwaomba Oxfam waendelee na Shindano hili muhimu.
Jackson Yusuph Mzumba Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kibweni akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya Serikali ya Kijiji cha Kisanga 
Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula wakiimba wimbo maalum ikiwa ni Ishara ya hitimisho katika Shindano hilo
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kisarawe Bw. Ellioth Phillemon Mwasambwite akiwashukuru Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 , na kuwaaaga rasmi, pia kumpongeza Mshindi wa Shindano hilo msimu wa Nne Bi. Carolina Chilele , Mwisho aliwapongeza Oxfam kwa kuanzisha shindano endelevu kwa Maendeleo ya wakulima hasa wanawake.
Mmoja wa akina mama ambao walikuwa wanakaa na Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Kisanga Bi. Sophia Shomvi akitoa neno la Shukurani kwa washiriki hao kwa  jinsi walivyo kaa vizuri pamoja na pia kuwaachia elimu kubwa wanakijiji hao. Mwisho alitoa neno la Kuwaaga Rasmi 
Anaitwa Misoji akiwa anatoa Burudani ya Nguvu
Kiongozi wa Timu ya Urasimishaji ardhi vijijini kutoka Wizara ya Ardhi nyuma na Maendeleo ya Makazi Bw. Swagile Msananga akiwapongeza washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015, pia kwa mshindi wa Shindano hilo kwa msimu wa Nne 2015 Bi. Carolina Chilele kwa ushindi wake na kumtaka kuwa mfano Bora kwa jamii kwa ujumla, Pia alisisitiza watu sio kuwa tu na ardhi lakini pia kupata umiliki wa ardhi  walizonazo.
Msema Chochote katika Sherehe ya kuhitimisha shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 zilizofanyika Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam Suhaila kutoka Oxfam akiendelea na ratiba.
Baadhi ya Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakipewa  tuzo za ushiriki wao na Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster
Bi. Hawa Mkata aliyekuwa Mshiriki kutoka Mtwara akitoa neno la Shukurani kwa wanakijiji wote ambao waliishi nao Kijijini kwa Muda wa Siku zote 21, na zaidi zile Familia ambazo wao wamekuwa nao kwa kipindi chote cha Shindano hilo, Mwisho aliwaomba washiriki wenzake kujua kuwa wote ni washindi lakini mmoja ndio kawawakilisha kwa kuchukua zawadi ile ya Milioni Ishirini.
Eva Mgeni, Mshiriki kutoka Bagamoyo Kutoka Mkoa wa Pwani, Akitoa Shukurani zake kwanza kwa Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow ambayo kauli mbiu yake ni kuwekeza kwa wakulima wadogo wadogo wanawake inalipa kwa kuendesha shindano hili na kuwa kupitia washiriki wa shindano hilo wamejifunza mambo mengi na ya kimaendeleo, Mwisho aliwashukuru wanakijiji wote kwa ushirikiano wao na Moyo wa Ukarimu katika kipindi chote wakiwa Kijijini.
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akitoa salam zake za Shukurani kwa wote waliofanikisha shindano la Mama shujaa wa Chakula kwenda vizuri tangu mwanzo mpaka mwisho, aliwashukuru wanakijiji cha Kisanga kwa kukubali kwao shindano lifanyike katika kijiji hicho pia aliwapongeza washiriki wote wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula na kuwasihi kuwa wote walikuwa ni washindi, Mwisho alichukua nafasi hiyo kumpongeza Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 na kumsihi aende kuwa mfano wa kuigwa kwa wakulima wenzake pia akawe Balozi mzuri na kuiwakilisha vema Oxfam
Baadhi ya Wageni waalikwa , Wafanyakazi wa Oxfam, Ndugu jamaa na Marafiki wakiwa katika Sherehe za Fainali za Shindano la Mama shujaa wa Chakula.
Picha ya pamoja

MAANDALIZI YA UZINDUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU CCM YAKAMILIKA, MAGUFULI, SAMIA KUUNGURUMA JANGWANI KESHO

Katibu Muenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Juma 'Gadafi' akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisi kwake leo asubuhi, kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya uzinduzi wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu wa chama hicho utaofanyika kesho viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Picha zikichukuliwa.

Na Dotto Mwaibale

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kimetangaza ratiba ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.

Katibu Muenezi wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Juma 'Gadafi' akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake Dar es Salaam leo asubuhi, alisema maandalizi yote ya uzinduzi huo tayari yamekamilika.

"Maandalizi yote tayari yamekamilika na leo jukwaa kubwa la kukaa viongozi linafungwa na tunategemea kuwa na watu wengi katika uzinduzi huo" alisema Gadafi.

Gadafi alisema kuanzia saa tatu asubuhi watu kutoka sehemu mbalimbali na wapenzi wa chama hicho wataanza kuwasili katika viwanja hivyo ambapo viongozi wastaafu wa chama na serikali na wale waliopo kazini watafuatia na kisha watawasili mgombea nafasi ya urais kupitia CCM Dk.John Magufuli na mgombea mwenza wake Samia Hassan Suluhu na baadae Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.

Alisema katika uzinduzi huo wageni mbalimbali wamealikwa kutoka mikoa ya jirani na mabalozi kadhaa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Gadafi alisema kuwa wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo viongozi wa chama hicho wakiwemo mgombea urais Dk.Magufuli na mgombea mwenza wake watahutubia wanachama kuelezea sera za chama hicho na utekelezaji wa ilani ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu.

Gadafi alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi, wanaccm na makundi mengine kufika katika uzinduzi huo ambapo kutakuwepo na vikundi mbalimbali vya burudani na kufanyika kwa dua za madhehebu yote za kukiombea chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu kama inavyofanyika vipindi vyote wanapo zindua kampeni za uchaguzi mkuu.

Katika hatua nyingine Gadafi amekemea vikali vitendo vya udhalilishaji kwa wanachama wake vya kuzomewa na kuchaniwa nguzo zao wanapopita maeneo ya Kariakoo na Mwenge.

Alisema kila mwana chama yeyote wa chama cha siasa ana haki ya kuvaa nguo za chama chake hivyo kuwazomea wanachama wao ni kukiuka sheria ya nchi na inaweza kuleta ugomvi pale upande wa pili utakapoamua nao kujibu mapigo.

"Napenda kuiomba serikali ya mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Suleiman Kova kukomesha vitendo hivyo dhidi ya wanachama wetu na kama wanaona tunawakera wasubiri majibu yao baada ya uchaguzi kwani CCM itachukua ushindi mapema huku wakibaki wakishangaa" alisema Gadafi.

BREAKING NEWS: SUMAYE AJIUNGA NA UKAWA.

CHAMA Cha Mapinduzi, CCM, kimetikiswa tena leo Agosti 22, 2015, baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tatu Mh. Frederick Sumaye kujivua uanachana na kujiunga na UKAWA.

Sumaye ametangaza uamjuzi huo mbele ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jioni hii pale Bahari Beach Hotel, jijini Dar es Salaam.

Ni mahala hapo hapo ambapo Waziri Mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa, alitangaza kujivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na CHADEMA.

Sumaye anakuwa mtu wa pili wa CCM aliyewahi kushika wadhifa wa juu serikalini kutangaza kujivua uanachama wa chama hicho.
Pichani Sumaye akiwa meza kuu na Mgombea urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, anayewakilisha vyama vya UKAWA, Mh. Edward Lowassa, na viongozi wengine wa UKAWA.

Akieleza sababu za kukihama chama hicho, Sumaye amesema, CCM imejaa kiburi na kwa kudhihirisha hilo, wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi, viongozi wa chama hicho,  waliokuwa wakizunguka nchi nzima, walijielekeza zaidi kjuishambulia serikali badala ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura. "sitoki CCM labda nina hasira na ccm, au sikutchaguliwa kwa vile sikuteuliwa, na wala sitoki CCM ili kudhoofisha chama cha Mapinduzi, na badala yake nakiimarisha." alisema wakati akitangaza kujivua uanachama wake.

Kulizuia wimbi la mageuzi ninaloliona ni ngumu kweli kweli, amesema na kjuwahimiza waliobaki CCM na walio kwenye madaraka, wajiunge na upinzani ili kuharakishwa mabadiliko hayo.

GLOBAL EDUCATION LINK (GEL) YASAFILISHA WANAFUNZI KWENDA KUSOMA NCHINI INDIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi, Abdulmalik Mollel akiwa ameambatana na wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwasindikiza wanafunzi 30 wanaokwenda kusoma nchini India jana Agosti 21, 2015 katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi, Abdulmalik Mollel akiwaita majina wanafunzi waliokuwa wanaondoka kwenda kusoma vyuo vikuu nchini India mapema jana Agosti 21, 2015 katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi, wakikagua wanafunzi vyaraka muhimu walizopaswa kusafiri nazo ikiwemo viza, vyeti, na passport.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi, Abdulmalik Mollel akiwaonyesha wanafunzi sehemu ya kwenda kukaguliwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakibadilishana mawazo mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi, Abdulmalik Mollel akiwaelekeza wanafunzi jinsi ya kuingia kwenye sehemu ya ukaguzi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi, Abdulmalik Mollel akiambatana na wanafunzi kuelekea sehemu ya ukaguzi.
Wafanyakazi wa kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukamilisha zoezi muhimu katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka.

Friday, August 21, 2015

HII HAPA VIDEO YA CHADEMA WAKIREJESHA FOMU ZA KUGOMBEA URAIS NEC.


MBIO ZA URAISI - AUGUST.21.2015 | AZAM TV
Mgombea urais kupitia TLP Macmillian Lyimo na mgombea mwenza nao wafika katika ofisi ya tume ya uchaguzi NEC kurejesha fomu ya kuwania urais,
Posted by Simu.TV on Friday, August 21, 2015

FUMO FELICIAN AKITAJA KIKOSI BORA CHA YANGA ENZI ZAKE.


1.Kwa mtazamo wako mwenendo wa timu ya Yanga Africans unakuridhisha?

2.Ni kipi kikosi bora cha Yanga Africans zama zako?

3.Hofu ya mchezo wa Simba na Yanga huwa inaishia kwa mashabiki tu au kiwewe hutawala pia kwa wachezaji?

4.Mchezo gani hutousahau uliowakutanisha ninyi dhidi ya Simba? 

5.Timu gani enzi zako ilokuwa na wachezaji wababe mwanzo mwisho na mchezaji gani aliyekuwa anaongoza kwa undava + uhuni dimbani? 

**SPORTS RIPOTI** ya 93.7 jEMBe fM inayoruka kila siku za juma ambapo jumatano na alhamisi tunakutana katika Jukwaa la Wakongwe inamalizia mazungumzo na Fumo Felician mchezaji wa zamani wa Yanga Africans. 

Ungana na @johnanatory Muda saa tatu kamili usiku hadi saa nne kamili. BOFYA PLAY KUSIKILIZA

Tupate popote ulimwenguni nenda kwenye play store yako download kitufe cha jEMBe fM sikiliza LIVE kwa simu yako ya mkononi.


JEMBE HABARI: MWENYEKITI WA BAVICHA (CHADEMA) ALIYETEKWA APATIKANA AKIWA HOI, WATOTO WAUZWA WILAYANI KAHAMA

Je umeipata habari inayohusu watoto kutoka Burundi waliokamatwa wakisafirishwa kuelekea Tabora kwa ajili ya ajira ya kilimo?? Wamo pia watoto wa Kitanzania wote wakiwa na umri wa kati ya miaka tisa na 14. Jembe Habari imepiga hodi wilayani Kahama na kufanikiwa kumpata kamanda wa Polisi wilayani humo. 

Kwa undani zaidi jiunge na Harith Jaha itakapofika saa moja kamili jioni hii katika Jembe Habari ya 93.7 @jembefm Mwanza. BOFYA PLAY KUSIKILIZA 

Pia siku za juma kila saa moja kamili asubuhi, saa kumi kamili jioni na saa moja kamili jioni.

TIMU YA KAMATI YA AMANI YA VIONGOZI WA DINI MKOA WA DAR WAENDELEA KUJIFUA KUJIANDAA KUWAKABILI WENZAO WA MKOA WA ARUSHA

  Wachezaji wa timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa katika mazoezi ya pamoja yanayoendelea kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki kati yao na timu ya Kamati ya Amani ya Mkoa wa Arusha unaotarajiwa kuchezwa mwishoni mwa mwezi huu. 

Mbali na mchezo huo pia timu hizo zinatarajia kufanya shughuli za Kijamii, ikiwa ni pamoja na kutembelea wagonjwa na Vituo vya Albino kwa lengo la kudumisha Amani na Mshikamano Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu unaotarajia kufanyika Oktoba 25.
 Mazoezi yakiendelea 
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) akishiriki katika mazoezi ya pamoja na timu yake yaliyofanyika leo asubuhi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
 Kontroo imelala hapa.......
 Mbona wa Arusha watakoma.....
 Mazoezi ya viungo......
 Kuweka misuli sawa.....
 Mazoezi ya viungo....
 Baadhi ya Wachezaji wakizungumza na kocha wao baada ya mazoezi.....
 Mazoezi ya viungo........
Picha Na www.sufianimafoto.com