ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 11, 2015

TOP 5 YAZUA VURUGU JIONI HII DODOMA, KUNDI LA LOWASSA HALIJAKUBALIANA NA MATOKEO.

VURUGU zimezuka mchana wa leo zilizodumu hadi majira ya alasili wakati kiza kikiingia wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea na mkutano wake.

Kutangazwa kwa majina matano na kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa (CC-NEC) ya chama hicho jana usiku, kumeibua mgawanyiko miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo, ambapo watatu wa wajumbe 32 wa kamati hiyo waliibuka wazi na kupinga uteuzi wa majina hayo mbele ya vyombo vya habari. 

 Baadhi ya Wanachama kwa idadi kubwa wameonekana waziwazi wakiandamana kuishinikiza Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM kulirudisha jina la mgombea wao Mhe. Lowassa.

 ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA KILICHOJILI.
Barabara kuu iendayo jengo kuu la Chama cha Mapinduzi mkoani (CCM) Dodoma, (Nyerere road) imegeuka kuwa ukumbi wa mkutano kwa umati wa watu kufurika.

Alasiri hii halmashauri kuu ya chama hicho ilifaanya kikao chake kupata majina matatu, halafu baadae leo jioni mkutano mkuu wa chama hicho unatarajiwa kukaa kupigia kura jina moja kati ya hayo matatu.

Yule atakayeibuka mshindi kati ya watatu hao ndiye atakaye kuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Ulinzi umeimarishwa.
Kutoka juu, taswira ya eneo la viwanja vya ukumbi wa mkutano sanjari na maeneo jirani.
Polisi wakiendelea kuwanasa wanaosadikika kufanya maandamano ambayo yanaashiria vurugu.
Wanachama wa chama hicho wametapakaa kila kona.
Mpasuko huu unaonekana kuwa mwanzo wa kutimia kwa utabiri wa wachambuzi mbalimbali ambao walionya mchakato huu unahatarisha uhai wa chama kikongwe nchini Tanzania.

Majina matano yaliyopitishwa na Kamati Kuu ni Bernard Membe (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. John Magufuli (Waziri wa Ujenzi) Dk. Asha-Rose Migiro (Waziri wa Katiba na Sheria) January Makamba (Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia) na Balozi Amina Salum Ali (Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Tume ya Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa, Marekani)

Kufikia Jumapili, tarehe 12. Julai, Watanzania watakuwa wamejua ni nani atakayekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM kwa uchaguzi mkuu ujao.

PICHA NA MWANDISHI WA Gsengo blog ZEPHANIA MANDIA: DODOMA

NIA YA UDIWANI KATA YA SEGEREA NUSURA UMTOE ROHO MTOTO WA MASSABURI

Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea,  Steve Massaburi akiwa Hospitali ya Aga-khan leo akiendelea na matibabu.
Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea,  Steve Massaburi akiwa Hospitali ya Aga-khan leo akiendelea kuuguza majeraha baada ya kujeruhiwa kwa mapanga nyumbani kwake Segerea jijini Dar es Salaam jana na watu wasiojulikana. Kushoto anayemuhudumia ni jamaa yake Martin Pemba.

Na Dotto Mwaibale

WATU wasiojulikana wamejeruhi kwa mapanga Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea Steve Massaburi usiku wa kuamkia juzi nje ya nyumba yake alipokua akirejea kutoka matembezini.

Kwa mujibu wa Steve aliyelazwa katika Hospitali ya Aga khan, watu hao wapatao wanne wakiwa na Pikipiki, walimvamia majira ya saa tatu usiku nje ya geti la nyumba anayoishi na kuanza kumshambulia huku yeye akijaribu kupambana nao.

Steve ambaye ni mtoto wa Meya wa Jiji la Dar es salaam Dk. Didas Massaburi, alisema wakati watu hao wakimshambulia walikuwa wakisema wazi wazi kuwa lengo lao ni kumuona hagombei nafasi ya udiwani katika Kata hiyo ya Segerea baada ya yeye kuonyesha nia ya kutaka kugombea nafasi hiyo.

“Walikuwa wakiniambia kuwa wewe si unautaka udiwani sasa utaugombea ukiwa kitandani au kaburini, hapa hakuna na umaharufu wa mtu kwa kuwa kila mtu anaitaka nafasi hiyo” alisema Massaburi.

Alisema wakati akiendelea kupambana na watu hao alikuwa akipiga kelele jambo lililowafanya watu hao kumuacha na kasha kukimbia huku yeye akiwa amelala chini damu zikimtoka sehemu za shavuni kutokana na panga alilopigwa.

Pamoja na sehemu ya shavuni, watu hao pia wamemjeruhi sehemu mbalimbali za mkono wake wa kushoto alipokuwa akijaribu kuzuia panga kumdhuru sehemu za usoni.

“Kelele nilizopiga ndizo zilizonisaidia kwa kuwa ziliwafanya watu watoke katika majumba yao kuja kunisaidia wakati huo huo watu hao wakikimbia kwa kutumia pikipiki zao mbili walizokuwa wamekuja nao” aliongeza.

Alisema kwa sasa hali yake inaendelea vizuri  tangu alipofikishwa hospitalini hapo jana huku akishonwa nyuzi zaidi ya ishirini katika taya lilipigwa na panga na watu hao. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

MKUTANO WA NEC DODOMA: MEMBE APONGEZWA KUINGIA TANO BORA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete na Makamu Mwenyekiti Visiwani na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Visiwani na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akipongezwa na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa baada ya kuteuliwa kuingia katika tano bora ya wawania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akipongezwa na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa baada ya kuteuliwa kuingia katika tano bora ya wawania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.
Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) (NEC) wakimpongeza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia), baada ya kuteuliwa kuingia katika tano bora ya wawania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC, katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha Rose Migiro wakipongezana baada ya kuteuliwa kuingia katika tano bora ya wawania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta (kushoto) akimpongeza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe  baada ya kuteuliwa kuingia katika tano bora ya wawania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.

DODOMA NUSU PEPONI, NUSU AAaaaaYAaaaaa!!!!.

Wassira out Top 5.
MARA baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC-NEC) ilipotoa orodha ya wagombea watano na baadhi ya majina makubwa yaliyokuwa yakitawala kwenye, vyombo vya habari, mitandao na vinywa vya watu wengi kubwagwa, kama vile jina la Mhe. Edward Lowassa, Mhe. Waziri Mkuu Pinda na wengineo hii ndiyo taswira ya mji wa Dodoma hii leo. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

Lowassa out Top 5.
Lowassa out Top 5.
Mhe. Chegeni.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mgeja.
Makamba katinga Top 5.
Mama Zakia Meghji.
Nyalandu out Top 5.
Membe katinga Top 5.
Vijana wakipongezana Ngeleja out (L) Makamba in (R) kwenye Top 5.
Mhe. Ngeleja akubali maamuzi ya Kamati kuu akisema asiyekubali kushindwa si mshindani.
Wapambembe..
M-NEC toka wilaya ya Tarime Mhe. Gachuma (wa pili kulia) naye huko mjini Dodoma kuwakilisha akiwa na wajumbe wenzake toka maeneo mbalimbali nchini.
 Wagombea Urais walioingia katika hatua ya tano bora, ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Mh. Bernard Membe, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. January Makamba pamoja na Balozi Amina Salum Ali. Majina hayo yanapelekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kujadiliwa na kupatikana matatu yatakayopelekwa kwenye Mkutano Mkuu na kupatikana moja ambaye ndie atakuwa Mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM.

PICHA ZOTE NA: ZEPHANIA MANDIA WA Gsengo blog DODOMA.

MIKIKI MIKIKI YA TOP 5 ZA CCM




PICHA ZOTE NA MPIGA PICHA WETU ZEPHANIA MANDIA WA Gsengo blog DODOMA.

MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM, EDMUND RUTARAKA ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI.

Mtangaza nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini ,Edmund Rutaraka akiwasili katika ofisi za Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro,kwa ajili ya kikao na wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho wa wilaya chenye lengo la kutangaza azma yake ya kugombea Ubunge katika jimbo hilo.
Mwenyekiti wa Makatibu, wa CCM,Kilimanjaro Nemes Kaingirila Maufi akizungumza wakati wa kikao malumu cha kutangaza nia kilichoitishwa kwa ajili ya Naibu kamanda wa vijana wilaya ya Moshi mjini na Mjumbe wa NEC wa chama hicho,Edmund Rutaraka (kulia) kutangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini.
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya  CCM wilaya ya Moshi mjini wakifuatilia mkutano huo.
Naibu Kamanda wa Vijana wa CCM Manispaa ya Moshi na mjumbe wa NEC ,Edmund Rutaraka akizungumza na wajumbe wa Halmshauri kuu  CCM ya wilaya ya Moshi mjini 
Mtia nia Edmund Rutaraka pia ametumia maji ya kunywa kutangaza Nia yake hiyo baada ya wajumbe wote walioshiriki mkutano huo kugaiwiwa yakiwa na lebo maalumu yenye maandishi pamoja na picha yake.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

WAGOMBEA WATANO WA CCM HAWA HAPA, CC YAPASUKA

Dk. Emmanuel Nchimbi akitoa malalamiko yake mbele ya vyombo vya habari mara baada ya kutoka kwenye kikao cha CC.

HABARI CHANZO: MWANAHALISI 
KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC-NEC) imetoa orodha ya wagombea watano bila ya jina la Edward Lowassa kuwemo ndani. Lakini katika hali inayoonesha mpasuko, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu wamepinga uamuzi huo. Anaandika Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Majina yaliyopatikana, ambayo hata hivyo hayajatangazwa rasmi na chama, ni ya Bernard Membe, Dk. John Magufuli, Dk. Asha Rose-Migiro, January Makamba na Balozi Amina Salum Ali.
Membe ni mbunge wa Mtama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Magufuli ni mbunge wa Chato na Waziri wa Ujenzi, Dk. Migiro ni mbunge wa kuteuliwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Makamba ni mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, na Balozi Amina ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Tume ya Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa, Marekani.

Maamuzi hayo hayakuwaridhisha baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu hasahasa wanaojulikana kuwa ni waungaji mkono wa Lowassa, na wametokeza hadharani kuyapinga huku wakilalamika kuwa kanuni zimevunjwa.

Dk. Emmanuel Nchimbi, Sophia Simba na Adam Kimbisa wamefika mbele ya vyombo vya habari mara tu kamati kuu ilipomaliza kikao chake usiku huu, na kusema hawakubaliani na kilichotendwa.
Wajumbe hao wakizungumza kwa kupokezana huku wakitoa kauli kali, wamesema kanuni za utendaji katika vikao vilivyotangulia Kamati Kuu zimekiukwa. Kamati Kuu ina wajumbe 32.

Wamesema ukiukaji umekuja pale Kamati Kuu ilipopatiwa majina matano, badala ya kupokea majina yote ya wanachama walioomba kuteuliwa, ili yenyewe ndiyo itoke na majina matano baada ya kuyafanyia uchambuzi.

“Kanuni zinasema Kamati Kuu itapokea majina ya waombaji wote na ikishafanya uchambuzi wa kila muombaji, yakiwemo maoni ya kamati ya usalama na maadili, ndiyo huchagua majina matano yanayofikishwa mbele ya Halmashauri Kuu,” alisema Dk. Nchimbi ambaye alitokea kama kiongozi wa hao wajumbe watatu.

Kimbisa ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, amesema hawakubaliani na maamuzi yaliyofanywa na Kamati Kuu kwa sababu hawakutarajia Kamati Kuu itakiukwa na kupokea majina ya baadhi tu ya waombaji.

“Haijawahi kutokea tangu nilipoingia katika Kamati Kuu kushuhudia ukiukaji wa kanuni kama ilivyotokea leo (jana) hii. Tumejitahidi kuuliza kwa mwenyekiti imekuaje kanuni inakiukwa lakini tumekosa maelezo ya kuridhisha,” amesema Simba, waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Wakati wajumbe wa Kamati Kuu walipokuwa wanatoka nje ya ukumbi wa kikao, Nape Nnauye, Katibu wa Itikadi na Uenezi, aliwaambia waandishi wa habari kikao kimemaliza kazi, tayari anayo majina matano ya waombaji walioteuliwa kupelekwa NEC, lakini “nitayatangaza kesho (leo) saa 4 asubuhi.”

Muda huo ni muda ambao kwa mujibu wa ratiba aliyoitoa mapema jana, kikao cha NEC kimepangwa kuanza. NEC yenye wajumbe wapatao 378 huwa inajadili majina hayo na kupiga kura ili kuchagua majina matatu ambayo hupelekwa mbele ya Mkutano Mkuu kwa uamuzi wa kupata mgombea.
Mgombea wa CCM anatarajiwa kutangazwa mara tu mkutano mkuu ambao utaanza mchana, utakapomaliza kupiga kura. Mkutano Mkuu una wajumbe zaidi ya 2,000.

Kabla ya hapo, itakuwa yametolewa matokeo ya kura alizopigiwa Dk. Ali Mohamed Shein aliyepitishwa kugombea tena nafasi ya urais wa Zanzibar.

Friday, July 10, 2015

KAMANDA WA JIMBO LA CHUMBUNI AFUTURISHA WANANCHI WA JIMBO LAKE.

Kamanda wa Jimbo la Chumbuni UVCCM Ndg Ussi Salum Pondeza Hanjad akikaribisha wageni wake katika futari aliowaandalia Wananchi wa Chumbuni ikiwa ni kawaida yake kila mwaka hujumuika na Wananchi hao katika futari katika mwezi mtukufu wa ramadhani.
Wananchi wa Chumbuni wakijumuka katika futari ilioandakliwa na Kamanda Hamjad katika viwanja tawi la CCM Muembemakumbi Zanzibar.
Wananchi wakijumuika katika futari ilioandaliwa kwa ajili yao.
Akinamama na watoto wakijumuika katika futari ilioandaliwa kwa ajili yao.
Akinamama
Akinamama
Mzee wa Chumbuni akitowa shukrani wakati wa hafla hiyo ya futari ilioandaliwa na Kamanda wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza.
  Mzee wa Muembemakumbi akisoma dua baada ya hafla hiyo ya futari.
  Dua.