ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 4, 2015

WATUHUMIWA 8 WA MAKONTENA 329 YALIYOPOTEA KIAINA BANDARINI WAFIKISHWA MAHAKAMANI.

 Mshitakiwa namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, Tiagi Masamaki (katikati) na washitakiwa wenzake wakitoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo mchana baada ya kusomewa mashitaka yao.
 Watuhumiwa hao wakisindikizwa na maofisa wa polisi kuingia chumba cha Mahabusu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
 Hapa Masamaki na wenzake wakiingia ndani ya gari kuelekea gereza la Segerea.
 Watuhumiwa wa kesi hiyo wakiingia ndani ya gari.


 Mmoja wa watuhumiwa hao akiwa ndani ya gari la Polisi.
 Watuhumiwa hao waliokaa wakiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Gari la polisi lililowabeba watuhumiwa hao likiondoka mahakamani hapo.


Na Dotto Mwaibale




KASI ya utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa Kasim Majaliwa imeanza kuwagusa baadhi ya watendaji wa Serikali baada ya maofisa wanane wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA), akiwemo Kamishna wa Forodha wa mamlaka hiyo Tiagi Masamaki (56) kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutoa makontena 329 bandarini bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 12.7 za kitanzania.




Ukimuondoa Masamaki maofisa wengine waliopandishwa kortini ni Habibu Mponezya (45) Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja,Bulton Mponezya (51) 

  
Wakili wa Serikali Mwandamizi Christopher Msigwa akisaidiana na Peter Vitalis  ameadi leo mchana mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa makosa mawili.



Alidai makosa mawili ya uhujumu uchumi ni kula njama ya kuidanganya Serikali na kuisababishia Serikali hasara. Kesi hiyo ni namba 35/2015 ya uhujumu uchumi.  




Ilidaiwa katika shtaka la kwanza katika tarehe tofauti kati ya Juni 1 na Novemba 17 mwaka huu, sehemu isiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama ya kuidanganya Serikali  kuwa sh. bilioni 12.7 zimetolewa kwa kutoa makontena 329 katika Bandari Kavu ya Azam, baada ya kodi zote kutolewa.




Katika shtaka la pili, washtakiwa wanatuhumiwa katika ya Juni Mosi na Novemba 17 mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam walishindwa kutimiza majukumu yao kwa namna inavyotakiwa na kusababisha Serikali kupata hasara ya sh. bilioni 12.7.




Baada ya washtakiwa hao kusomewa makosa yao, Hakimu Shahidi aliwaeleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo hawatakiwi kujibu chochote kama kweli au si kweli.




Aliongeza kuwa Mahakama Kuu ndiyo inamamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo kama wanataka dhamana wapeleke maombi ya dhamana katika mahakama hiyo.




"Kama mnataka dhamana pelekeni maombi Mahakama Kuu kwa sababu mahakama hii hawezi kutoa dhamana," alisema Hakimu Shahidi 




Hata hivyo, upande wa utetezi ulidai kuwa kesi hiyo ifikishwa mahakamani hapo bila kibali na pia waliomba mshtakiwa namba nne Mrema anamtoto mchanga kwa hiyo wanaiomba mahakama imfikirie.


Wakili Msigwa alidai upelelezi bado unaendelea, wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Kesi hiyo itatajwa Desemba 17 mwaka huu kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika.





Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.