ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 12, 2015

LOWASSA AZIDI KUVUNJA REKODI YA WADHAMINI, APATA 9516 MKOANI TABORA LEO


Waziri Mkuu wa Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wana CCM waliofika kumdhamini pamoja na wananchi wengine, kwenye viwanja vya ofisi za CCM Tabora Mjini, leo Juni 12, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wana CCM 9516 kwa mkoani Tabora, ikiwa ni muendelezo safari yake ya kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kimteue kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea majina kutoka kwa Naibu Katibu wa CCM Wilaya ya Tabora Mjini, Bi. Hidaya Rashid yenye idadi wanachama wa CCM 9516 waliomdhamini ili aweze kuteuliwa na Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza na WanaCCM waliofika kumdhani pamoja na wananchi wa Mji wa Tabora, kwenye viwanja vya ofisi za CCM Tabora Mjini, leo Juni 12, 2015.
Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akimsikiliza Mzee Juma Nkumba, aliewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoani Tabora miaka ya nyuma.

Mh. Lowassa akisalimiana na Mmoja wa Wazee wa Mji wa Tabora.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, PAUL MAKONDA KUTUMIA SEHEMU YA MSHAHARA WAKE KUWALIPA WANASHERIA

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa taarifa ya utatuzi wa migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo.
 Wanahabari wakiwa katika mkutano na Bwana Makonda.
Waandishi wa habari kutoka vyombombalimbali wakichukua taarifa hiyo.

Dotto Mwaibale.
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema atachukua sehemu ya mshahara wake kwa ajili ya kuwalipa wanasheria watano watakao kuwa wanafanya kazi ya kusikiliza na kuwasaidia wananchi wenye migogoro ya ardhi.

Makonda alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya utatuzi wa migogoro ya ardhi katika wilaya yake ya Kinondoni Dar es Salaam leo asubuhi.

"Kama nilivyobadilisha mfumo mzima wa PF3 ndivyo ninavyofanya kwenye ardhi nimechukua hatua mahususi kuchukua sehemu ya mshahara wangu na kuajiri jumla ya wanasheria watano watakao wasaidia wananchi hasa wanyonge kupata haki zao juu ya madai yao mbalimbali yahusuyo ardhi" alisema Makonda.

Alisema wanasheria hao watachukua asilimia 75 ya mshahara wake kwa kazi hiyo hivyo mwananchi wa Wilaya ya Kinondoni hatatakiwa kulipa hata senti tano atakapokuwa amekwenda kupata huduma hiyo.

Makonda alisema kuwa kuanzia Jumatatu ya Juni 15, 2015 wanasheria hao watakuwepo ofini kwake watakaofanya kazi saa zote kwa lengo la kusaidia ili wapate uelewa wa kisheria juu ya haki zao zozote kuhusu umiliki wa ardhi.

Makonda alisema heshima aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete ya kumteua kuwa mkuu wa wilaya hiyo kwake anatafsiri kama changamoto kubwa ya kuhakikisha anashughulikia kwa kina matatizo ya msingi ya wilaya hiyo.

Alisema katika wakati huu huwezi kutaja changamoto kubwa tatu za wilaya hiyo ukaacha kutaja migogoro ya ardhi na kuwa kwa ufafanuzi zaidi unaweza kurejea hotuba yake ya Februari 28, 2015 wakati akianza kazi mambo aliyoyataja na kuyapa kipaumbele ambapo alitenga kila siku ya Ijumaa kuwa ni siku ya kukutana na watu wenye migogoro ya ardhi ili kuitatua.

Makonda alisema ili kumaliza changamoto hiyo ya migogoro ya ardhi kama si kuipunguza kwa kiwango cha juu kila mkazi wa wilaya hiyo anatakiwa kuchukua kopi ya hati au nyaraka yoyote ile inayompa uhalali wa kumiliki ardhi, shamba au kiwanja na kopi hizo zipelekwe kwa ofisi ya mtendaji wa kata kwani kuanzia Julai 2, 2015 yeye na timu ya watu wa ardhi atahamishia ofisi yake kwenye kata hizo kwa ajili ya kuzihakiki nyaraka hizo.

Alisema pindi watakapo baini kuwa kiwanja kimoja kina zaidi ya mmiliki mmoja watamtafuta mmiliki halali kupitia vyombo walivyonavyo na atakayebainika ameghusi atachuliwa hatua.

Alisema lengo la kuhamishia ofisi yake kwenye kata ni kufuta kabisa uzoefu wa kusikitisha wa wananchi mmoja kugundua kwamba kiwanja chake kinamilikiwa na mtu mwingine baada ya kumwaga roli la mchanga ama tofali. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com- simu namba 0712-727062)

PINDA ATEGUA KITENDAWILI CHA UWANJA WA NYAMAGANA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipiga mpira wakati alipofungua mashindano ya UMISETA kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akisalimia maelfu ya wananchi vijana waliofurika katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, hivi majuzi kwenye uzinduzi wa Mashindano ya 37 ya Michezo ya Shule za Sekondari nchini UMISETA. 
Ze nyomi.
Watoto, vijana, akina mama na akina baba wako hapa.
Parade.
Washiriki wa UMISSETA Kanda ya Kati Singida na Dodoma.
The parade.
Kanda ya Kaskazini Magharibi.
Kanda ya Kaskazini Mashariki.
The parade.
Vijana wamejitokeza kushiriki kikamilifu.
Michezo ni furaha, michezo ni afya.
Nyanda za juu kusini.
Mwonekano wa uwanja kwa eneo la kati.
Wimbo maalum uliimbwa kama sehemu za shamrashamra za Mashindano.
HATIMAYE huenda kitendawili cha uwanja wa Nyamagana sasa kikateguliwa baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda kuahidi kulifanyia kazi suala hilo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo majuzi jijini Mwanza katika uzinduzi wa Mashindano ya 37 ya Michezo ya Sekondari nchini UMISETA.
Hali ya uwanja wa Nyamagana ulivyo sasa. 


Awali Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Magesa Mulongo alimueleza Waziri Mkuu suala la Uwanja wa Nyamagana kuwa Changamoto kubwa, naye waziri anayehusika na TAMISEMI Hawa Ghasia akiwasihi wanamichezo kujitokeza kwa wingi katika Mashindano hayo mwanzo hadi tamati.

MEMBE ANUSURIKA AJALI YA NDEGE, ZANZIBAR.

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (pichani) , amenusurika kifo baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kutoka Iringa kwenda Zanzibar kutaka kugongana uso kwa uso na ndege nyingine dakika moja kabla ya kutua.

Waziri Membe akiwa na ujumbe wake wa watu wanane, walikuwa wakisafiria ndege ya kukodi kampuni ya 5H NEG Precition Aviation ikirushwa na rubani Mathew Mhahiki, ambaye ameonyesha kushangazwa na tukio hilo alilodai “ni kwa rehema za Mungu tumepona ajali hii.”

Akizungumza na mwandishi wetu aliyeko katika ziara yake, rubani Mhahiki alisema: “Lazima kuna tatizo katika control center hata hivyo tayari nimeongea nao na wameniomba samahani na kudai walipitiwa, maana kwa hali ilivyokuwa ni kwamba tungegongana wakati wa kutua maana nimeshangaa tu kuona ndege hii hapa ndiyo maana nikaamua kumkwepa mwenzangu nikapanda juu.”

Waziri Membe alisema: “Nina uzoefu mkubwa wa kusafiri na ndege mahali pengi duniani, hali hii ilikuwa ni ajali na labda sasa tungekuwa dead bodies, lakini ninajua Mungu yuko upande wetu katika safari hii ya uhakika, lakini pia izingatiwe nimekuja kufanya kazi ya Mungu.” 

“Katika safari hii tutashuhudia mambo mengi sana, lakini kwa kuwa kila ninapotaka kuondoka nyumbani ama hotelini mara nyingi nimekuwa nikimtanguliza Mungu maana bila Mungu hii ilikuwa ni mwisho wa maisha yetu tuliokuwa kwenye ndege hii.”

Waziri Membe alikuwa amealikwa mjini hapa na Umoja wa Akimama wa Kikristu (Umaki) wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar waliokuwa wakifanya mkutano wao mkuu unaofanyika kila baada ya miaka mitano akitokea Iringa ambako alikwenda kutafuta udhamini wa chama ili kumwezesha kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, CCM.

Akiwa uwanjani hapo, Waziri Membe alikutana na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba aliyekuja hapa Zanzibar kutafuta wadhamini ambapo makada hao walipata nafasi ya kuzungumza. 
Akiwa katika mkutano huo, Waziri Membe alisema: "Miongoni mwa mambo yanayonikera ndani nafsi yangu ni kuona mwanamke bado anaachwa nyuma, hili halipendezi, ni lazima tuhakikishe wanawake wanapata elimu ya ufundi stadi maana mwanamke akiwezeshwa hasa katika eneo hili la elimu wanaweza hata kushinda wanaume wengi.”

“Ni lazima kina mama wawezeshwe kujiajiri ili msiwategemee kina baba kwa kila jambo lakini pia ili kufikia malengo hayo ni lazima tuwape elimu kina mama.”

WASHINDI WA PROMOSHENI YA KILI WAWASILI KUSHUHUDIA TUZO ZA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2015.

Baadhi ya washindi wa prpmosheni za Kilimanjaro waliowasili jijini Dar es Salaam kushuhudia  Kilimanjaro Tanzania Music Awards zinazotarajiwa kufanyka kesho katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Msham Isihakamwaka kutoka Mtwara, David Justin kutoka Mtawara na Robson Steven kutoka mkoani Mbeya.Tayari wako jijini Dar es Salaam kushuhudia Tuzo za Kilimanjaro kesho.
Na Mwandishi Wetu.
WASHINDI waliopatikana katika Promosheni za Bia ya Kilimanjaro zilizofanyika nchini kote wameanza kuwasili jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo kushuhudia Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards. Hafla ya kukabidhi tuzo hizi inategemewa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kesho Jumamosi 13 June 2015.

Akizungumza na mwandishi wetu, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Bi. Pamela Kikuli amesema jumla ya washindi 22 wanatarajiwa kuwasili leo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania. Washindi hawa wataungana na washindi wengine 4 wa Hapa Dar Es Salaam.

Bi. Pamela amesema washindi hawa walichaguliwa kwanjia ya kuponi baada ya wao kama wanywaji kununua bia ya Kilimanjaro kwenye Bar zilizokuwa na Promosheni. Washindi hawa wanalipiwa gharama zote za usafiri, Malazi na chakula kwa kipindi cha siku zote tatu watakazo kuwa hapa jijini.


Bi. Pamela amesema washindi wanaokuja nikutoka katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Dodoma, Tanga, Mtwara, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Kahama, Musomana Dar es Salaam.

PICHA NA PRESS RELEASE YA UZINDUZI WA KINYWAJI KIPYA TBL - KILIMANJO TWIST

Waremo wa kinywaji kipya cha Kill Twist wakishangilia boti ya kisasa iliyokuwa imebeba warembo wenzao na kinywaji hicho wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Ufukwe wa Azura jijini Dar es Salaam.
Waremo wa kinywaji kipya cha Kill Twist wakiwasili katika ufukwe wa Azura wakiwa na kinywaji hicho wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam.
Waremo wa kinywaji kipya cha Kill Twist wakiwasili katika ufukwe wa Azura wakiwa na kinywaji hicho wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam.
Waremo wa kinywaji kipya cha Kill Twist wakishangilia mara baada ya wenzao kuwasili na boti ya kisasda ya kisasa iliyokuwa imebeba kinywaji hicho wakati wa uzinduzi uliofanyika katika Ufukwe wa Azura jijini Dar es Salaam.Kulia ni waandishi wa habari wakiwa kazini.
Waremo wa kinywaji kipya cha Kill Twist wakishangilia mara baada ya wenzao kuwasili na boti ya kisasa ya kisasa iliyokuwa imebeba kinywaji hicho wakati wa uzinduzi uliofanyika katika Ufukwe wa Azura jijini Dar es Salaam.
TBL YAZINDUA BIA MPYA
Dar es Salaam, Alhamisi 11 Juni 2015; Kampuni ya Bianchini (TBL) leo hii imezindua bia mpya ya Kilimanjaro Twist (Kili Twist) yenye ladha ya machungwa. Hii ni mara ya kwanza kwa bia ya aina hii yenye ladha ya matunda kuzinduliwa hapa nchini.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa bia hiyo, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Twist Edith Bebwa alisema, “Leo hii TBL 

imebadilisha mtazamo wa watu wanavyoifikiria bia kwa kuzindua kinywaji hiki. Hii ni bia ya kwanza ya ladha ya matunda humu nchini na tunatarajia kuwafikia wateja wengine ambao wanataka kuhisika mawanakunywa bia lakini kupata ladha iliyo laini na tamu zaidi na ladha halisi ya machungwa”.

Bia ya Kilimanjaro Twist ni bia yenye asili ya Kitanzania kwa 100% na ladha halisi ya machungwa, ina kilevi cha asilimia 2 % tu.

Bia hiiinatengenezwahapanchinikwakutumiaviuongovyenyeuborananimwanafamiliawabiaya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ni kati ya bia bora zaidi nchini.

Biaya Kilimanjaro Twist itauzwakwabeiya TZS 1,500/= na itapatikana katika baa na hoteli zote kubwa za Dar es salaam. Kutoka na namtindowakimiminika cha biahii, mnywajianaptakiburudisho cha hali ya juu na hivyo inawaruhusu wanywaji kuinywa hata mida ya chakula cha mchana, wakati wa mapunziko nyumbani au ufukweni kitu  ambacho bia za kawaida haziruhusu.


“TBL imekuwa mstari wa mbele katika maswala ya uvumbuzi ya viwanwaji vyake na tumeendelea kufanya hivyo na bia hii ya Kilimanjaro Twisti nadhibitisha hilo. Nawasihi wateja waijaribu Kilimanjaro Twist kwani ina ladha nzuri na inastahili katika tukio lolote” alimalizia kwa kusema.

UNFPA-TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA TUME YA MIPANGO YAENDESHA WARSHA MKOA WA MARA

Mgeni Rasmi Bw. Ibrahim D. Kalengo, Mtakwimu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambae anamwakilisha Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, akitoa neno kwa ajili ya warsha hiyo kufunguliwa rasmi.

 SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA IDADI YA WATU (UNFPA) TANZANIA
KWA KUSHIRIKIANA NA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YAENDESHA
WARSHA KATIKA HOTEL YA AFRILUX MJINI MUSOMA

Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, wameandaa warsha kwa ajili ya kuhamasisha na kuwajengea uwezo watumishi wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu kujumuisha masuala ya vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya.

Warsha hiyo inafanyika katika vituo vya Mwanza na Musoma. Katika kituo cha Musoma warsha inafanyika katika ukumbi wa Afrilux Hotel tarehe 11 na 12 Juni 2015. Kituo hiki kinajumuisha Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mkoa wa Mara na Simiyu.

Washiriki wa warsha ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya.
Mwezeshaji Dr. Deograsias P. Mushi ambae pia ni Mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mtafiti wa Ecom Research Group akishusha nondo kwa wanawarsha juu ya mambo mbalimbali yanayohusu ujumuishaji wa masuala ya vijana katika mipango ya maendeleo ya mkoa na wilaya.
Afisa kutoka UNFPA anaeshughulikia maswala ya vijana Bi. Tausi Hassan, akisisitiza jambo kwa washiriki wa warsha kuhusu program za vijana katika shirika la UNFPA.
Washiriki wa warsha kutoka Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mkoa wa Mara na Simiyu ambao ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya wakimsiliza kwa makini mwezeshaji.
Washiriki wa warsha kutoka Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mkoa wa Mara na Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa warsha hiyo.

SHINDANO LA ON LINE ART &SCIENCE LAPATA WASHINDI

Baadhi ya  washindi wakiwa wanakabidhiwa zawadi zao.
Baadhi ya  washindi wakiwa wanakabidhiwa zawadi zao.
Burudani ya sanaa ikiendelea.
Mmoja ya washiriki akiwa anaendelea kuchora wakati wa Sherehe hizo.
Picha ya Pamoja 

SHIRIKA la FASDO (Faru Arts and Sports Develepment Organization) leo hii limetoa zawadi kwa washindi wa shindano la Na Mimi Nipo- Online Arts and Science Competition katika ukumbi wa  kituo cha utamaduni cha Urusi nchini (Russian Tanzania Cultural Center).

Shindano hilo linalohusisha vipaji vya uchoraji, sanaa za mikono na ubunifu wa kisayansi lililozinduliwa mwezi Februari mwaka huu kwa lengo la kutambua vipaji vya vijana wenye umri kati ya miaka 12 hadi 24 limefikia kilele chake leo hii kwa kuwapata washindi sita, wawiliwawili kutoka katika fani za Uchoraji, Sanaa za Mikono na Ubunifu wa Kisayansi. 

Zoezi la kutoa zawadi kwa washindi hao lilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Dr. Diodorus Buberwa, Mkurugenzi wa Kituo cha utamaduni cha Urusi nchini hapa, Alexander Tsykunov na wageni waalikwa.

Akizungumza na washiriki pamoja na wageni waalikwa katika Sherehe hizo Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji aliwapongeza sana vijana kwa kuwa na vipaji vya hali ya juu na kusisitiza kuwa eneo hili la sanaa ya Uchoraji linatakiwa kupewa kipaumbele, aliongeza kuwa Tanzania sasa inatakiwa kuwa na maeneo zaidi kwa ajili ya kukuza sanaa hizi, na katika kuendeleza na kusapoti sanaa , Mh.Balozi Buberwa amechangia Tsh 1,000,000.

Washiriki walikuwa 27 lakini waliopata zawadi walikuwa ni washiriki 6 ambao walizingatia umri kati ya miaka 12 hadi 24 na washindi hao ni pamoja na Thomas Mwakilima, Anhony Tendwa, Primus Mapunda, Philipo Frolian, Cornelio Malya na Anderson Msangi washindi wote wamepata zawadi Dola 300.

Thursday, June 11, 2015

CHUMBA CHA HABARI CHA GAZETI LA JAMBO LEO NA STAA SPOTI CHAZIZIMA KWA HUZUNI BAADA YA KUFIWA NA MENEJA WAO MZEE RAMADHANI KIBANIKE

Marehemu  Ramadhani Kibanike enzi za uhai wake.
 Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Julian Msacky na Mwandishi wa Habari, Stela Kessy (kulia), wakiendelea na kazi huku wakiwa na hudhuni baada ya kupokea taarifa ya kifo cha Kibanike leo jioni.
Mwanahabari Celina Mathew akilia kwa uchungu baada ya kupokea taarifa hiyo.
Ofisa Matangazo, Kinai akiwa amepigwa butwaa kutokana na  kifo hicho.
Wanahabari Nyendo Mohamed (katikati), Edith Msuya (kulia) na  Magendela Hamisi wakiwa katika hali ya huzuni kufuatia kifo hicho.
Mwanahabari Magendela Hamisi akitafakari juu ya kifo hicho.
Msanifu kurasa wa gazeti la Jambo Leo, Elizabeth Mkeleja alishindwa kujizuia kulia.
Mwanahabari Grace Gurisha akisaidiwa na wenzake baada ya kuishiwa nguvu muda mfupi baada ya kupata taarifa hizo za kifo cha Meneja  Ramadhani Kibanike.


Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya JL Comunications inayochapisha magazeti ya Jambo Leo, Staa Spoti, imepata pigo baada ya aliyekuwa Meneja wake Mkuu Ramadhani Kibanike kufariki.

Kibanike amefariki dunia leo mchana nyumbani kwake Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Akitoa taarifa ya kifo hicho kwa wafanyakazi wa Kampuni hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Theophil Makunga alisema Kibanike alikumbwa na mauti leo mchana.

Taarifa hiyo ambayo iliwashtua wafanyakazi wa Kampuni hiyo na hata kupelekea baadhi yao kupoteza fahamu, ilisababisha pia kusimama kwa muda kwa shughuli za Kampuni hiyo.

Mipango ya mazishi bado inapangwa, na msiba upo nyumbani kwa marehemu Tabata Jijini Dar es Salaam. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com- simu namba 0712-727062)