ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 21, 2015

LEO NDANI YA JEMBE BEACH NI KUJEMBEKA TU NA SAUTI SOL.


Ilikuwa Mwezi, siku hatime zimesalia dakika ule mpango mzima wa kuzifungulia burudani ulioasisiwa na redio mpya ya jijini Mwanza JEMBE FM na kubatizwa jina 'JEMBEKA' uanze rasmi. 

Ni leo JUMAMOSI tarehe 21/02/2015 ndani ya kiota cha burudani cha kitalii Jembe Beach Mwanza.

Burudani itakayo fungua mpango huo wa 'JEMBEKA' ni kutoka kwa kundi maarufu Afrika Mashariki lililovuka mipaka na sasa muziki wake kuchezwa hadi barani Ulaya kundi la Sauti Sol toka nchini Kenya ambao watapiga muziki LIVE.

Vijana wa Nyumbani JJ Band nao watakuwepo ndani ya Jembe Beach Resort kwaajili ya kumwaga burudani ya kijanja zaidi ya vile ulivyowazoea.

Kiingilio ni shilingi 10,000/= kwa tiketi za awali na Tshs 15,000/= ukinunua getini.
Tiketi zinapatikana SASA ofisi za Jembe Fm zilizopo PPF Plaza Mwanza. 
Ni matayarisho ya mwisho mwisho ndani ya Jembe Beach.
Mwonekano wa leo.
Jiografia ya leo.

ALLIANCE YAFAULISHA WANAFUNZI WOTE KIDATO CHA NNE KWENDA CHA TANO YAWA YA PILI MKOA YAONGOZA

NA PETER FABIAN, MWANZA.
MATOKEO YA KIDATO CHA NNE KWENDA CHA TANO KITAIFA NA MKOA WA MWANZA .
*Kitaifa sekondari ya wavulana imeshika nafasi ya Pili kati ya sekondari 2,322 na Mkoa imekuwa ya Kwanza kati ya sekondari 174.
*Kitaifa sekondari ya wasichana imeshika nafasi ya 13 kati ya sekondari 2,322 na Mkoa imekuwa ya Pili kati ya sekondari 174.
*Wanafunzi wamepata daraja la Kwanza na Pili  (Division one na two) hakuna la tatu, nne au waliofeli.
* Masomo waliofanya vizuri ni Uraia, Historia, Biologia, Kemia, Kingeleza, Hesabu na Biashara.
SEKONDARI za Alliance, Wavulana na Wasischana za jijini Mwanza zimeongoza nafasi ya kwanza naya pili kwa shule za sekondari za serikali na binafisi mkoani Mwanza, baada ya kutangazwa hivi karibuni.

Mkurugenzi na Mmiliki wa Kampuni ya Nyamwaga Ltd ya jijini Mwanza inayopilikia Shule za Sekondari, Msingi, Awali na Kituo cha Michezo vya Alliance, James Bwire, akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa alisema kwamba, matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2014/2015 sekondari ya wavulana Kitaifa imeshika nafasi ya Pili kati ya sekondari 2,322 nchini na Mkoa ya Kwanza kati sekondari 174.

Bwire alisema sekondari hiyo kwa Mkoa wa Mwanza imeshika nafasi ya Kwanza kwa kufaulisha wanafunzi 43 kwa daraja la kwanza (Division one) na daraja la pili mwanafunzi mmoja (Division Two) kati ya watahiniwa 44 waliofanya mtihani wa Taifa katika sekondari hiyo mwaka 2014/2015 na hakuna aliyefanya vibaya  na kupata GPA alama 4.4937 huku wakifaulu masomo ya Uraia (Civics), Historia, Geografia, Engilishi, Fizikia (Physics), Kemia (Chemistry),Biolojia na Hesabu (Basic Mathemastic).

Mkurugenzi huyo alisema sekondari ya wasichana Alliance kwa Mkoa wa Mwanza imeshika nafasi ya 13Kitaifa na Mkoa wa Mwanza imeshika nafasi ya Pili kati ya sekondari 174 kwa  kufaulisha ambapo wanafunzi waliopata daraja la Kwanza ni 42 (Division one) na daraja la pili ni 11 (division Two) na hakuna waliofanya vibaya kati ya watahiniwa 53 waliofanya mtihani wa Taifa mwaka 2014/2015 na kupata GPA alama 4.1866 huku wakifaulu masomo ya Biashara (Commerce), Biolojia, Kemia, Fizikia, Kiswahili na Book Keeping.

Bwire alisema siri ya mafanikio ya shule za sekondari Alliance wavulana na wasichana kufanya vizuri ni pamoja na kuwa na walimu wenye sifa na weledi wa kufundisha kwa kujituma, ubunifu wa walimu kutekeleza mikakati ya shule na usimamizi mzuri wa uongozi kwa utekelezwaji wa malengo yanayowekwa kwa walimu na wanafunzi na mazingira bora ya shule kuwa rafiki kwa walimu na wanafunzi.

Aidha aliongeza kuwa pamoja na mafanikio hayo , kumekuwa na motisha kwa walimu kwa kila somo ambalo wanafunzi wanapata alama za juu katika mitihani ya kawaida na ile ya kitaifa, kuwanjengea uwezo walimu na kuwapatia mikopo ya magari, mishahara mizuri na kuwapatia nyumba za kuishi katika eneo la shule jambo ambalo huchangia uwajibikaji wenye tija kwa wanafunzi.

“Kama ilivyo kwa walimu pia shule hutoa motisha kwa wanafunzi wanaofaulu vizuri katika madarasa yao kwa kupata alama za juu kwa kuwalipia ada yam hula mmoja au miaka miwili kulingana na mwanafunzi anavyofanya vizuri jambo ambalo pia limewapa fursa wanafunzi kujituma ili kupata ufaulu mzuri kwa kujisomea wakati wa likizo yam hula na mwaka,”aliseama.

Mkurugenzi huyo alisema kwamba kutokana na uongozi mzuri wa shule zote za Alliance kufanya utafiti na kujiwekea mikakati iliyo na utekelezaji umefanya baadhi ya shule za msingi na sekondari kutoka mikoa ya Mbeya, Dar es salaam, Arusha, Dodoma na Morogoro kuja kujifunza ikiwemo Vituo vya michezo ili kuona Alliance inavyoweza kufanya vizuri zaidi kitaaluma na kimichezo.

RAIS KIKWETE AKABIDHIWA RASMI UENYEKITI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI



Rais Jakaya Mrisho Kikwete(kushoto)akipokea bendera ya Afrika Mashariki(EAC)kutoka kwa Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ikiwa ni ishara ya kumkabidhi rasmi Uenyekiti wa  EAC  kwenye  mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo Ijumaa Februari 20, 2015 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi. Picha na IKULU
TANZANIA inaunga mkono kwa dhati Ushirikiano wa Kikanda na muumini mkubwa wa Umoja wa Africa na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). 

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo  jijini Nairobi mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa EAC na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye amekua mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita
 "Tunaamini kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyogawanyika, haitaweza kuchukua nafasi yake kamili na heshima katika familia ya Mataifa ya Afrika na dunia kwa ujumla" Rais amesema na kuongeza kuwa Tanzania inakua kuwa masoko yaliyogawanyika, miundombinu hafifu baina ya nchi, havina nafasi katika dunia ya leo wala ya baadaye. 

Rais Kikwete amesema na kumpongeza Rais Kenyatta kwa kusimamia utekelezwaji wa maazimio na miradi ya pamoja ya Jumuiya wakati wa kipindi chake cha uenyekiti na kuahidi kuwa Tanzania haitawaangusha wana Afrika Mashariki katika kutekeleza azma yao ya pamoja ya kuendeleza Jumuiya ambayo inaundwa na nchi za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda. 

Rais Kikwete amesema katika utekelezaji wa ajenda ya EAC, biashara imeongezeka kwa kiasi kikubwa na kwamba nchi zote wanachama zinayaona matunda hayo. Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2013 biashara katika nchi za EAC imeongezeka kutoka dola za kimarekani 3, 722.9 hadi dola 5,805.6 ambapo kati ya mwaka 2012 hadi 2013 kumekua na ongezeko la asilimia 6. 

"Kama biashara isiyo rasmi ingerasimishwa, kwa hakika, ongezeko hili la biashara lingekua juu zaidi ya hapa, hivyo imefikia wakati muafaka kurasimisha biashara isiyo rasmi katika ushirikiano wetu" Rais amesema na kuongeza kuwa " kwa njia hii serikali zitakusanya kodi na hivyo kuna umuhimu wa kuelekeza nguvu katika kusaidia biashara ndogo ndogo na zile zisizo rasmi kwa kuziwekea mazingira mazuri".

Rais Kikwete amerejea nyumbani mara baada ya mkutano huo ambao umehudhuriwa na Marais wa nchi zote tano za Jumuiya na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ambaye amehudhuria kama mualikwa maalum katika kipindi hiki ambapo mazungumzo ya awali ya kuijadili nchi yake kama inaweza kupata uanachama katika EAC yanaendelea.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizungumza chemba kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa  Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya  katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa  Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya  katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Kenya, Mhe. William Rutto na maafisa wengine wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa  Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015
Kutoka kushoto ni mgeni mwalikwa, Rais wa Sudani Kusini, Mhe Salva Kiir, Rais wa Burundi, Mhe Pierre Nkurunziza, Rais Jakaya Mrisho Kikwete(Tanzania),Rais Uhuru Kenyatta(Kenya)Rais Yoweri Museveni (Uganda) Rais Paul Kagame (Rwanda) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Balozi Dk Richard Sezibera wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano kwenye  mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki

Friday, February 20, 2015

USIKOSE USIKU HUU BBC DIRA YA DUNIA NA STAR TV.

Hii leo wale vijana machachari wa Yamoto Band kutoka Afrika Mashariki watakuwa LIVE ndani ya BBC DIRA YA DUNIA.  ZAIDI chungulia video ifuatayo hapa chini.

JITIHADA ZA HOSPITALI YA BUGANDO KATIKA KUKABILIANA NA UGONJWA WA SARATANI

Mkuu wa Kitengo cha Saratani Hospitali ya Rufaa Bugando.
 SIKU ya saratani imeadhimishwa mkoani Mwanza kwa uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kukutanana waandishi wa habari kwa lengo la kuelezea mikakati inayofanywa na hospitali hiyo katika kuimarisha tiba ya Saratani.


Maadhimisho hayo yamefanyika wakati huu ambapo idadi ya wagonjwa wa Saratani ikiongezeka katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Dr. Nestory Masalu ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Saratani  Hospitali ya Rufaa ya Bugando anabainisha kasi ya ongozeko la wagonjwa. (BOFYA PLAY KUSIKILIZA)

Mmoja kati ya waathitika wa kansa.
Moja kati ya vichocheo vinavyosababisha ongezeko la idadi ya wagonjwa wa Saratani ni pamoja na... (BOFYA PLAY KUSIKILIZA)


Sehemu ya madaktari kitengo cha upasuaji hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na vitengo mbalimbali.
Wataalamu.
Jengo la matibabu ya Saratani ndani ya Hospitali ya Rufaa Bugando.
 Hospitali ya Bugando tayari imekwisha kamilisha ujenzi wa jengo la matibabu ya Saratani lililogharimu jumla ya Fedha za Kimarekani dola bilioni 7, Je Nini jitihada zaidi kuhakikisha huduma zinaanza katika hospitali hiyo. (BOFYA PLAY KUSIKILIZA)

Asilimia 60 ya wagonjwa wa Saratani nchini wanatoka katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Sehemu ya madaktari kitengo cha upasuaji hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na vitengo mbalimbali.
Lango kuu la jengo la Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.
Kutoka mbali muonekano wa jengo kuu la Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.

PUSH OBSEVER YAZINDUA TEKNOLLOJIA YA KISASA YA UKUSANYAJI WA TAARIFA IJULIKANAYO KWA JINALA NEWS RADAR

Mshauri mkuu wa mradi wa NewsRadar, Romana Gersuni kutoka Ujerumani akielezea jinsi teknolojia hiyo mpya na ya kisasa ya ukusanyaji taarifa mbalimbali ya Push Observer inavyofanyakazi zake.
mkuu wa mikakati wa kampuni ya Six Telecoms ambayo ni kampuni mama ya Push Observer, Rashid Shamte akielezea faida ambazo watazipata kampuni mbalimbali nchini, husasani za kibiashara kwa kujiunga na huduma ya NewsRadar waliyoianzisha nchii.
Mkurugenzi Mtendaji wa  Kampuni ya Push Mobile Fred Manento akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ufanisi wa mradi wa NewsRadar ambao utawawezesha wafanyabiashara kupata taarifa mbalimbali kwa kutumia mradi huo mpya na wa kisasa nchini
Afisa Mawasiliano wa kampuni ya Push Observer, Tunu Makamula akiteta jambo na wadau wa kampuni hiyo waliohudhuria semina elekezi na uzinduzi rasmi wa mradi wa NewsRadar ambao utawawezesha wafanyabiashara kupata taarifa mbalimbali kwa kutumia mradi huo mpya na wa kisasa nchini.
SEKTA zote Nchini sasa zinaweza kupata taarifa mbali mbali zilizorushwa kwene vyombo vya habari kupitia teknolojia mpya ya usambazaji taarifa ijulikanayo kwa jina la NewsRadar ya kampuni ya Push Observer.

Push Observer Limited ni kampuni ya Tanzania inayomiliki vyombo vya kiinteligencia na teknolojia ya sanaa ya kufuatilia, kukamata na kuchuja vyombo vya habari - magazeti, matangazo (radio & televisheni), Internet na uchambuzi, ripoti ya ushindani kwa ajili ya biashara, serikali na wateja wengineo wa mashirika yasiyo ya kiserikali.

Hivi sasa, Push Observer wanachunguza vituo vya redio 90+, vituo vya televisheni 15+, magazeti (magazeti, majarida, magazeti na majarida) 70+ na machapisho online ikiwa ni pamoja na blogs na mitandao maudhui. Observer ni kampuni ya kiTanzania inayoongoza kidigitali, kwa viwango vya kimataifa na ushirikiano wa kimataifa katika data na uanachama na vyombo kama FIBEP, Nudge, Vision Critical, na Harvard Innovation Labs.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mikakati wa Six Telecoms, Kampuni mama ya Push Observer, Rashid Shamte alisema kuwa kupitia teknologia hii ya usambazaji ya kisasa, wateja wao wataweza kupata habari taarifa muhimu na mpya masaa ishirini na nne ya wiki. Aliongeza kuwa,tumezindua teknolojia hii kwa wateja wetu kutokana na teknologia ya uchunguzi wa vyombo vya habari kubadilika sana miaka ya karibuni”.

“Huduma hii ya kusambaza taarifa imekuwa ya kisasa, rahisi na ya ubora wa hali ya juu kutokana na uwekezaji wetu katika teknolojia hii. Wana vifaa vya kisasa ambavyo vinaweza kupata taarifa kupitia televisheni, magazeti, mitandao ya kijamii na redio kwa muda muafaka, vifaa hivyo vinauwezo wa kupata taarifa had 350,000 kutoka vyombo mbali mbali. Kwa kutambua mahitaji ya wateja wetu kupata habari na taarifa za muhimu tumeamua kuzindua huduma hii na ili kuwahakikishia wateja wetu upatikanaji wa taarifa muhimu na taarifa zinginezo za kwene vyombo vya habari kwa muda muafaka” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Push Observer, Tom Kyalo.

AIRTEL YAMTANGAZA BINGWA WA AIRTEL TRACE MUSIC YAMZAWADIA MILIONI 50TZS

Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga (kushoto) akimkabidhi mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga hundi ya mfano yenye dhamani ya sh. 50mil baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya Airtel Trace Music Stars, pia atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya Afrika yatakayofanyika Mjini Nairobi Kenya mwezi machi, anaeshuhudia ni Afisa Uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki.
Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga akifurahia zawadi yake baada ya kuibuka mshindi wa mashindano hayo yaliyofanyika hivi karibuni. Mshindi huyo pia atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya Afrika yatakayofanyika Mjini Nairobi Kenya mwezi machi,
Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga (kati) akiwaimbia waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika hafla ya makabidhiano ya zawadi yake hundi ya sh. Milioni 50 kushoto yake ni Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki (kushoto) na Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga (kulia). Press Release Airtel yamtangaza Bingwa wa Airtel Trace Music, yamzawadia milioni 50TZS

* Nyota wa Airtel Trace Music Stars apatikana Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo imemtangaza rasmi mshindi wa shindano la Airtel Trace Music star, shindano lilidumu kwa muda wa miezi mitatu maalum kwa wasanii chipukizi kuweza kuimba na kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi kama studio kwa lengo la kusaka na kuibua vipaji kwa wanamuziki chipukizi nchini.

Akiongea na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga alisema"Leo tunayofuraha kubwa kumtangaza mshindi wetu wa shindano la Airtel Trace Music Stars mara baada ya kuchaguliwa na majaji na kupigiwa kura na watanzania "Washiriki watano ni kati ya wengi waliothubutu kuonyesha uwezo wao wa kushiriki kwa kupiga simu, kuimba na kutuma nyimbo zao na hatimae majaji wamesikiliza vipaji vyao kama walivyoimba na kuwachagua kuingia tano bora (top 5)" alifafanua Muga.

Washiriki waliokuwa wamebahatika kuingia tano bora ni Nalimi Mayunga mwenye namba ya ushiriki (55100182), Christopher Kihwele (5510050), Tracy Eminence (55100420), Beautus Henry (55100106) na Rose Mbuya (55100366) Mshindi wetu ni Nalimi Mayunga mwenye namba ya ushiriki (55100182) ambae amechaguliwa na majaji wetu pamoja na kupigiwa kura nyingi na wananchi Zawadi yake ni milioni Tshs 50mil, na pia atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya Afrika Nairobi Kenya yanayoshirikisha nchi 13 barani Afrika ambapo pia mshindi atakaepatikana atarekodiwa nyimbo zake katika studio za kimataifa nchini uingereza, na kupewa mafunzo toka kwa msanii nguli wa Afrika Akon.

Nchi nyingine zinazoshiriki mashindano haya na zitakazotoa jumla ya vijana 13 barani Afrika ni pamoja na Kenya, Uganda Zambia, Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, The Democratic Republic of Congo (DRC), na Gabon

Thursday, February 19, 2015

MENGI YAIBULIWA LEO KATIKA MAFUNZO YA KUZUIA UKATILI WA KIJINSIA NA MAAMBUKIZI YA VVU KWA WAANDISHI WA HABARI NA WATOA HUDUMA MWANZA

Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI Yassin Ally akiwasilisha maelezo kuhusu mradi wa mpya ujulikanao kwa kifupi SASA katika semina ya mafunzo ya kuzuia ukatili wa kijinsia na maambukizi ya VVU kwa waandishi wa habari na watoa huduma iliyoanza leo katika ukumbi wa mikutano Hillfront Hotel Igoma Mwanza. 
BAADHI ya Waandishi wa Habari na Watoa huduma mkoani Mwanza wamekutanishwa katika Mafunzo ya kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia yanayotolewa na Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za Wanawake na Watoto la KIVULINI.
Mafunzo hayo yanatolewa kipindi hiki ambapo Mikoa ya kanda ya Ziwa inatajwa kuongoza nchini kwa vitendo vya Ukatili hususani wa kijinsia. (BOFYA PLAY KUMSIKILIZA)

Meneja wa mradi wa SASA wilayani Misungwi Bi.Juliana Myeya akiwasilisha maelezo kuhusu mradi, malengo, utafuti, changamoto  na jinsi utakavyofanya kazi katika awamu ya pili na ya tatu.   
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi KIVULINI Gasper Mwanalyela (Wakili) akiwasilisha changamoto na ugumu wa upatikanaji wa haki kwa wanawake wanaotendewa Ukatili wa kijinsia kupitia sheria ya ndoa na sheria ya Ardhi.
Maimuna Kanyamala ni Muasisi wa Shirika la KIVULINI anabainisha hali ya kijinsia ilivyo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. (BOFYA PLAY KUSIKILIZA)

Sehemu ya wadau na wawakilishi wa mashirika mbalimbali katika mafunzo.
Kwa upande wake mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Mwanza, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Jonathan Shana ametumia ufunguzi wa mafunzo hayo kutoa salamu kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya Ukatili. (BOFYA PLAY MSIKILIZE)

Sehemu ya wadau na wawakilishi wa mashirika mbalimbali katika mafunzo.
Mwandishi wa habari toka Sahara Media Maliganya Charahani akishiriki kutoa uzoefu wake kuhusiana changamoto mbalimbali alizozibaini wakati wa ukusanyaji taarifa za Ukatili wa kijinsia ambazo zimekuwa sugu katika jamii dhidi ya wanawake na watoto.
Suala la katiba iliyopendekezwa ikisubiri kupigiwa kura nalo halikusahaulika ambapo Serikali imeombwa kuharakisha zoezi la kuchapisha katiba iliyopendekezwa na kuisambaza mapema ili wananchi wapate muda wa kutosha kuipitia kabla ya kuipigia kura  ili kubaini kama kuna mapungufu hususani vipengele vilivoongezwa kumpa nafasi zaidi mwanamke. (BOFYA PLAY SIKILIZA)

AIRTEL YAMKABIDHI MKAZI WA KYELA MBEYA BWANA EDOM MWANSASU GARI LAKE

Kamanda mkuu wa polisi wa Mkoa wa Mbeya Bwana Hemed Msangi (wa pili kulia)  akimkabithi mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Edom Dickson Mwansasu  mkazi wa Kyela Mbeya baada ya kuibuka moja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. pichani kushoto ni mke wa Edom Mwansasu na kulia ni Meneja biashara wa Airtel  Nyanda za juu kusini Bwana Straton Mushi.
Mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Edom Dickson Mwansasu  akiwasha gari mara baada ya kukabithiwa gari lake baada ya kuibuka moja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi.

mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Edom Dickson Mwansasu  akiwa ndani ya gari pamoja na mke wake baada ya kukabithiwa gari lake kufatia kuibuka kuwa mshindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi katika droo iliyofanyika ijumaa iliyopita.

Airtel yamkabithi Mkazi wa Kyela Mbeya Bwana Edom Mwansasu gari Lake
·         Baada ya kuibuka kuwa moja kati ya washindi wa wiki ya pili ya Airtel Yatosha Zaidi
Mkazi wa kyela mkoani Mbeya Bwana Edom Dickson Mwansasu amekabithiwa gari aina ya Toyota IST na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mara baada ya kuibuka mshindi kupitia droo ya wiki ya pili ya promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi iliyofanyika siku ya ijumaa iliyopita
Bwana Edom Mwansasu mwenye umri wa miaka 40 anajishughulisha na shughuli za kilimo huko Ngonga Kyela  Mkoani Mbeya  ameibuka mshindi baada ya kununua na kujiunga na  vifurushi vya siku vya huduma ya Airtel yatosha kila siku.
Akiongea baada ya kukabithiwa gari bwana Edom Mwansasu alisema ninafuraha sana kuwa mshindi  na kutumiza ndoto yangu ya kumiliki gari.  Nilipopigiwa simu sikuamini kuwa nimeshinda gari , nilifurahi sana nakupasha habari kwa familia yangu. Sijawahi kumiliki gari hivyo najisikia furaha sana Airtel kunizawadia mimi hii gari kupitia hii promosheni ya Airtel yatosha. Kwa kupitia gari hili sasa na uhakika wa usafiri mimi pamoja na familia yangu lakini pia litanisaidia katika kazi yangu ya kilimo na kuniwezesha kusafirisha mazao yangu kirahisi ukilinganisha na  awali nilikuwa natumia baskeli au kukodi gari.
‘Nawapongeza sana Airtel na nawashauri watanzania kuendelea kutumia huduma ya Airtel yatosha na kuamini kuwa nao wanaweza kubahatika na kushinda kama mimi” aliongeza Mwansasu
Kwa upande wake Kamanda mkuu wa polisi wa Mkoa wa Mbeya Bwana Hemed Msangi alisema”  kwanza kabisa napenda kuwapongeza Airtel kwa kuanzisha promosheni hii kabambe inayowawezesha watanzania kutoka sehemu mbalimbali kujishindia magari.  Naamini kwa kupitia promosheni hii mtawawezesha watanzania wengi kujikwamua kiuchumi na kuwawezesha kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi kirahisi na kwa ufanisi zaidi. Nawapongeza washindi wote waliopatikana mpaka sasa.  Lakini natumia fulsa hii kuwaomba wananchi wadumishe amani maana kama sio amani tulionayo basi promosheni kama hizi zisingeweza kufanyika”
Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja biashara wa Nyanda za juu kusini Bwana Straton Mushi Alisema”  promosheni hii ya Airtel yatosha zaidi ni mahususi kwa wateja wetu Tanzania nzima wanaotumia huduma hii ya Airtel Yatosha kuweza kujishindia gari aina ya Toyota IST kila siku .  kujiunga na vifurushi vya Airtel yatosha mteja anatakiwa kupiga *149*99# au kwa kununua vocha vya Airtel yatosha au kununua kupitia huduma ya Airtel Money na kuunganishwa moja kwa moja kwenye droo itakayomwezesha kushinda.
Mpaka sasa washindi 10 wamepatika ambapo kati yao wawili wanatoka kanda ya nyanda za juu kusini na leo tunamkabithi mshindi wetu wa Mbeya Bwana Edom Mwansansu gari lake na kisha tutamkabithi mshindi wa mkoa wa sumbawanga bwana Saidi Mashiko ambaye ni mganga wa tiba za jadi na mkazi wa Katavi hivi karibuni”
“Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu kujiunga na vifurushi hivi vya Airtel yatosha na kupata nafasi ya kujishindia gari aina ya Toyota IST kila siku”. Aliongeza Mushi
Washinde wengine waliojishindia Toyota IST toka promosheni hii ianze ni pamoja na Ramadhani Dilunga mkazi wa Pwani, Namtapika Kilumba Mkazi wa Mtwara, said Mashiko mkazi wa katavi, Hamim Yoyo mkazi wa Korogwe Tanga, Esther Mashauri Mkazi wa Mwanza, Ibrahim Kimondo mkazi wa Kondoa pamoja na Mwajabu Churian, Sakina Libwana na Justin Wilium wote wakazi wa Dar